Rais Magufuli: Sitatenga hela ya Katiba Mpya ili watu waende Bungeni kula; wala sikuinadi kwenye kampeni

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,801
11,961
Kongamano linaanza saa 3:00 asubuhi hii.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ni Mshiriki Maalum kwenye Kongamano hilo. Watoa Mada ni Wanazuoni wabobezi katika masuala ya Uchumi, Siasa ya Uchumi,Siasa ya Jamii, Sheria n.k

3193D1F8-E9B5-45CC-B64D-279C3BF72219.jpeg

John Pombe Joseph Magufuli - Tanzania President



======

UPDATES

Kongamano UDSM

MADA: Hali ya Uchumi na Siasa nchini Tanzania 2018

Kanuni 3 zitazingatiwa ktk mjadala
  1. Uwazi na Uhuru
  2. Heshima na staha
  3. Kuzingatia muda

Rais Magufuli hatazuiliwa kuongea hata akizidisha muda


Profesa Humphrey Moshi

Nitazungumzia “Umuhimu wa Viwanda ktk Uchumi wa Nchi hii”​

Kwa miaka 15 Uchumi wa TZ ulikuwa ukikua kwa 6-7% lakini haukuwa Uchumi Shirikishi.

Sekta ya Madini haikuweza kupunguza kasi ya umasikini na ajira.

Bado mfumo wetu wa uchumi haukuwa umebadilika; hakukuwa na mfumo mbadala.

Ukitaka kupunguza umasikini kwa haraka na kufikia uchumi, viwanda ni lazima.

Viwanda ni sekta vuguvugu, ni kiwanda cha uvumbuzi. Hakuna sekta yoyote katika taifa lolote iliyo na mahusiano na uchumi kama viwanda.

Kwa nchi za Afrika hasa Tanzania viwanda ni sekta kombozi, kwahiyo kwa Serikali ya Awamu ya Tano inafanya kitu sahihi kinachopaswa kufanyika

Wakati wa Mwalimu, tulikuwa na viwanda vya kila aina na viwanda vinazalisha ajira zenye hadhi.

Kulikuwa na mpango wa SAPs lakini baadaye tukaja kuwa na ubinafsishaji ambao ulifyekelea mbali viwanda

-Wafadhili wanatoa mapendekezo yao ambayo hayaendani na mipango ya Taifa​
-Wakati huo kulikuwa na viwanda vya umma lakini hakukuwa na wataalamu, sasa wapo​
Miaka ya nyuma hatukuwa na uwezo wa kununua katika masoko ya kimataifa

Kulikuwa na uwekezaji katika tafiti za mipango na hakukuwa na utekelezaji, watu wa nje wanakuja kuchukua mipango Tanzania na kwenda kuitekeleza

Serikali ni lazima ikae mbele wakati wa kuendeleza viwanda, tulikaa miaka 25 tukisubiri sekta binafsi ituletee umeme.

Tulikaa miaka mingi tukisubiri sekta binafsi ituletee kilimo cha miwa. Miradi mikubwa ya Marekani inamilikiwa na serikali

Elimu, miundombinu na viwanda lazima viende pamoja. Tuboreshe uhusiano na nchi za Asia

China wakati wanajenga SGR walikuwa wana kipato cha 1/3 ya Watanzania lkn sasa ni zaidi ya mara 10

Tuimarishe mahusiano na nchi hizo, tupunguze utegemezi kwa nchi za Magharibi


Profesa Hudson Nkotagu

Nitazungumzia Nishati na Miundombinu katika kuendeleza uchumi wa viwanda

Vyanzo vya nishati ni vingi vikiwemo vanzo 'jadidifu na vile visivyo jadidifu'

Chanzo jadidifu kama Mto Rufiji kufikia 2020-2025 kitakuwa kinachangia asilimia 21 ya nishati ya umeme nchini

Yako maeneo yenye dalili za kuwa na mtiririko wa mafuta. Serikali imejipanga kuzalisha Mewati 5,000 na kufikia 2020-2025 kupitia Stieglers Gorge itafikia Megawati 10,000 Ili Serikali imeweza kutekeleza miundo mbinu wezeshi ikiwemo Reli, barabara ya kuunganisha mikoa na nchi za jirani. Barabara za vijijini. Usafiri wa anga na Majini vimeboreshwa. Ndege zimenunuliwa karibu 9. Kuimalisha usafiri wa angIa. Meli zinatengenezwa na nyingine zinakarabatiwa. Hiyo ni miundombinu wezeshi ya kuinua uchumi

Changamoto

Wataalamu ni wachahce sana. tunatakiwa tuwe na injinia 1 kwa mafundi watano na wafundi michundo 25. Tnatakiwa tuwe na Injinia 10 Mafundi 50 na fundi michundo 250,hiyo ni ya kitaifa.

Tuhakikishe nishati zetu hazipotei, mfano taazinawaka na jua linawaka

Stiegler's Gorge

Faida ya Huu Mradi wa Stiegler's Gorge

Tutatumia asilimia 3 tu ya eneo lile.

Itapunguza ukataji miti

Hii nishati ni endelevu sababu haihitaji wabia.

Itavutia wawekezaji

Itaongeza ukuaji wa miji

Mapendekezo

Napendekeza Serikali iweze kuendekeza vyanzo mbalimbali vya nishati, Kuongeza Wataalam, Kuongeza Tafiti na kuwawezesha watafiti na kuelimisha raia.


Profesa Martha Qorro

Fursa ya lugha na Maendeleo

Katika mada hii ntazungumzia mchango wa lugha ya kiswahili katika kuleta maendeleo, Mawasiliano na maendeleo,Tafiti zilizofanyika na changamoto katika ufundishaji wa lugha

Lugha ni chombo au nyenzo kuu ya mawasiliano. Na kwa nafasi hiyo lugha huwa inamuwezesha mwanadamu kufikiri, kuchambua kupanga kuamua na kutekeleza kwa pamoja kuboresha maisha.

Mawasiliano na maendeleo

Lazima lugha iwe inaeleweka kwa pande mbili. Msemaji na msikilizaji. Yasipokamilika, lugha haiwezi kuleta maendeleo.Bila kusikilizana hakuna maendeleo

Kuna Elimu, Maendeleo na lugha. [Mawasiliano ya maendeleo]

Uhusiano wa Elimu na Lugha wengi hawaufahamu

Tafiti zilizofanywa africa zinasema moja ya sababu ya kutokuwa na maendleo africa ni kwamba mipango ya maendeleo yanafanyika kanika lugha za kigeni ambazo ni kileno, kingeleza Kifaransa wengine kiarabu. Ili kuapata maendeleo lazima tuingize lugha za jamii kwenye maendeleo.

Tanzania tunakabiliwa na changamoto za elimu katika kufundisha lugha. Mtoto anaanza na lugha ya Nyumbani shule msingi anafundishwa kiswahili na sekondari anafundishwa kingeleza. Tunajenga misingi tofauti za Lugha.

Tafiti zinasema ili mtoto aweze kujifunza lugha ya kigeni anatakiwa awe vizuri katika lugha mama. Mtoto anakosa msingi wa llugha yoyote

Unapowakataza watoto kuzungumza lugha za jamii inamaana unamwambia mtoto hizi lugha hazina maana kwa lugha nyingine hizi ni dhalau

Katika mpango wa maendeleo wa miaka mitano 1969 hadi 1974 ulisema

Tuna msingi wa lugha za kiswahili na kingeleza, litasbabisha matabaka na elimu ya Sekondari haitakuwa na maana kwa jamii.

Kutumia lugha mbili unatenga wasomi na Jamii.

Miaka mitatu ya awamu ya tano

Wanaona fahari kuzungumza kiswahili hata rais wetu. Tunaposhiriki lugha moja na viongozi tunajiona tupo pamoja na viongozi

Hii ya elimu pasipo ada imeongeza fursa ya kuzungumza kiswahili.

Nini kifanyike?

Mfumo wa elimu wa sasa duniani, unafaa kuzungumza lugha za kigeni nyingi tofauti na kingeleza tu. tufundishe lugha zaidi na moja

Kiswahili kitumike katika ngazi zote za elimu, hii itaunganisha jamii

Baba wa taifa alisema Wasomi ni watu waliotumwa. Nchi nyingine wakienda kusoma wanarudi kwenye jamii kuwatafsiria kile walichokisoma. Hivyo kila mtu aludishe kwa jamii kile walichokisoma kwa kiswahili. kuna tafiti nyingi sana ili zimefungiwa katika ngome za lugha na wenye ufunguo ni wasomi.

Tunahitaji kukipeleka kiswahili nchi za nje kwenye balozi zetu. Mabalozi wafundishe kiswahli. Google wanasema Kiswahili Kenya, kwanini sio Kiswahili Tanzania? Tunarudi nyuma kwa kukataa vitu vyetu.


Profesa Kitila Mkumbo

Atazungumzia Huduma za Jamii.

Ni muhimu tujue tumetoka wapi.
  1. Mwalimu Nyerere alipigania uhuru, huduma za jamii zilikidhi wakati huo
  2. Mwinyi alingoza mageuzi ya kisiasa na kiuchumi
  3. Mkapa alijenga taasisi Imara za
  4. Kikwete alijitahidi kulinda mafanikio yaliyopatikana kipindi cha mkapa
  5. Sisi tulioingia awamu ya tano tumekuta Uchumi unaokuwa, Ujenzi wa Miundo mbinu nk.

Changamoto ilikuwa inakuwa bila kupunguza umasikini, Kulikuwepo kulegalega kwa uwajibishaji. Awamu ya nne ubora wa huduma za jamii tuliyumba.

Mpango wa pili wa maendeleo

Bajeti yake ni Til 129 huduma za jamii, Afya elimu na maji. Maji pekee til 10.4

Mkazo wa awamu hii ni nini? Rais alipohutubia bungeni alisemawananchi wamechokana wana Chuki dhidi ya ufisadi pamoja rushwa, mimi nmeahidi wananchi kwamba ntapambana na rushwa na ufisadi bila haya yoyote

Serikali hii imefanikiwa kulinda uchumi wa awamu iliyopita

Serikali imedhamilia kusimika weredi katika nyanja mbalimbali katika Siasa, ajira, utumishi nk

Serikali imedhamilia Kujenga uwajibikaji katika utumishi wa Umma

Serikali imedhamilia Kupambana na rushwa. Mfano saga la IPTL. Lipo kipindi kirefu kwa miaka 25.

Elimu bure imekuwa mkombozi sana. Hili liliwahi kutajwa lakini ndani ya Serikalini walikuwa wanakataa, awamu ya tanno imewezekana.

MAJI

Maji imechukuliwa kama ni sekta mtambuka ambayo ndio kiini cha uchumi. Inatakiwa tulinde rasilimali za maji. Kama kila mtu ukimgawia maji, kila mtu anaweza kupata Mapipa 9000.

Kila awamu imejitahidi kupiga hatua katika usamabazaji wa maji hadi 50% ndani ya kipindi cha mikata mitatu tumeongeza asilimia 6. Upande wa uwekezaji miradi ya maji ilikuwa til2, kwa miaka mitatu tumeongeza til 2 nyingine japo zinahitajika til 8.

Tnahitaji kuchangisha kununisha Mfuko wa maji

Nini kimefanya tufanikiwe?

Ujasili wa kufanya maamuzi makubwa

Uwezo wa kufanya maamuzi sahihi bila halama za kisiasa za muda mfupi

Ana uwezo wa kufuatilia utekelezaji

Ujasili wa kuwawajibisha wasaidizi wake bila woga wala upendeleo

Na ameweza kupambana na Ruswa

Tunakoelekea tunatalinda mafanikio ambayo tumeyapata

Tuna mpango wa kutumia maji ya ziwa Victoria, nyasa kupeleka maji kwenye maeneo yenye ukame wa kudumu.

Katika kipindi cha miaka mitatu rais amefanikiwa kuvuruga na kutibua mtandao wa watu wajanja wajanja.

Msingi wa yote haya ni Uongozi, ujasiliwa kufanya mageuzi makubwa ya kisiasa, kiuchumi nk

Ili tufanikiwe tunatakiwa tuwe utulivu na kisiasa na Utawala wa Sheria


Profesa Rwekaza Mukandala

Anazungumzia Hali ya Siasa na Utawala​

Nabaini mambo matatu

Mtanziko wa wanasiasa

Siasa ni mchezo mgumu wa mikakati ya wanasiasa

Malengo ya mwanasiasa ni

Kuapata madaraka na kudumu ofisini

kutawala nkuongoza kwa mafanikio

kujenga chama chenye utiifu kwake

Tathimini ya kupima utendaji wa rais ni Mgumu

Wapo wanaoshabikia Maendeleo[ Quantity na quality]

Kuna vigezo vingine havionekani mfano watu wanavyojisikia, watu wanafurahi, wana morali,watu wameridhika nk

Kundi la tatu ni wale wanaoichukulia nchi kwa ujumla wake. je kuna amani? Kuna maendeleo

Mchakato tunapima bidii au juhudi sio matokeo

Nyerere hajatoa umasikini lakini tunampenda.

Ukitaka kupima vita ya rushwa unaangalia dhamira na juhidi japo rushwa haijaisha

Kigezo kingine unaangalia uwezo. Majeshi yanaangalia uwezo. Wanaweza kuwa na vifaa vita ikija watu wanaingia mitni

Swali la kwanza

Je, kumekuwa na uelewa na ulimwengu na changamto zake?

kumekuwa na uchbmuzi na uelewa katika nchi yetu?

Ameweza kuongoza kuwa msitaliwa mbele kwa vitendo?

Ameweza kubuni lugha ya kufanya watu wamfuate?

Ameweza kujenga chaa kinachomuunga mkonno?

Utawala umezingatiwa?

Tulikotoka uelewa wa Ulimwengu na mifumo yake ulieleweka sana mfano wa wakoroni na mabeberu.

Magufuli hajaandika machapisho juu ya misimamo yake. Ila misimamo yake ni kama ya Mwalimu

Kuhusu uelewa wa nchi. Mwalimu aliongozwa na azimio la Arusha, Magufuli ana uelewa mzuri wa changamoto za nchi.

Rais ndio kiongozi na mwanasiasa wa nchi, anatakiwa kuwa mfano. ufuasi hauhitaji nguvu bali hiari. anafanya kazi sio hadi waziri, haendi nje, hospitali anatumia za ndani. amejirundikia mtaji wa jamii. amekuwa mwepesi wa kutenda na kuchukua hatua. ameweza kubuni msamiati. Mwalimu alikeea kupe Magufuli anakemea kajipu.

Kuna aina mbili za Viongozi, Viongozi mageuzi na viongozi nipe nikupe/Wapiga dili. Mwalimu na nyerer ni Viongozi Mageuzi

Kukisafisha na kukinyosha chama ni kazi kubwa sana, Mwalimu alianzisha vyama vingi. Kazi ya kukisafisha na kukinyosha chama ndio imeanza. Viongozi na wanachama wanahitajika ili kumuunga mkono rais.

Kuna tatizo kukosekana kwa itikadi yenye mvuto katika chama.

Dola na taasisi zake ni muhimu sana. Swala la muundo ni muhimu. Benki ya dunia ilizoofisha dola. Serikali ya awamu ya tano inaonekana kupendele Serikali kuu.Mishahara inalipwa kwa wakati, Serikali inahamia dodoma,Wafanyakazi hewa wameodnolewa, uzembe vinakemewa, Ufuatiliaji wa miradi unafanywa, kodi inakusanywa. Miradi midogo na mikubwa inajengwa. Mifuko ya jamii imeungamishwa

Mchakato wa katiba utakapolejewa kuna umuhimu wa kurejewa upya kwa rasimu ya katiba mpya sababu miaka minne imeshapita.

Mahakama ya kupambana rushwa imeundwa, mahakimu wameongezeka. Uamuzi wa kujipima kwa kila jaji unatekelezwa. Ofisi DPP imerekebishwa. Kubambwa na kuwekwa ndani kiholela inaendelea kupungua, kamisheni ya kupiga ita madawa kulevya imepewa meno zaidi.

Uwezo wa Polisi kiutendaji bado mdogo hata Magereza nao hivyo hivyo. Bado kuna changamoto ya kupata haki. Hakuna uhakika wa kupata haki. Rushwa na ufisadi bado adui kwani vimeenea katika vyombo. Takukuru inatakiwa kuongeza juhudi.

Bunge limeendelea kutimiza wajibu wake na kuboresha utendaji.

Swala la Zanzibar zilijitokesha tofauti 2015 na CUF walijiondoa kwenye uchaguzi. CUF wameendelea kutafuta haki kwa njia za amani na kisiasa.Serikali imeendelea kudumisha amani Zanzibar

Tathimini ya miaka mitatu ya Magufuli ni ngumu sababu hapakuwa na vigezo vya kutumia.


SASA HIVI KINACHOENDELEA NI MAJADILIANO

Watu watauliza maswali na kujibiwa.

Yeremia

Anasema Serikali itoe fursa kwa vijana wa kitanzania kupata ujuze, kama wanavyotoa elimu bure


Padre Kitima wa Baraza la Maaskofu anasema

Kuna tatizo kwenye tume ya Uchaguzi naomba iongelewe

Kuna tatizo kwa watendaji wa chini wananyanyasa wananchi mfano Wakuu wa Wilaya

Uchumi umekuwa lakini kwa wananchi haionekani. Sekta binafsi ijengwe ambayo itasaidiana na Serikali. asanteni


Frank nasema

Rais kama itakupendeza tuandalie sisi vijana chombo cha kutuwezesha sisi vijana kukabiliana na ajira kwa vijana. Kituunganishe vijana na Serikali


Prof. Agness

Kilimo ni kichocheo cha Viwanda na biashara, Nchi zilizofanikiwa zimewekeza sana kwenye tafiti za kilimo hadi 10% lakini Tanzania tunachechemea kwa 1% kwenye utafiti.

Wale wenye dhamana waangalie kwa karibu kilimo kisaidiwe kwa namna gani

Mchango wangu wa pili, 52% kwenye nchi hii ni vijana tuwaangalie kwa karibu. Tnajitahidi kuwaweka kwenye mstali kielimu kiroho na Kimwili.Ila sasa hivi kuna vitu vya ajabu vimezuka sana kama Kucheza kamali. Tunajenga taifa la ajabu. Kiimani ni kosa. Marekani ukitaka kuchez akamali unaenda Las Vegas. Watoto hawawezi kutengenezea maua lakini anajua kucheza kamali. Hali iliyopo ni hatari.


Jesca John - Mwanafunzi wa kidato cha Sita chang'ombe.

Tutathini ni nini kifanyike ili rais ajaye asiharibu kile kilichofanywa na Magufuli, tunahitajij wakina Magufuli katika Miongo mitatu. Asante


Tumaini Boniface

Natoa mapendekezo katika mada ya uchumi ni nishati. Sijasikia jinsi ya kuwasaidia wagunduzi wetu na wanasayansi wa hapa Tanzania. Kama serikali ikiwaangalia hawa na kuwainua, Tanzania itafika mbali sana.


Prof. Issa Shivji

Hatuwezi kuendelea kwenye uchumintegemezi, hatuwezi kuendelea bila sekta binafsi

Tulikuwa na sera na maelekezo ya kujenga viwanda awamu ya kwanza.

Kwakuwa tumekuwa na uzoefu, jambo muhimu ni kujifunza kutoka awamu ya kwanza. Tulikosea wapi?

Mwalimu aliorodhesha makosa

1.Sekta ya viwanda ilikuwa tegemezi kuanzia mali ghafi, vipuli na mashine

2. Sekta ya Viwanda na Kilimo havikuingiliana, kila moja ilikiwa huria.

3.Menejimenti ilikuwa dhaifu na ubadhilifu wa mali ya Umma

Suala la Viwanda sio idadi ya Viwanda bali ni swala ambalo lazima inaendana na kujenga uchumi wa kitaifa.

Hatukuwa na mipango kamili ya kushirikisha wafanyakazonkatika mipango.

Tunifinze kutokana na hayo

Sisi hatuwezi kufuata njia ya Magharibinkufikia Viwanda. Sisi inabidi tujikite kwenye kilimo kupitia wakulima wadogo. Wanaweza kulima kilimo chemye tija.

Nampongeza rais Magufuli kwa jambo moja tu la tukio la leo la kukaa na sisi na kusikiliza maoni ya wanazuoni wake.


Prof. Kabudi

Mwalimu mzuri ni yule anayotumia elimu na maarifa aliyoyapata shuleni katika kuongoza. Rais Magufuli amesoma hapa mambo ya Chemistry lakini somo la Development studies analitendea haki.

Malengo makuu ya kiuchumi ya awamu ya tano.

Maadili, vita ya ufisadi rushwa nk

2. Kuimarika kwa uchumi kwenye madini, uchukuzi, mawasiliano, kilimo, kuongezeka kwa mapato ya kodi na yasiyo ya Kodi.

Tunajenga Miradi ya umeme, barabara. Mradi wa umeme utatekelezwa, wapende wasipende utatekelezwa.

Ujenzi wa reli ya kati SGR unaendelea vizuri. Reli ya hatutaing'oa, zitaendelea kusaidoana.

Kufufua shirika la ndege la Tanzania. Ndege zimenunuliwa, zipo zilizofika na nyingine zinakuja.

Bomba la mafuta gafi kutoka Ohima hadi Tanga. Bandari ya Tanga itakua.

Kuboresha Viwanja vya ndege na Magati ya bandari, upanuzi wa bandari ya Tanga na Mtwara.

Ujenzi na ukarabati wa Hospitali 10 za Wilaya. Nyumba 306 za watumishi wa afya zimekamilika.

Tumeondoa ada kwenye elimu sasa wanafunzi wameongezeka. Mikopo ya elimu ya juu imeongezeka.

Huduma za maji zimeongezeka.

Rais Magufuli anasimmia mali zetu na raslimali.

Prof. Kabudi: Mbunge wa Ukonga Mwita Waitara amerudi ndani ya CCM sio kwasababu ya rushwa bali ameguswa na mambo yanavyoendelea

Tufanye kazi tathmini zitakuja kuanzia mwakani kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu 2020


Rais Magufuli

Leo sikutegemea kuzungumza. Nlipanga kuja kusikiliza tu na kijinoti changu. Nmeandika yote.

Chuo kikuu nakipenda, nimesoma na kukaa hapa. Nlifungia ndoa hapa. Mimi sikuvaa koti wala mke wangu hakuvaa shela lakini tulifunga noda kwenye kanisa la chuo kikuu. Pete alitununulie padre na soda. Mi nlikunywa Pepsi na mwenzangu Milinda.

Sio kwamba sikuwa na uwezo bali huo ni utaratibu. Watoto wangu watoto wamefunga ndoa na wengine nikiwa rais, haujawahi kusikia sherehe hizo.

Wote waliochangia mada wamezungumza kutoka moyoni. Yote yaliyozungumza tutayafanyia kazi.

Niseme kw auwazi kwamba uongozi ni kazi ngumu. Sikutegemea kwenye uongozi nipate kazi ngumu hivi.

Nlikiwa Waziri miaka 20,nlikiwa naona changamoto lakini si kama za rais. Chumbani kwangu ukiingia kina mafile hadi kitandani. Na kila file lina umuhimu huwezi kulipeleka kwa mtu mwingine. Saa nyingine inahitaji maombi maalum ili uweze kutenda haki.

Ni ukweli pia kwamba nchi yetu imepitia katika hatua mbalimbali. Ilikuwa imefika hatua ya hovyo katika maswala ya rushwa na ufisadi..

Ndugu zangu nafahamu yapo mambo tumeanza kuyafanya. Katika hali ya uchumi tunakiwa kwa asilimia 7, tunataka ukue zaidi ya hapo. Mfumko wa bei umeendelea kua 3. Nchi yetu ni miongoni mwa nchi tano ambauo uchumi wake unakuwa kwa kasi.

Viwanda 3066 vipya vimejengwa

Si vyema kw anchi kama tanzania kuendelea kuzalisha mali ghafi tu bali kama ni pamba nguo tutengeneze hapa, tuvae nguo halafu wao tuwapelekee mitumba

Tanzania ni ya pili kuwa na mifugo mingi. Je viwanda vya nyama na ngozi vipo vingapi?

Ifike wakati tuvae nguo na viatu vya hapa.

Nchi yetu bado ina akiba ya fedha za kigeni dola bil 5.4 tunaweza kuendesha nchibkwa kununua bidhaa kwa kipindi cha miezi 6.

Tumebana mianya ya kupoteza fedha.

Tulikuwa na madeni hewa. Watumishi hewa walikuwa 20 elfu. Tulikuwa tunalipa bil zaidi ya 200 kwa mwaka.

14 elfu wa vyeti feki tulikuwa tunawalipa bil 186 tulikuwa bil. Wote hao jumla tulikuwa tunalipa bil 423 kwa mwaka

Kuna mtu alikuwa analipwa mishahara ya watumishi 17

Tulikuwa tunalipa mishahara Bil 777 kulipa mishahara sasa hivo tunalipa bil 251.

Katika maswala ya barabara 1500 KM tumeshazijenga.

Tunajenga kutoka Kimara hadi Kibaha barabara ya njia 8.

Til 7.06 zinajenga KM 700 fedha za Serikali.

Katika swala la elimu bure tulizungumza wakati wa Kampeni. Bil 23.85 zinatolewa kwenye elimu bure

Wanafunzi waliongezeka kutoka Mil 1 hadi Mil 2.

Vyuo vikuu wanafunzi kukopwa ilikuwa hadi waandamane kwanza. Kulikuwepo na rushwa kwneye bodi ya mikopo.

Sasa Bil 483 inatolewa mikopo na wanafunzi wameongezekakutoka 98 elfu hadi 124 elfu.

Kuna vyuo vikuu vilikuwa havikidhi vigezo mfano chuo kikuu cha Kampala. Wizara ya elimu inalishughulikia hili. Nia ilikiwa ni kupata hizi hela. Tunataka vyuo vikuu vyenye ubora.

Chuo kikuu cha Dar mumeendelea kumantain standard hongereni sana.

Nitoe wito kwa wale wanaotsfuta vyuo, waende kwenye vyuo vyenye ubora.

Katika maswala ya miundombinu tumeamua kupanua bandari ya Dar Es Salaam. Pale kina kirefu tulikuwa tunawapa wawekezaji, kwahiyo tumeamua kuanua na kuchimba upya til 1.2 zinatumika.

Bandari ya tanga tunaipanua sabbau kuna kiwanda kinajengwa pale kinachozalisha Simenti.

Tumeamua kupanua bandari ya Mtwara.

Tumeamua kununua meli. Tangu MV Bukoba izame hakuna meli ililetwa. Tunajenga meli mpya ya Mil 89 na tunakarabati meli nyingine pia.

Tunakarabati reli ya Dar Arusha, ukarabati ushafika Tanga. SGR tutaiunganisha na Rwanda pamoja na Burundi.

Tumenunua ndege. Watalii 1.5 walikuwa hawafiki. Egypt wanafika mil 10 Sababu wana ndege zao. Hatukukopa sehemu yoyote. Unambana fisadi kule analia unaenda kununua ndege. Ukilipa kwa mkupuo gharama zinakuwa ndogo. Lengo kubwa ni kuinua utalii.. Mwaka huu watafika mil 2. Watalii wanachnagia pato la taif akaribia 17%.

Miradi mingine tunafadhili wenyewe na mingine marafiki wanatusaidia.

Tunabadilisha barabara za dar es Salaam, sasa zinajengwa kwa bil 660. Interchange zitajengwa nyingi. Kamata, Ubungo. Tumepata mkopo wa kujenga km 359 kutoka katavi hadi tabora.

Baada ya sheria ya madini. Tulitegemea kukusanya bil 194 tumekusanya zaidi ya 300

Tumenunua rada. Ndege zinapopita lazima zilipe. Usalama ulikuwa unatisha. Swala la umeme hakuna kitu unaweza kuzungumzia uchumi bila kuwa na umeme. Ndonmaana tumeamuankujenga mradi wa Stiegler's gorge.

Kama una kiwanda na umeme bado upo juu, unatumia umeme wa mafisadi. Senti 11 za kimarekani wakati uingeleo 0.20 marekani. 12.Umeme wa kutumia maji ni rahisi. Sh 36bkw aunit. Umeme wa jua na upepo 114.2 kwa unit umeme wa gesi 118 per unit. Umeme wa themo 114.2 mpaja 206 per unit mafuta 547 per unit. SG. unatoa 2100.

Aliyeandika ripoti analipwa na anatumiwa na watu. Wasomi wetu wengine wana matatizo. Tanzania ina Eneo ni 32.5 imeachiwa kwa ajili ya mazingira. Kuna sehemu nyingine tunataka yatangazwe. Ni lazima jile tunachokifanya tuangalie watu wetu. Watu, ng'ombe, mbuzi vinaongezeka. Huwezi kutunza tu wazingira wakati watu hawana sehemu ya kukata kuni na kulima. Tunatumia 2.8% ya eneo la selous tupawasaidie hawa wanaokata miti wapate umeme. Na bei ya umeme utapungua.

Tunataka tuwe na umeme wa uhakika wa bei rahisi

Wito wangu tuwe wazalendo. Tusikubali kutumiwa. Aliyefanya utafiti wa Mazingira ni Prof tena wa hapa. Aliwahi kuwa mbunge. Alisema tutakapokuwa tunajenga tusiweke choo pale. Kila kitu kitakachoingia pale laizima kipimwe. Anashindwa kujua mto unatoka mbali. Toilet wanazuia pale wakati huku mto unapotoka watu wanajisaidia kwenye mto.

Wabaya wakaitumia hiyo ripoti, uzuri tumeshairekebisha.

Haitakuwa mara ya kwanza. Kule Songea Palipatikana urenium, wakatoa vibali haraka sababu wana manufaa nayo, lakini hapa tunataka umeme wanatusumbua.

Mkumbo alosema mumepeleka vilaza pale dodoma kusoma chuo kikuu, mawazo yake yakapingwa. Mimi nikayafanyia kazinna nikamchukua nikamfanya katibu mkuu

Ninaposema nchi yetu inaweza kuwa donor country watu wanshangaa.. It's true. Ukizungumza matanzanite yote yasingekuwa yanauzwa nchi za nje. Sisi tulikuwa tunafaidika 20% tu. Watu walikuwa wanachimba bila sheria. Kwenye shahabu huku mtu anasomba. Halafu unakuta prof anasema 0.02% ya dhahabu ndo imo kwenye makinikia na kukuta kuna madini ya kila aina. Watanzania nawaomba uzalendo kwanza.

Watu unakuta wanazungumza hovyo hovyo wale ni visenti walivyopewa. Si umesikia leo nimesema.

Ninachotaka kuwaambia mimi ni mtoto wa hapa ninajisikia fahari sana. Sitawaangisha

Katika maswala ya Demokrasia. Watu hawawezi kumaliza uchaguzi halafunkesho yake unakuta wanaandamana mtaani. Demokrasia nayo ina mipaka yake. Mkimaliza uchaguzo sehemu za mabishano ni bungeni na kwenye halmashauri. Kuna wanasiasa wengine ni wazuri hadi natamani kuwateua kama mzee cheo na profesa pale.

Tunataka kwenda mbele. Unapoamua kuhusika na mafisadi wakubwa si kitu rahisi. Wapo kila mahali, ccm, chadema na wengine hawana vyama. Ndo maana nimeanzisha mahakama ya ufisadi. Kuna reform nyingi zinafanywa.

Hii sheria ya madini wapo waliyoipinga bungeni.

Sokoine tumetoa matrekta 10, walikuwa wnafundisha watu bila mafunzo ya vitendo

Amani: kule Kibiti maaskari karibia 16 walifariki. Vyombo vyetu vya ulinzi viliwatuliza sijui kama watarudi tena.

vyombo vya ulinzi wamejenga ukuta miezi 3 nlijua watajenga mwaka au miezi sita. Unakuta mtu anawatukana tu hadharani hivi vyombo vya amani. Leo Libya wanalia wanaomba Ghadaffi angekuwepo wamfufue. Hawakutaka wawe hivyo. Lazima watanzania wote kwa pamoja tusimama tuitunze hii Amani

Wale wanaojaribu kuharibu amani tuwakemee kwa nguvu zote.

Nmefurahi, ntakuwa ninakuja tena. Siku nyingine ntakuja bila hata kunialika, msije mkanifukuza.

Rais Magufuli: Najua nimewakera nilipotaja majina ya Maprofesa Hata nilipotaka kumteua Dkt. Bashiru niliambiwa ni CUF na wana CCM. Kulikuwa na ka-Syndicate flani ambako ilikuwa kazi kukasambaratisha, Mnisamehe kwa kuteua viongozi wenu wa chuoni

Nimeteua sana vijana, nafahamu kuna makosa mengi watakuwa wanafanya kwa sababu ya kuchemka damu, muwasamehe. Nimeteua pia wanawake wengi, lakini kila unayemteua, ni hawara wako, sasa sijui wanataka niteua wanaume tu? Tena hayo wanayasema wanawake.

Tumezuia safari za nje. Watu walikuwa wakipishana angani. Tumekubaliana kushusha mishahara ya wateule hata mshahara wa Gavana tumeupunguza. Wangu ni milioni 9 tu.

Kuwa na sekta binafsi ni vizuri lakini tusifikirie ndio suluhu, wale wako kwa kujiongezea faida

Wengine wanasema sijui Kiingereza! Sasa sijui nilipitaje kwenye maandiko yangu ya chuo. Sijui nchi gani sijaenda. Nilikuwa Mwenyekiti wa Mawaziri kwenye Mkutano kule Vancouver - Canada, asa sijui niliendeshaje vikao.

Wachina wako Bilioni 3 lakini hawazungumzi Kiswahili wala Kiingereza wao wanazunguza Lugha yao ya Kichina. Vivyo hivyo kwa Warusi, Wajerumani na Wafaransa lakini sisi wa hapa akija Muingereza tunabadilisha hadi namna ya kuongea

Najua nimewakera nilipotaja majina ya Maprofesa. Hata nilipotaka kumteua Dkt. Bashiru niliambiwa ni CUF na wana CCM. Kulikuwa na ka-Syndicate flani ambako ilikuwa kazi kukasambaratisha. Mnisamehe kwa kuteua viongozi wenu wa chuoni


KATIBA MPYA

Naelewa kuhusu watanzania kutaka Katiba mpya, sasa tunaendaje? Tunaenda na katiba pendekezwa au tunaenda na rasimu ya Warioba? Manake miaka minne imeshapita. Huu sio muda wa porojo bali wa kufanya kazi.

Sitegemei kutenga fedha kwa ajili ya watu kula wakakae bungeni kujadili katiba, hata kama kuna mtu anataka kutupa hizo fedha, atupe tukatengeneze reli. Watu wanakaa wanapiga kelele katiba mpya, utadhani katiba ndio mwarubaini wa kila kitu.
 
Sidhani kama kutakuwa na uhuru wa kuhoji ununuzi wa madiwani na wabunge na tume huru ya uchaguzi. Itakuwa ni kusifu kusifu na kusifu tu.
UDSM wajihadhari kwa kuandaa vitu bogus kama hili "kongamano" na kumshirikisha Mkuu wa Nchi ambaye hapendi kukosolewa faraghani nahadharani. Wanazidi kushusha hadhi ya chuo kama academic institution.
 
Nitakuwepo pale na nitakuwa miongoni mwa watakaomshushia nyundo huyo "Jiwe" kama nitapewa fursa. Akileta longo longo basi nyundo italisambaratisha "Jiwe" kabisa kabisa.

I will be counteracting & intelligently opposing you with vivid facts..!! Ukiona mtu mrefu strong & colored na in CCM uniform ndio mm..!! Plz usikae beside me anything painful and unethical can happen..!!:oops:
 
Tujongee kwenye Azam Two kwa ajili ya Kongamano la Hali ya Uchumi wa Tanzania kwa kipindi cha miaka 3 ya Utawala wa Rais Dk. John Pombe Magufuli katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Rais Magufuli ni Mshiriki Maalum.

IMG_9856.JPG
IMG_9857.JPG
 
Safi sana tunasubiri. Live hapa kumusikia mwenye nchi anasema nini? Je leo atalegeza? Je atabana Zaidi vyuma?
 
Back
Top Bottom