Rais Magufuli, so far, is the best president this country has ever had. Msikivu, ana upendo na huruma. Atabarikiwa sana. Tanzania itabarikiwa!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,468
113,582
Wanabodi

ANGALIZO:

Naomba kuanza bandiko hili kwa angalizo, kuna watu humu wana allergy kila rais Magufuli akisifiwa na kupongezwa kila ananapofanya jambo zuri, au jambo jema lolote, wao wanakasirika, hivyo rais Magufuli akipongezwa kwa mazuri yoyote au mafanikio yoyote, wao wananuna, wanaumia, wanakasirika na kubeza kwa sababu wanatamani rais Magufuli na serikali yake, ashindwe ili wakosoe, wabeze na kutukana. Ukimpongeza tuu rais Magufuli kwa lolote, utawasikia kuwa huku sii kupongeza bali ni kujipendekeza, kujikomba kuusaka uteuzi, u-DC, au kusaka shavu au mara hizi ni njaa tuu za jina la Mayalla!!. Kama wewe ni mtu wa kundi hili, nakuomba uishie hapa ili nisije kukuharibia siku yako ya Jumapili ya leo na kuianza Jumatatu ya kesho kwa kisirani.

Pongezi za Kweli na za Dhati.
Kiukweli tunapompongeza rais wetu Magufuli, sio wote ni praise team, ndio maana pongezi zetu ni pale anapofanya mambo mazuri, ni pongezi genuine sio za kujikomba au kufukuzia uteuzi, mtu anayesaka uteuzi kazi yake itakuwa ni kupongeza tuu, lakini mimi napongeza kwa mazuri na kwenye mabaya nakosoa.

Kwanza tukubalieni, hakuna mkamilifu isipokuwa Mungu pekee na malaika wake!. Pili Rais Magufuli ni binadamu, na sio malaika, hivyo pia sio mkamilifu!, hivyo pamoja na madhaifu yake yote ya kibinadamu, kama binaadamu mwingine yoyote, anaweza kufanya makosa ya kisiasa, kiuchumi na kijamii, ambayo rais Magufuli na serikali yake wanaweza kuwa wametenda, kwa mawazo, kwa maneno, kwa matendo, au kwa kutokutimiza wajibu wao, lakini kwa mazuri na mema ambayo Rais Magufuli na serikali yake, wanayatenda kwa taifa hili, hata yale mabaya na maovu yaliyostahili adhabu kali ya karma, hiyo karma inakuwa reversed kwa mema makubwa zaidi kuliko ule ubaya au uovu, hivyo
nasema kiukweli kabisa kutoka ndani ya nafsi yangu na kwa dhati ya moyo wangu kuwa, pamoja na yote yanayolalamikiwa, lakini bado rais Magufuli na serikali yake, watabarikiwa kwa mema yao wanayolitendea taifa hili, na hata kama kuna uovu, maana yeye sio malaika, uovu huo unaweza kufunikwa na mema yakizidi huo uovu!.

Trends readings zangu zinanielekeza kuwa rais Magufuli, so far, so good, might end up being one the best presidents this country has ever had, save for Baba wa Taifa kutupatia uhuru!. Rais Magufuli ni msikivu sana, ana upendo sana wa kweli, upendo wa dhati, upendo wa ajabu. Ni mtu mwema, mwenye huruma sana, huruma ya kweli na huruma ya ajabu, japo sio kwa wote!, hivyo akiendelea hivi, atabarikiwa sana na Mungu!, Tanzania itabarikiwa!.

Mungu Mbariki Rais Wetu Dr John Pombe Joseph Magufuli. Mungu Ibariki Tanzania,
karibu bandiko hili.


Kwanza msikilize Rais Magufuli hapa

Kisha anzia hapa

Bandiko hili ni la Septemba 4, 2018.
Ili kuwasaidia wavivu wa kusoma links, nawawekea na specific quote
Wanabodi,
Nimemuona akihutubia kwa humility na genuinity, hivyo mnaweza kushangaa akasimamia haki na kuhakikisha ofisi ya DPP inatenda haki kweli na haki hiyo ikaonekana inatendeka, hivyo wote wanaoozea kwenye mahabusu za nchi hii wengine kwa zaidi ya miaka 7 kama wakili Medium Mwale, na wale wanaozea Keko, Ukonga, Segerea na mahabusu nyingine kama kina Harry Kitilya, Sioi Sumari, Shose Sinare, Isaack Kasanga, Gonzaga, James Rugemalila, Jamal Malinzi, Peter Noni, Dr Ringo Tenga, wale Ma Sheikh wa Uamsho na wengine wengi, wanatendewa haki, na haki kuonekana inatendeka!. Kuna watu wanaoshitakiwa kwa makosa ambayo ukikutwa na hatia adhabu yake ni kifungo cha mwaka mmoja jela, lakini mtu yuko mahabusu mwaka wa 7 sasa na kesi haijaanza kusikilizwa!, huu ni uchunguzi gani ambao haukamiliki, na hii ni haki ya aina gani inayocheleweshwa?!.

Huwezi jua, kufikia 2025, President Magufuli might end up being the best president, this country had ever had, na sisi Watanzania katika umoja wetu, tukamlilia aendelee na kufanya maandamano nchi nzima kushinikiza katiba ibadilishwe, kipengele cha ukomo kiondolewe!.

Hongera sana rais wetu Magufuli, you are changing for the better!.
Big up! and God bless you.

Viva Magufuli!.
Viva Tanzania!,
Mungu mbariki Magufuli, Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali.
Kisha tembeleeni bandiko hili
Bandiko hili ni la 18 September 2019.

Kwa faida ya wengine ambao hawawezi kusoma links, nakuwekea quote yenyewe
9. My Take.
1. Kwanza kitu alichokifanya rais Magufuli cha kuwasamehe wakosaji hawa, ni kitu kizuri sana, rais Magufuli ameonyesha yeye ni mtu mwenye huruma na mwenye upendo. Ningemuomba rais Magufuli ailekeze huruma yake na upendo wake kwa mamia ya Watanzania wanaoozea mahabusu na magerezani, iwe ni wakosaji wa kweli au laa, kuna watu wanaozea magerezani kwa kesi ambazo hazina dhamana bila kesi zao kusikilizwa kwa muda mrefu, hawa ni baadhi yao tuu ninaowafahamu mimi, akiwemo Erick Kabendera, James Rugemalila, Peter Noni, Dr. Ringo Tenga, Harry Kitilya, Jamal Malinzi, Kaburu, Isaack Kasanga, Sioi Sumari, Shose Sinare, Gonzaga Mandago, Asa Mwaipopo, Deo Mwanyika, Dickson Maimu, Alex Lugendo, masheikh wa uamsho, and the list goes on, kiukweli hawa watu wanateseka.
2.Udukuzi ni kosa la jinai, ili nchi yetu kuonyesha inaheshimu utawala wa sheria, baada ya zoezi la misamaha kukamilika, naomba serikali yetu iwachukulie hatua wadukuzi sio waliodukua, maana hawa tunawajua na tunajua usukuzi unaendelea, bali walio likisha sauti hizo zilizodukuliwa kinyume cha sheria, wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria, tena kitu cha ajabu, unaweza kukuta hakuna hata mtu mmoja kati ya walidukuliwa amekwenda kushitaki ay kulalamika rasmi mawasiliano yake binafsi kudukuliwa.

10. Hitimisho.
Huu utamaduni wa mtu kusema ukweli halafu kwenda kuomba msamaha kwa rais na kusamehewa, unatia moyo sana, Hata mimi na kampuni yangu ya PPR, kuna madhila fulani ninayopitia, sasa sijui kama ni lile swali langu la Ikulu siku ile au ni zile makala zangu za kwa maslahi ya taifa magazetini, au ni hii michango yangu humu jf, hivyo nami najifakari mara mbilimbili, hata kama unajua kabisa hujakosa, lakini kama Wazee wanakasirika, nawaombeni sana msinishangae siku mkisikia na mimi nimeomba msamaha kwa maswali yangu, makala zangu na michango yangu humu jf, ambayo haikuwapendeza wakubwa, na nikiona vipi, naombeni msinishangae nikiamua kuachana kabisa na hii kazi ya uandishi wa habari, nikajiunga na chama, nikaunga mkono juhudi na kujitolea kumsaidia ...

Nawatakia Ijumaa Kareem, Furahi Dei Njema.
Paskali
Dodoma.

Paskali.
Baada ya hizo quotes mbili, Wakuu Wanabodi wenzangu , naomba uzisome kwa makini hizo quotes
Tukiwaambia rais Magufuli ni mtu msikivu, mwenye huruma, upendo wa kweli na upendo wa dhati, kuna watu humu walikuwa hawaamini.

Naamini by now wengi mmeishasikia rais Magufuli ametangaza nini.

Kiukweli kwa tangazo hili, rais Magufuli atabarikiwa sana, na Tanzania pia itabarikiwa, amini usiamini, this man might end up being one the best president this country has ever had, iwapo tukimpa kipindi cha pili, na akaamua kutuletea katiba mpya na kuisuka upya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa Tume huru zaidi na inclusive.

Hongera sana rais wetu Magufuli, you are changing for the better!.
Big up! and God bless you.

Viva Magufuli!.
Viva Tanzania!,
Mungu mbariki Magufuli, Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali.
 
Raisi wetu anasikitishwa kuona watu wanasota rumande na kukaa jela

Anatamani magereza yote yafungwe watu waijenge nchi.

Kiukweli kabisa kiongozi wetu ni mzalendo na mwenye huruma sana kwa raia wake

Hakika nakukubali sana Pasco mzee wa kung'ata na kupuliza.

Unafununu zozote za kibendera ataachiwa lini?
 
Tangu lini umeanza kufanya kazi ya uchungaji?
Wanabodi
Anzia hapa


Wanabodi, naomba isome kwa makini hiyo quote,
Tukiwaambia rais Magufuli ni mtu msikivu, mwenye huruma, upendo wa kweli na upendo wa dhati, kuna watu humu walikuwa hawaamini.

Naamini by now wengi mmeishasikia rais Magufuli ametangaza nini.

Kiukweli kwa tangazo hili, rais Magufuli atabarikiwa sana, na Tanzania pia itabarikiwa, amini usiamini, this man might end up being the best president this country had ever had.

Hongera sana rais wetu Magufuli, you are changing for the better!.
Big up! and God bless you.

Viva Magufuli!.
Viva Tanzania!,
Mungu mbariki Magufuli, Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali.
 
Raisi wetu anasikitishwa kuona watu wanasota rumande na kukaa jela,
Anatamani magereza yote yafungwe watu waijenge nchi.
Kiukweli kabisa kiongozi wetu ni mzalendo na mwenye huruma sana kwa raia wake.
Hakika nakukubali sana Pasco mzee wa kung'ata na kupuliza.
Unafununu zozote za kibendera ataachiwa lini?
Yaani wanatengeneza virusi na baadae kuvitafutia dawa
 
Back
Top Bottom