Rais Magufuli: Siwezi kusikiliza madai ya malipo yoyote wakati kuna malipo hewa kila kona

Hashim bin Faustin

Senior Member
Jan 30, 2017
177
216
JPM akihutubia umati wa watu Leo hii Mjini Lindi amesema serikali yake siyo ya kutishwa tishwa na hivyo hawezi kusikiliza madai yoyote wakati kuna Malipo hewa kibao kila Kona.

Mishahara Hewa, Matibabu Hewa, Malipo ya Uhamisho Hewa.. Hewa hewa hewa!


Maoni yangu:

Juzi nilisikia viongozi wa walimu wakitangaza mgogoro na Serikali. Kwa hotuba hii poleni sana walimu wote kwani mkuu hatishwi kabisa na kelele za Nyau.

Mtalipwa tukimaliza Hewa! Poleni Sana.
 
Nimemsikia rais akisema halipi madai ya watumishi "eti" kuna madai hewa mengi.

Ninachojua watumishi hawalipwi kiholela,kuna sheria za fedha zinazoongoza mchakato mzima,madai huanzia kwa mfanyakazi,yanaenda kwa mwajiri,kisha yanaenda kwa mkaguzi wa ndani,baadae yanafanyiwa uhakiki kwa CAG(mkaguzi wa mahesabu ya serikali)

Baada ya Mkaguzi wa mahesabu kuthibitisha uhalali wa madai,humrudishia mwajiri,mwajiri naye hupeleka hazina na hazina hulipa.

Nashangaa kwamba eti kuna mtu anasema halipi kana kwamba kulipa ni hiari yake!! Kulipa ni kwa mujibu wa sheria.

Ni yaleyale ya maalim seif kwamba hujanipa mkono wa salamu sikulipi,

Nchi ilianza kuangamia,watu wakakaa kimya,sasa kila mtu ajionee,na achukue sheria ambazo aliapa kuzilinda pale uwanja wa uhuru

Hakuna aliye juu ya sheria
 
JPM akihutubia umati wa watu Leo hii Mjini Lindi amesema serikali yake siyo ya kutishwa tishwa na hivyo awezi kusikiliza madai yoyote wakati kuna Malipo hewa kibao kila Kona, Mishahara Hewa , Matibabu Hewa, Malipo ya Uhamisho Hewa , hewa hewa hewa !!

Juzi nilisikia viongozi wa walimu wakitangaza mgogoro na Serikali , kwa hotuba hii Poleni sana walimu wote kwani Mkuu hatishwi kabisa na kelele za Nyau.... Mtalipwa tukimaliza Hewa !! Poleni Sana.

32a06f4cf91d79f3bf379a7694708a63.jpg

NA VYETI HEWA
 
Back
Top Bottom