Rais Magufuli: Tetemeko halijaletwa na Serikali, watu wafanye kazi

Sio kila tamko lazima tulifikirieeeee saaaana!!! Mengine unayapuuza maisha yanasonga mbele!!
 
HOTUBA YA RAIS DKT MAGUFULI BAADA YA KUPOKEA TAARIFA YA MAAFA YA TETEMEKO LA ARDHI KAGERA,KIPINDI,SEPT 17,2016

 
Hotuba imerudiwa jpili channel 10. I am bit disappointed na miss-interpretation ya hotuba ya mkulu kwenye huu uzi. Kwa mwendo huu JF iaanza kua a mere political propaganda platform na sio great thinkers platform kama ilivyokua. Wengi tunakuja JF kupata breaking/update news bila kijali political ideology ya mtu. Kwa walioisikia hotuba yote ya mkulu, mengi kazungumza, but is just not right kutumia sentensi moja negatively katika 30mins speech. Moderators tunaomba kwa credibility ya JF habari iwe inakua scrutinised kabla haijawa posted.

Mkuu, wengi wao ndio walivyo - shedding crocodile tears!
 
Kwa hiyo allihairisha safari ya Zambia kwa maneno ya kejeli kama haya kwa wahanga?
Rais anatakiwa awafariji wafiwa sio kuwasimanga
Yaani vifo va zaidi ya watu 15 ndiyo Rais anatoa maneno ya hovyo hovyo kama haya?
Unamnakili baba yako Mbowe. Akenda hata Mkuu wa mkoa ndio Rais kaenda. Hakuna siasa za kujionyesha hapa. Ukisikia tetemeko mahali unakimbia mbio huko na kuleta siasa. Siku moja hao wanasiasa wenu watakuja chooni kukuchokonoa mavi kwa sababu hayatoki. Misaada ya serikali inaratibiwa na responsible kwa wananchi wake tofauti na hao mamc@ washereheshaji wa kusaka kura kwenye maafa maana kila wakisikia maafa hao mbioooo na kuwaambia wananchi siasa maji taka
 
naona hataki mbowe ndio amlazimishe kwenda wakati yeye ana taratibu tofauti kushughulikia tetemeko sio kwenda kuuza sura umbea na fitna bukoba.
 
Unamnakili baba yako Mbowe. Akenda hata Mkuu wa mkoa ndio Rais kaenda. Hakuna siasa za kujionyesha hapa. Ukisikia tetemeko mahali unakimbia mbio huko na kuleta siasa. Siku moja hao wanasiasa wenu watakuja chooni kukuchokonoa mavi kwa sababu hayatoki. Misaada ya serikali inaratibiwa na responsible kwa wananchi wake tofauti na hao mamc@ washereheshaji wa kusaka kura kwenye maafa maana kila wakisikia maafa hao mbioooo na kuwaambia wananchi siasa maji taka
Akili mtope hizi
Wapiga kura wa MAGUFULI zaidi ya 16 wamekufa then ww unatuletea porojo kuwa RC anamuwakilisha Rais?
Punguzeni utoto wenu wa vyama tunapo jadili mambo ya maana tafadhali
 
Serikali iwasaidie lakini si vizuri kuwapa ahadi hewa hasa kujenga nyumba zao. Labda serikali iwaondolee kodi kwenye vifaa vya ujenzi hasa cement, bati na nondo
Nahili ndio lingekuwa swala muhimu kufanya kwa wakati huu kwani hata hizo bati na cement zilizochangiwa kama pakiwekwa msamaha wa kodi kwa hiyo bill.3 inaweza piga tafu kubwa kwa waathirika kurejesha makaz yao serikali ishughulike na miundombinu ya umma iliyoharibika
 
Hatimaye mkuu kazungumza japo kwa kuchelewa sana. Ila naomba niulize: hivi inawezekana kukawa na watu wanaoamini kuwa "tetemeko limeletwa na serikali" mpaka mkuu atake wananchi wafahamishwe kuhusu hilo?
Anajua wengi huko mtaani nahumu mtandaoni wanaamini hivyo that's y kasema hivyo....kule mbeya watu waliishukuru serikali kwa kuwapelekea mwezi wakaomba upelekwe tena mwaka ujao....xo lipo wazii kabisa hilo
 
Hatimaye mkuu kazungumza japo kwa kuchelewa sana. Ila naomba niulize: hivi inawezekana kukawa na watu wanaoamini kuwa "tetemeko limeletwa na serikali" mpaka mkuu atake wananchi wafahamishwe kuhusu hilo?

Anamaana kuwa, unapokaa na kuisubiri serikali ilete msaada (Ambao unakuwa unasubiriwa kama fidia) inakuwa na mantiki ya as if serikali ndo imesababisha hilo tetemeko.
Kwakuwa, nyumba imeanguka, ni kweli kuna watu watakuwa hawana namna ya kujisaidia, lakini kwa wale wenye namna ya kujisaidia kwa kurekebisha nyumba zao, ni vyema wafanye hivyo kwa kuwa hili ni janga na lisitumike tofauti.
 
Hilo la kusema watu wajiongeze wasisubir serikal ni ukwel fulan mchungu ambao hatuwez kuukubali.
Kwa maana kuna mtu anaweza kua na ufa tu Ila akakaa kusubir....
As long as una uwezo wa kufanya kitu fulan basi uanze nacho.

Rais amesema ukweli. Kagera ina watu wengi sana na ina wasomi wa kutosha. Ukitathmini kwa undani unaweza ukawatenga waathirika katika makundi yafuatayo:

1) Kundi la Familia ya Watu Maskini kabisa, kama wazee wanaoishi peke yao au na watoto wadogo baada ya wazazi wao kuwaterekeza au kutangulia mbele ya haki, Hawa hawana mahala pa kupata msaada wowote
2) Kundi la Familia ya Watu wasio na kipato cha kila siku, Maisha yao wanayaendesha kwa kazi za mikono, hivyo nguvu ya kufanya kazi wanayo.
3) Kundi la Familia ya Watu wenye kipato cha kati. Wanafanya kazi na kupata mshahara kila mwezi
4) Kundi la Familia zinazojiweza. Zina watoto wasomi na wanauwezo wa kusaidia kujenga makazi mapya hata bila msaada wa serikali.

Kwa kuzingatia mahitaji, Kundi la kwanza linahitaji msaasa zaidi wa kujengewa nyumba. Kundi hili bila serikali kulisaidia itakuwa haijatenda haki.

Kundi la pili, nalo linahitaji msaada lakini si kujengewa nyumba. Kundi hili wasaidiwe vifaa vya ujenzi ili waweze kurekebisha nyumba zao kwa nguvu zao wenyewe.

Kundi la tatu, linaweza kusaidia kwa kiwngo tu kama fidia. Wote wanaweza wakapewa pesa kiasi fulani ili kuwasaidia kurekebisha nyumba zao.

Kundi la nne, halihitaji msaada wowote. Wanafamilia wanao uwezo wa kujenga au kurekebisha nyumba iliyoharibika.

Hivyo serikali inabidi itulie na ifanye tathmini ya kutosha ili kutambua familia zilizoathirika na kuzitenga katika makundi wakati wa kutoa msaada. Ikikosea ikakurupuka tu na kuanza kugawa misaada kiholela, kitakachotokea ni malalamiko mengi na wananchi kuichukia serikali yao.
 
Hatimaye mkuu kazungumza japo kwa kuchelewa sana. Ila naomba niulize: hivi inawezekana kukawa na watu wanaoamini kuwa "tetemeko limeletwa na serikali" mpaka mkuu atake wananchi wafahamishwe kuhusu hilo?
Mkuu jibu lako liko hivi, inaezekana na ndivyo ilivyo ila watu wanapunguza makali ili kujiepusha na mikosi zaidi... nikuulize kaswali kwani sasa hivi serikali ni nani? majanga asili yake nini? kwa nini yanatokea? kwa ufahamu wangu mdogo ambao hata vitabu vya dini vinaelezea ni kwamba Mambo hayo yanatokea kwa kutokua na mahusiano mazuri kati ya MUNGU/MIUNGU NA TAWALA AMA JAMII YOTE ILIYOPO KTK TAWALA HUSIKA.. KWANINI JAMII INANYOOSHA KIDOLE KWA MTAWALA, HII NI KWASABABU MTAWALA NDIO LANGO KUU KATI VIWILI HIVYO.
 
Ni kweli watu wasisubiri kujengewa,, ila kwa kauli kama hyo isee wakati kuna watu wanalala nje wengine wamefiwa na ndugu wa familia inahuzunisha ki ukweli,, we will miss you edward ngoyai lowassa SEE YOU AGAIN
 
kwa uwelewa wangu michango ilikuwa inaenda kuwasaidia wahanga wa tetemeko kama ujenzi wa nyumba zao zilizoharibika, chakula na matibabu pamoja na ujenzi wa shule na huduma zingine muhimu. Kama kulikuwa na mpango tofauti na huo ni bora wachangiaji wangepewa tarifa mapema kabla yakuchangia. nasema hivi kwa sababu makazi ni kitu muhimu kwa kila mtu. mtu anawezaje kwenda kazini wakati familia iko nnje, hilo linaweza kumuathiri hata kisaikolojia. Ushauri wangu kwa serikali ifanye uhakiki wa kila kaya na uaribifu uliotokea kwenye nyumba zao, ili wajue kila kaya itahitaji mifuko mingapi ya cement na matofali , hili linawezekana wakiongea na makampuni ya cement wakatoa mifuko hiyo kwa punguzo la bei alaf michango ikatumika kuwanunulia hivyo vitu hata kama wao wapambane na ela za kuwalipa mafundi wa ujenzi litakuwa jambo zuri sana.

Kwa kweli sina milioni saba ya kulipa... Ila Mkuu ana maneno mazito! Anasema waathirika wasikae tu huko wanangoja hela za serikali kwa sbb wanasikia zimechangwa,waanze kujisaidia kwanza wao na serikali itawasaidia pale waliposhindwa.

Mkuu anasema mtu ukuta umedondoka, anataka asubiri serikali ndio imtengenezee! Watu wajue tetemeko ni janga la asili halijaletwa na CCM. Waanze kwa kujenga wenyewe kuta zilizodondoka sio wasubiri serikali, sababu maisha yanendelea na watu wanatakiwa wafanye kazi kwa kujenga nyumba zao na sio kila kitu serikali itafanya.

Na wale wanasiasa wanaotaka kutumia janga hili kujinufaisha kisiasa mkuu anasema waache mara moja.

Na kasema wote wanaotumia janga hili kukusanya misaada kwa njia ya kitapeli, basi wakamatwe mara moja.

=======

Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amepokea taarifa ya maafa yaliyosababishwa na tetemoko la ardhi lililotokea katika Mkoa wa Kagera na mikoa jirani ya Mwanza, Geita na Mara kutoka kwa Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, Ikulu DSM.

Magufuli%20tetemeko1.JPG

Rais Magufuli akipokea taarifa pamoja na misaada iliyochangwa na nchi jirani

Pamoja na kupokea taarifa hiyo Rais Magufuli amepokea mchango wa fedha taslimu kiasi cha Dola za Kimarekani laki mbili (USD-200,000/-) sawa na takribani Shilingi za Kitanzania Milioni Mia nne na therathini na saba (Tshs-437,000,000/-) kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni na pia amepokea taarifa ya mchango wa mabati, blanketi na magodoro vyenye thamani ya Shilingi za Kitanzania milioni 115 kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera.

Katika taarifa yake Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amesema tetemeko hilo limesababisha vifo vya watu 17, majeruhi 440, nyumba 2063 zimeanguka, nyumba 14,081 zipo katika hali hatarishi na nyumba 9,471 zimepata uharibifu mdogo, huku watu 126,315 wakihitaji misaada mbalimbali.

Mhe. Waziri Mkuu ameongeza kuwa Serikali imechukua hatua mbalimbali zikiwemo kupeleka chakula, huduma za matibabu na hifadhi za dharura kwa waathirika na pia inaratibu ukusanyaji wa michango kutoka sehemu mbalimbali ambapo mpaka sasa kiasi cha Shilingi za Kitanzania Bilioni tatu nukta sita (Tshs Bilioni 3.6) zimepatikana.

Akizungumza baada ya kupokea taarifa ya maafa na michango kwa ajili ya waathirika wa maafa hayo, Rais Magufuli amewashukuru wote waliojitoa kusaidia waathirika wakiwemo Marais Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda, Mhe. Uhuru Kenyatta wa Kenya na Paul Kagame wa Rwanda ambao wamempigia simu za kumpa pole na tayari wametoa misaada yao, na pia nchi mbalimbali, mashirika, wafanyabiashara, watumishi wa umma na watu binafsi na amesema michango hiyo ina umuhimu mkubwa katika kukabiliana na athari za maafa haya.

Dkt. Magufuli ametoa wito kwa Watanzania na wote walioguswa na maafa haya kuendelea kutoa misaada kwa waathirika kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, huku akionya na kuvitaka vyombo vya dola kuwafuatilia watu wanaotaka kutumia maafa haya kukusanya michango kwa lengo la kujinufaisha.

Rais Magufuli amebainisha kuwa Serikali itahakikisha inarekebisha miundombinu iliyoharibika zikiwemo shule, vituo vya matibabu, barabara na huduma nyingine za kijamii na pia ametaka wananchi waliokumbwa na madhara ya tetemeko hususani nyumba zilizobomoka, wajipange kurekebisha nyumba zao kwa kuwa Serikali pekee yake haitaweza kujenga nyumba zote zilizobomoka.

Aidha, Rais Magufuli amewasihi Watanzania kuwapuuza watu wanaotaka kutumia maafa haya kueneza uchonganishi na chuki dhidi ya Serikali na ameweka wazi kuwa mpaka sasa hakuna teknolojia ya kutabiri kutokea kwa tetemeko la ardhi na kwamba tetemeko hili halikuletwa na Serikali.

Dkt. Magufuli amesema hata mataifa makubwa yenye maendeleo makubwa ya uchumi na teknolojia yanakumbwa na tetemeko la ardhi na kusababisha vifo vya idadi kubwa ya wananchi na uharibifu mkubwa wa mali.

"Nilikuwa najaribu kuangalia kwa mfano nchi kama China kwenye mwaka 2014 watu 617 walipoteza maisha, Mwaka 2013 walipoteza watu 193, Mwaka 2010 walipoteza watu 2,998 Mwaka 2008 China ilipoteza watu 98,712.

Ukijaribu kuangalia Japan, nchi ambayo imeendelea na ina utaalamu wa hali ya juu sana, kwenye mwaka 2016 tarehe 14 mwezi wa nne ilipoteza watu 6, baada ya siku mbili tarehe 16 mwezi wa nne 2016 tetemeko likatokea tena na likaua watu 35, mwaka 2012 likaua watu 3, mwaka 2011 likaua watu 15,904 mwaka 2008 likaua watu 12, mwaka 2007 likaua watu 11, mwaka 2004 likaua watu 40, mwaka 1923 liliua watu 142,800 na hiyo ni Japan. Amesisitiza Rais Magufuli.

Shughuli ya kupokea taarifa ya Waziri Mkuu na michango kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera na Mikoa jirani imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt Suzan Kolimba, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Balozi wa Uganda nchini Tanzania Mhe. Dorothy Hyuha na Naibu Balozi wa Kenya nchini Tanzania Mhe. Boniface Muhia.


Chanzo: IPP Media
 
Back
Top Bottom