barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
Rais Magufuli alichepuka kidogo kutoka kwenye zulia na kuwafuata wananchi...Akapiga kijembe kidogo kuwa tumewatandika wapinzani huko kwenye uchaguzi,wananchi bado wana imani na CCM na wameitikia wito wa hapa kazi tu.
Hiyo ilikuwa ni mapokezi ya Rais wa Uturuki Ikulu,yaani ilikuwa ni shughuli ya kitaifa,ambapo Rais mwenyewe alisema haihusiani na mambo ya vyama vya siasa.Maana hao wafanyabiashara 150 waliokuja na Rais wa Uturuki hawataangalia CHADEMA wala CCM,wao wamekuja kufanya baishara na watanzania.
Rais aliwahi kusema yanapokuja mambo ya Kitaifa kama haya,ndio maana hawavai sare za vyama bali suti ili kuonyesha kuwa shughuli ni ya KITAIFA na si kichama.Hapa Rais atakuwa "alichomekea tu" kama siku ile alivyochomekea kuwa "Tufyatuane tu" maana atatulipia ada za watoto mpaka elimu ya Upili