Rais Magufuli timiza ahadi yako ya kumpatia ajira Joshua Nassari

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
18,921
31,155
Mheshimiwa Rais Dr John Pombe Magufuli wakati wa kipindi cha kampeni ulitoa ahadi ya kumpatia kazi kijana wetu mpendwa Joshua Nassari.

Muda unakwenda kasi sana tangu kampeni zimalizike na wewe kuibuka na ushindi wa kishindo.Kijana wetu wetu ana mtoto ambae anahitaji matunzo ya kiwango cha nafasi za juu za kiserekali kama Regional Commissioner au High Commissioner au Mkuu wa shirika lolote zuri la umma kama NSSF, PSPF, TANAPA, NCAA, CRDB, KADCO, TANESCO, TANROAD, UWASSA,TBC, na NK.

Kijana wetu Nassari alishiriki kikamilifu kampeni hadi ukapata ushindi wa kishindo,hata kama yule jamaa wa ubelgiji anasema kulikuwa na kosoro nyingi lakini wewe sasa ni Rais wa JMT.Kwa nafasi yako una nafasi kibao kuanzia serekali kuu,serekali za mitaa,mawizara kibao,nafasi za ubunge 10 jimbo la Ikulu.Najua una shughuli nyingi kiasi unaweza kusahau ebu tupia jicho kama ikishindikana basi mpatie nafasi ya RAS kijana asiteseke na kusahaulika.

Wasalamu Ngongo safarini Chato National Park.
 
Nassari ameapa kuwa kama hadi March mosi hajapewa kazi atahama nchi na akifika mbele ndiyo ataiumbua CCM na ataeleza yote yaliyo nyuma ya pazia kuanzia biashara ya kununua wabunge wa upinzani hadi hawa covid 19, na kwa jinsi anavyozungumza kwa hisia kali atafanya kweli.
 
Mh.Rais sidhani kama yupo tayari kutishwa eti huyo Nassari atatoboa siri na ieleweke hapangiwi cha kufanya...atakalolifanya analijuwa mwenyeweg.
Nassary dont try to fool nambari one and the citizens at large
 
Tukumbuke Kijana wetu aliunga mkono juhudi bila kile chama cha sera ya uhuru haki na maendelea kugundua.Isitoshe Silinde aliunga mkono juhudi siku za karibuni lakini kazawadiwa uNaibu Waziri huwezi kumlinganisha na Nassari aliunga mkono juhudi kisayansi zaidi.
 
Back
Top Bottom