Rais Magufuli, timua huyu mkurugenzi wa TASAF

SONGOKA

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
1,843
1,841
Hivi hawa TASAF nani aliwambia kugawa pesa eti kwa kaya maskini ndo njia ya kuwaondolea umaskini. Hizi sh 20,000, 50,000, mnazogawa tena mara moja kwa miezi kadhaa zitaondoaje umaskini?

Vikao vyenyewe vya migao vimejaa fujo, majungu na ugomvi, mifano ni Mwanza na Arusha,
Mkurugenzi wa TASAF ameshindwa kubuni mbinu mpya za kusaidia kaya maskini Zaidi ya kuwapa hivyo visenti au ni mpango mnaoutumia kupiga pesa . Tunawajua sana mchezo wenu wa kugawa kwa kaya kadhaa alafu vitabu vyenu vinaonyesha mara mia ya idadi halisi.

Magufuli watu waliokosa ubunifu kama huyu mkurugenzi wa TASAF ni wa kutimuliwa since YESTERDAY.
 
Hao Tasaf hizo hela za kugawa wanazitoa wapi??

Au ni hizi kodi zetu wanazotukamua huku mitaani??
 
TASAF ni jipu, nishawahi kufanya kazi kwa mda mfupi katika hii taasisi, asee ni kichaka cha wapiga deal na ufisadi wa kutisha...
 
Hivi hawa TASAF nani aliwambia kugawa pesa eti kwa kaya maskini ndo njia ya kuwaondolea umaskini. Hizi sh 20,000, 50,000, mnazogawa tena mara moja kwa miezi kadhaa zitaondoaje umaskini?

Vikao vyenyewe vya migao vimejaa fujo, majungu na ugomvi, mifano ni Mwanza na Arusha,
Mkurugenzi wa TASAF ameshindwa kubuni mbinu mpya za kusaidia kaya maskini Zaidi ya kuwapa hivyo visenti au ni mpango mnaoutumia kupiga pesa . Tunawajua sana mchezo wenu wa kugawa kwa kaya kadhaa alafu vitabu vyenu vinaonyesha mara mia ya idadi halisi.

Magufuli watu waliokosa ubunifu kama huyu mkurugenzi wa TASAF ni wa kutimuliwa since YESTERDAY.

Dunia nzima huu utaratibu uko Tanzania tu

Badala yake TASAF wangewaorodhesha wote wasikuwa na uwezo na kuwakatia bima ya afya huko ndiko kuna matatizo makubwa kwa hawa masiokuwa na kipato.
 
good idea mkuu, hivi visenti wanawapa ni mpango wao tu wa kupiga pesa
 
Bora kambi za kuzalisha za Stalin kuliko hayo mambo ya kugawia watu pesa. Asilimia kubwa wanatumia vibaya. Wakijua kuzalisha itakuwa bora zaidi
 
Yaani hata mimi huwa nashangaa. Hawa jamaa lazima wanapiga sana pesa. Utaondoaje umaskini kwa kumwaga pesa. Kuna miradi hovyo kabisa.
 
hamna kodi ya Mtanzania hata 1 wala serikali kwenye hela za Tasaf-sasa unataka kuwapangia wanaokupa pesa,moja ya mashariti ya hizo hela ni kuzigawa kwa kaya masikini.ni kama zilivyo hela za UNCEF nazo huwa zina mashariti hivyo hivyo wanakupangia shughuli za kufanya.ukitaka kuondokana na hayo yote mwambie boss wako magufuli ajenge uchumi wa nchi.na sio kumpangia anayekupa pesa bure
 
TASAF ni jipu, nishawahi kufanya kazi kwa mda mfupi katika hii taasisi, asee ni kichaka cha wapiga deal na ufisadi wa kutisha...
ni kweli ufisadi unaweza kuwepo kwa namna moja au nyingine lakini sio kama anavyosema mtoa mada kuwa watafute njia nyingine na sio kugawa kwani hili haliwezekani kwa sababu ni mashariti ya watoa pesa kuwa fedha zigawiwe kwa masikini
 
Umaskini hauondolewi kwa kuwagawia watu pesa...

hizo hela ni bora wangewajengea viwanda vidogo vidogo vya kuongezea mazao thamani katika kila kata. Hili lingewaongezea hizi kaya kipato.

pia kuwapa watu hela "cash" kunajenga mianya mikubwa ya ubadhirifu... kwanini hawajawa wabunifu kwa kuwapatia bima za afya? maana kwa kaya za vijijini matumizi makubwa yapo katika suala zima la afya.
 
hamna kodi ya Mtanzania hata 1 wala serikali kwenye hela za Tasaf-sasa unataka kuwapangia wanaokupa pesa,moja ya mashariti ya hizo hela ni kuzigawa kwa kaya masikini.ni kama zilivyo hela za UNCEF nazo huwa zina mashariti hivyo hivyo wanakupangia shughuli za kufanya.ukitaka kuondokana na hayo yote mwambie boss wako magufuli ajenge uchumi wa nchi.na sio kumpangia anayekupa pesa bure
UKATAE, UKUBALI, TASAF INANUKA RUSHWA FULSTOP. Halmashauri karibu zote wahasibu waliopata nafasi ya kusimamia hela za TASAF kwa kipindi husika walifanya mambo yasiyoendana na mishahara yao ( Wanakuambia ni neema ).
 
hamna kodi ya Mtanzania hata 1 wala serikali kwenye hela za Tasaf-sasa unataka kuwapangia wanaokupa pesa,moja ya mashariti ya hizo hela ni kuzigawa kwa kaya masikini.ni kama zilivyo hela za UNCEF nazo huwa zina mashariti hivyo hivyo wanakupangia shughuli za kufanya.ukitaka kuondokana na hayo yote mwambie boss wako magufuli ajenge uchumi wa nchi.na sio kumpangia anayekupa pesa bure
usitake kutudangany hapa, husiwezi kupewa pesa za mradi alafu mtoa pesa ndo akakuandikia project proposal, aka outline goals, objectives, activities, outputs Na outcomes then akakukabidhi Na pesa.
TASAF hiyo ilikuwa idea Yao, Na inaonyesha udhaifu mkubwa Sana Katika kiwango chao cha ubunifu
 
Mtoa mada ungechukua muda na militia website ya TASAF ukajielimisha juu ya mradi huu halafu ukaja na hoja zenye mashiko kuukosoa. Unapotosha watu; miradi kama hii imefanikiwa nchi za Latin America na hizi so fedha za serikalini(kodi). Mradi una mambo mengi na kugawa fedha (condition cash transfers) ni sehemu tu ya mradi. Hebu kasome kuhusu Condition cash transfer halafu pitia website ya TASAF usome kuhusu Productive social safety net halafu uje na hoja za kuukosoa.
 
nimesomaa website yao mkuu, nachokuhakikishia huu mradi wa kugawa pesa ni kichaka cha ufisadi, alafu hata kama pesa sio ya walipa kodi siyo justification ya kuzifisadi hizo pesa.
Najua kuna wafanya kazi wa TASAF humu (maybe ur among them) lakini penye ukweli lazima tusema. Walengwa wenyewe wanalalamika kila siku kuwa pesa zinaenda kwa wasiokusudiwa, pia kuna variance kati ya wanaogawia na idadi inayotolewa report

umaskini hauishi kwa kupewa pesa, umaskini unaisha kwa kutengeneza njia endelevu za kupata pesa
 
usitake kutudangany hapa, husiwezi kupewa pesa za mradi alafu mtoa pesa ndo akakuandikia project proposal, aka outline goals, objectives, activities, outputs Na outcomes then akakukabidhi Na pesa.
TASAF hiyo ilikuwa idea Yao, Na inaonyesha udhaifu mkubwa Sana Katika kiwango chao cha ubunifu
basi kuondoa ubishi kama upo dar nenda makao makuu ya Tasaf pale nyuma ya water front kaulize kwa nini hizo pesa wanagawa badala ya kuiweka katika mfumo mwingine ambao utamusaidia mtu kutogawiwa tena pesa,alafu utuletee mtrjrsho hapa jamvini-kama kweli una nia ya kutaka kujifunza na kujua mambo.
pili nenda halmashauri yoyote ambayo wanapata fedha za unicef onana na waratibu wa mfuko wa uncef kwenye halmashauri husika waulize ni kwa nini hizo fedha unafanyiwa kazi hii na sio ile
 
nimesomaa website yao mkuu, nachokuhakikishia huu mradi wa kugawa pesa ni kichaka cha ufisadi, alafu hata kama pesa sio ya walipa kodi siyo justification ya kuzifisadi hizo pesa.
Najua kuna wafanya kazi wa TASAF humu (maybe ur among them) lakini penye ukweli lazima tusema. Walengwa wenyewe wanalalamika kila siku kuwa pesa zinaenda kwa wasiokusudiwa, pia kuna variance kati ya wanaogawia na idadi inayotolewa report

umaskini hauishi kwa kupewa pesa, umaskini unaisha kwa kutengeneza njia endelevu za kupata pesa
Mkuu usichanganye mambo; hata miradi yenye manufaa sana kama ujenzi wa barabara, zahanati nk. inaweza kugeuka kichaka cha mafisadi na kuwa na malalamiko. Mbona huongelei faida za mradi kama watoto kuhudhuria shule, watoto chini ya miaka 5 kuhudhuria kliniki na financial literacy training zinazotolewa kwa wananchi. Malengo ya fedha sio kuondoa umaskini rejea maana ya condition cash transfer=
 
basi kuondoa ubishi kama upo dar nenda makao makuu ya Tasaf pale nyuma ya water front kaulize kwa nini hizo pesa wanagawa badala ya kuiweka katika mfumo mwingine ambao utamusaidia mtu kutogawiwa tena pesa,alafu utuletee mtrjrsho hapa jamvini-kama kweli una nia ya kutaka kujifunza na kujua mambo.
pili nenda halmashauri yoyote ambayo wanapata fedha za unicef onana na waratibu wa mfuko wa uncef kwenye halmashauri husika waulize ni kwa nini hizo fedha unafanyiwa kazi hii na sio ile
mkuu nimefanya kazi UN agencies mbili tofauti kama meneja mradi, so nna uzoefu wa kutosha wa namna miradi inavyoendeshwa

Huwezi badilisha matumizi ya pesa katikati ya mradi kwa sababu pesa hutolewa baada ya donor kupitia andiko la mradi na kulilidhia, kwa hali hiyo pesa zitatumika kutekeleza majukumu ya mradi mliokubaliana na donor na si vinginevyo. Ingawa kuna miradi ambayo mnapofanya mid evaluation mnaweza kukubaliana na donor kubadili baadhi ya activities.

Lakini anayeandaa andiko la mradi ni recipient, na ndo anaandaa activities za mradi, kwa iyo TASAF hawakwepi hii lawama
 
Back
Top Bottom