Rais Magufuli tafadhali mulika TCRA

Randy orton

JF-Expert Member
Apr 29, 2019
1,338
3,541
Rais J.P.M amefanya mengi sana tangia ameingia madarakani, hilo ni jambo la kushukuru kwa kila mwenye nia ya dhati ya maendeleo ya taifa letu.

Kuna sehemu moja tuu ambayo naona kuwa imesahaulika na imeshindwa kabisa kuendana na sera ya Rais ya kuwakumbatia wanyonge, sehemu hiyo sio nyingine bali ni TCRA,.

Kila siku bei za vifurushi zinapanda tuu , nakumbuka wakati wa Kikwete Bunge la South Africa waliitolea mfano Tanzania kwa kuwa na gharama ndogo za vifurushi vya mtandao, tulipata sifa kedekede...

Tukawa mfano kwa nchi nyingine, lakini kadri muda unavyoenda gharama zinaongezeka tuu, makampuni ya simu yamegeuka wanyonya damu, TCRA wapo tuu ili hali hiyo ndiyo mamlaka husika ya kuzibana kampuni za simu, tume ya ushindani pia imekaa tuu kuona watu wanavyopandishiwa gharama za maisha na haya makampuni ya simu !!

Kuna muda najiuliza, je huu ni mpango kabambe wa kupandisha gharama ili ionekane awamu hii maisha yamekuwa magumu?, mbona wenzetu gharama zinakuwa ndogo wakati kwetu zinazidi?

Kwa nia ya dhati kabisa naomba hii mamlaka, wizara husika na tume ya ushindani wamulikwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi nashangaa yaani unakuta haya malalamiko ya wananchi kuhusu makampuni ya simu hayatiliwi maanani hata kidgo wngne kila ukiweka vocha haikai dk 15 umekatwa sh kadhaa bila hata sabab ya msingi daaaah fvxken tuu

yess BiShoo haswaaAaa
 
Back
Top Bottom