VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Ulisema kuwa katika utawala wako huu wa awamu ya tano ya uongozi wa Tanzania, hupendi wananchi wako 'wakudrive'. Kiufupi, hupendi wananchi wako, ingawa ndiyo waliokuchagua na ndiyo mamlaka yako unayowajibika kwayo, wakupangie cha kufanya. Ukasisitiza kuwa kwa jambo linalopigiwa makelele, wewe huwa ndiyo hulifanyi kabisa.
Hupangiwi, hupelekeshwi. Hutaki kelele kama kwenye kilele zinazoweza kuwa za milele. Unataka utulivu. Unataka uamue mwenyewe katika kuteua, kutumbua, kusimamisha, kuhamisha, kuwajibisha au kulinda wasaidizi wako. Unataka uwe huru ili uweze kuiona kuu nuru. Unataka Urais wako unoge kadiri Katiba yetu inavyounogesha.
Rais na Mwenyekiti wangu wa CCM Magufuli, watanzania tumekuwa kimya kuhusu Ndugu Daudi Albert Bashite alias Paul Makonda, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam. Tumekuwa hatumzungumzii wala kukwambia chochote kinachomhusu kwa muda sasa. Tumekuwa tunaepuka 'kuku-drive'. Ukimya wetu hauzai matunda na ukimya wako unatanda.
Bashite hafai. Bashite ni mhalifu wa kijinai kuhusiana na cheti cha kidato cha nne. Bashite amevamia studio za Clouds. Bashite ana utajiri wenye utata na urafiki wake na GSM una ukakasi utiao wasiwasi. Pale GSM, Bashite hufanya shopping bure kabisa kwa consideration isiyojulikana. Rais unajua. Rais tumekwambia kwa njia mbalimbali. Kwa ukimya wako wa kumuondoa Bashite, tuanze tena 'kuku-drive'?
Bastola ya nini tena jamani!?
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam