herikipaji
JF-Expert Member
- Aug 23, 2016
- 1,198
- 1,345
Naomba rais Magufuli katika mambo yote unayofanya au unayotaka kufanya utoe kipaumbele kwanza katika sekta ya elimu, Elimu ni dira kuu na msingi mkuu katika ustawi wa jamii na taifa lolote lile ndio maana hata Mwalimu Nyerere alitumia akili na nguvu zake zote kuwasomesha Watanzania kwa hali na mali hata kuwapeleka nje ya nchi mfano China, Urusi nk.
Mwalimu Nyerere aliamini katika Elimu bora kwanza na sio kitu kingine na alitarajia Watanzania kupata Elimu kwanza ili watumie kujenga taifa na kuushinda umaskini. Mwalimu Nyerere leo na hata kesho ataendelea kukumbukwa kwa hili la kupigania Elimu bora.
Hakuna viwanda, hakuna. Hakuna uchumi wa kati, hakuna. Hakuna chochote kitakachofanikiwa pasipo elimu, hakuna.
Mataifa yote yalio dunia ya kwanza hii leo yanatoa misaada kwenye nchi maskini Tanzania ikiwemo lakini waliwekeza katika elimu. Nenda China, Urusi, Sweden, USA, Israel nk wamewekeza kwenye elimu bora kwanza sio kingine.
Nakuomba rais Magufuli sitisha mambo mengine yote ufanye uwekezaji katika elimu bora, elimu bora italeta viwanda, elimu bora italeta uchumi wa kati, Tanzania itaondokana na umaskini tukifanikiwa kupata elimu bora na wewe rais Magufuli utakumbukwa kwa hilo kama tunavyomkumbuka Mwalimu Nyerere.
Pesa inayotumika kulipa madeni aliyosema Makamu wa rais Mama Samia Suluhu kiasi cha shilingi bilioni 900 itumike kwenye kutoa mikopo ya elimu ya juu kwanza hayo madeni sitisheni kulipa kwanza.
Jamii ya Watanzania inalia na kusaga meno sababu watoto wetu wanakosa mikopo ya elimu ya juu na kushindwa kusoma sifa na vigezo vyote wanavyo.
USISAHAU HAKUNA TAIFA LILILOENDELEA KWA KUIPUUZA ELIMU, HAKUNA.
ITAKUWA NI MAAJABU YA DUNIA TANZANIA IWE TAIFA LINALOPUUZA ELIMU NA LIPATE MAENDELEO.
herikipaji.
MDAU WA ELIMU TANZANIA.