Rais Magufuli, Tengua uteuzi wa Mbunge mmoja mwanaume umteue Aggrey Mwanry na kisha umteue waziri wa Nishati na Madini

Freed Freed

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
6,198
6,416
Habari zenu familia ya JF. Mi sio mnafiki wala sina undugu na wala ukabila na Agrey Mwanry. Wote mtakubali hii ni nyota iliyozimwa na Mafuriko ya UKAWA.

Sahivi ni RC Tabora na anafanya mambo mazuri tu ikiwa ni pamoja na mkoa wake kuvuka lengo ktk kutengeneza Madawati kwa shule za Msingi.

Pia alipokuwa Naibu waziri TAMISEMI alikuwa akifanya kazi vizuri sana kuliko hata waziri Kasim Majaliwa aliyekuwa juu yake.

Hivyo kwa heshima na taadhima namshauri Rais kama atapita humu, atengue uteuzi wa Mbunge mwanaume na kumpa Mwanry nafasi hiyo ili baada ya hapo ateuliwe Waziri wa Nishati na Madini.

Nafasi ya RC Tabora apewe mtu mwingine na Mbunge aliyetenguliwa uteuzi wake apewe pia kazi nyingine.

Agery Mwanry alikuwa Mbunge wa Siha- Kilimanjaro kabla ya kusombwa na mafuriko ya UKAWA mwaka 2015.

Naomba ushauri wangu ufanyiwe kazi. Naomba kuwasilisha.
 
Inawezekana wazo zuri lakini mimi ni msomaji mzuri sana wa katiba! Sijaona sehemu inayompa mamlaka rais kutengua uteuzi wa mbunge ingawaje, wanasheria nao, katika mazingira kama haya hawakawii kusema "...na hakuna kipengele kinachomzuia kufanya hivyo!"

Lakini shida yote hiyo ya nini?! Si wanaweza tu kutumia kale kamchezo kao ka "eliminate the threat" kama ambavyo yule wa kule walivyotaka kum-eliminate juma moja lililopita lakini Mungu akagoma kutoa funguo kwa shetani!

Lakini katika hili, badala ya kuwa "eliminate the threat" inakuwa "eliminate the barrier!" Unachinja Kondoo asiye na kosa na kuwapa mizimu damu ili hatimae shughuli za jadi zifanyike! Lakini nadhani hili lingeweza kufanyika zaidi kama ushauri wako ingekuwa ni kwa kum-favor yule Zirail aliyeonekana karibu na Segera akielekea kule kwenye mlima mrefu zaidi Afrika!

Katika hili nasikia hawa jamaa ni wazuri kweli! Huo ushauri wako ni wa kibinadamu zaidi lakini utahojiwa uhalali wake kisheria! Chambilecho mimi muumiani mnywa damu, ya nini kuniletea matembele ili nikufanyie shughuli yako! Nawe si ni muumiani mwenzangu bhana! Tuchinje tu mbuzi, tunywe damu, tupongezane na hatimae karamu ipite! Simple!
 
Habari zenu familia ya JF. Mi sio mnafiki wala sina undugu na wala ukabila na Agrey Mwanry. Wote mtakubali hii ni nyota iliyozimwa na Mafuriko ya UKAWA. Sahivi ni RC Tabora na anafanya mambo mazuri tu ikiwa ni pamoja na mkoa wake kuvuka lengo ktk kutengeneza Madawati kwa shule za Msingi. Pia alipokuwa Naibu waziri TAMISEMI alikuwa akifanya kazi vizuri sana kuliko hata waziri Kasim Majaliwa aliyekuwa juu yake. Hivyo kwa heshima na taadhima namshauri Rais kama atapita humu, atengue uteuzi wa Mbunge mwanaume na kumpa Mwanry nafasi hiyo ili baada ya hapo ateuliwe Waziri wa Nishati na Madini. Nafasi ya RC Tabora apewe mtu mwingine na Mbunge aliyetenguliwa uteuzi wake apewe pia kazi nyingine. Agery Mwanry alikuwa Mbunge wa Siha- Kilimanjaro kabla ya kusombwa na mafuriko ya UKAWA mwaka 2015. Naomba ushauri wangu ufanyiwe kazi. Naomba kuwasilisha.
Wewe humtakii mema Bulembo maana ubunge wake unanyemelewa na wengi akiwemo yule kijana almaarufu wa jiji la Mzizima anayetajwatajwa kwenye new cabinet!
 
Habari zenu familia ya JF. Mi sio mnafiki wala sina undugu na wala ukabila na Agrey Mwanry. Wote mtakubali hii ni nyota iliyozimwa na Mafuriko ya UKAWA. Sahivi ni RC Tabora na anafanya mambo mazuri tu ikiwa ni pamoja na mkoa wake kuvuka lengo ktk kutengeneza Madawati kwa shule za Msingi. Pia alipokuwa Naibu waziri TAMISEMI alikuwa akifanya kazi vizuri sana kuliko hata waziri Kasim Majaliwa aliyekuwa juu yake. Hivyo kwa heshima na taadhima namshauri Rais kama atapita humu, atengue uteuzi wa Mbunge mwanaume na kumpa Mwanry nafasi hiyo ili baada ya hapo ateuliwe Waziri wa Nishati na Madini. Nafasi ya RC Tabora apewe mtu mwingine na Mbunge aliyetenguliwa uteuzi wake apewe pia kazi nyingine. Agery Mwanry alikuwa Mbunge wa Siha- Kilimanjaro kabla ya kusombwa na mafuriko ya UKAWA mwaka 2015. Naomba ushauri wangu ufanyiwe kazi. Naomba kuwasilisha.
Wewe ni nani haswa mpaka umuelekeze cha kufanya?
 
Inawezekana wazo zuri lakini mimi ni msomaji mzuri sana wa katiba! Sijaona sehemu inayompa mamlaka rais kutengua uteuzi wa mbunge ingawaje, wanasheria nao, katika mazingira kama haya hawakawii kusema "hakuna kipengele kinachomzuia kufanya hivyo!"

Lakini shida yote hiyo ya nini?! Si wanaweza tu kutumia kale kamchezo kao ka "eliminate the threat" kama ambavyo yule wa kule walivyotaka kum-eliminate juma moja lililopita lakini Mungu akagoma kutoa funguo kwa shetani!

Lakini katika hili, badala ya kuwa "eliminate the threat" inakuwa "eliminate the barrier!" Unachinja Kondoo asiye na kosa na kuwapa mizimu damu ili hatimae shughuli za jadi zifanyike! Lakini nadhani hili lingeweza kufanyika zaidi kama ushauri wako ingekuwa ni kwa kum-favor yule Zirail aliyeonekana karibu na Segera akielekea kule kwenye mlima mrefu zaidi Afrika!

Katika hili nasikia hawa jamaa ni wazuri kweli! Huo ushauri wako ni wa kibinadamu zaidi lakini utahojiwa uhalali wake kisheria! Chambilecho mimi muumiani mnywa damu, ya nini kuniletea matembele ili nikufanyie shughuli yako! Nawe si ni muumiani mwenzangu bhana! Tuchinje tu mbuzi, tunywe damu, tupongezane na hatimae karamu ipite! Simple!
Hapa nimekuelewa, japo hekima kiasi yahitajika hapa kueleweka ulichosema.
 
Wabunge wa kuteuliwa na Rais kisheria na kikanuni wanaweza kusitishiwa Ubunge wao na Rais kweli? Baada ya kuapishwa?
 
Yaani kaka Freed Freed unataka kutuambia kuwa katika wabunge wote wa CCM waliopo (Zaidi ya 300) hakuna hata kichwa kimoja kinachofaa kuwa Waziri wa Madini? Kiasi kwamba mtu mmoja avuliwe ubunge kisha Mwanry ndio ateuliwe ubunge kisha Waziri wa Madini

Kweli Tanzania tuna kazi kubwa
 
Sijasoma comments za watu,kiukweli huyu mwanry ni mtendaji bora,sio mnafiki,Na hana kujipendekeza,Mimi mwenyewe nilifalijika alivyopewa u RC,Ila jamaa can deliver more than that.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom