Rais Magufuli: Sitasomesha Wanafunzi waliopata ujauzito, siwezi kusomesha Wazazi

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Habari wanaJF,

Leo akiwahutubia wakazi wa Bagamoyo, Mkoani Pwani. Rais Magufuli amesema hakuna Mwanafunzi aliyebeba ujauzito atakayerudi shule katika utawala wake. Akaongeza kuwa hawezi kufanya kazi ya kusomesha wazazi.

" Inaweza kufika kipindi darasa zima linawatoto, Mwalimu akifundisha wao wanatoka nje kwenda kunyonyesha".

Hata kama ni watoto wangu, yani nikupeleke shule alafu upate mimba nikurudishe? Aende akapate mimba aone kama nitamrudisha.

Mimi nimetoa fedha ili mwanafunzi asome bure, halafu leo mtu apate mimba arudi shule? Ndani ya utawala wangu, haitotokea.

Wakati mwingine ukizikiliza hizo NGOs zitakuwa zinalipeleka taifa pabaya. Ndani ya utawala wangu haitotokea. NEVER.

Hizi NGOs kama zinawapenda sana hao watoto zikafungue shule zao za kusomesha wazazi. Serikali haiwezi kuwasomesha.

Hawa wanaotuletea haya mambo hawatupendi ndugu zangu. Wametuletea dawa za kulevya, wameleta ushoga ambao hata ng'ombe hawana.

Huku kuiga iga tutakuja kuiga mambo ambayo hata hayafai. Wanakuja na misaada ambayo ni mali zetu wametuibia.

Nyie wafugaji mmefuga lakini hamjawahi kuona hata mbuzi au nguruwe amekosea huu mchezo. Lakini wao wanataka Watanzania wakosee.

Wakati huo huo, Rais amesema kuwa anawaomba msichukue maeneo ya Magereza, hata mimi nikifungwa siku moja nipate sehemu ya kulima.

Rais Magufuli ametoa eneo la ekari 65 kwa wananchi lililokuwa na mgogoro kati yao na Jeshi la Magereza.
 
Habari wanaJF,

Leo akiwahutubia wakazi wa Bagamoyo, Mkoani Pwani. Rais Magufuli amesema hakuna Mwanafunzi aliyebeba ujauzito atakayerudi shule katika utawala wake. Akaongeza kuwa hawezi kufanya kazi ya kusomesha wazazi.

" Inaweza kufika kipindi darasa zima linawatoto, Mwalimu akifundisha wao wanatoka nje kwenda kufundisha".

Wakati huo huo, Rais amesema kuwa anawaomba msichukue maeneo ya Magereza, hata mimi nikifungwa siku moja nipate sehemu ya kulima
Maneno huumba, hiyo kauli yake ya mwisho asishangae siku ikitimia
 
akiongea akiwa bagamoyo kwenye uzinduzi wa barabara ya bagamoyo msata chalinze rais amekemea vikali sana wote wanaopigia debe eti wanafunzi wazalishwe halafu waendelee na masomo, rais amesema hili haliwezekani na ole wake awaye....ole wake anatakayezaa halafu arudishwe shuleni. ole wake atakayempa mimba mwanafunzi halafu sheria imuache akirandaranda mitaani.
 
Kama kawaida ya mzee wa visasi, hivi hajui kuna watu wana chukua masters na tayari wana watoto wenye watoto.

Elimu ni haki ya kila mtu, hata kama mtoto wa sekondari kapata mimba haimaanishi hiyo haki yake inapotea, aendelezwe baadaye aje kuokoa mtoto sio kukaa anaongeza idadi ya wajinga wasio na kazi. Midingi yenye phd feki ndo haiwezi kuliona hili. Tz won't be saved by this guy, he's a joke.
 
Ameyasema hayo leo akiwa Bagamoyo kwenye uzinduzi wa barabara.

"Kwenye utawala wangu siko tayari kuruhusu ujinga kama huu, kama wanaona inafaa basi wafungue shule za wazazi ili huku wakiendelea na masomo waendelee kunyonyesha watoto wao."

Ameongeza kuwa hizo NGOs ndio zimeleta mambo ya ajabu ajabu hadi wanaume kwa wanaume kuingiliana, wanawake kwa wanawake kuingiliana.

"Hata wanyama hawafanyi hivyo mbuzi Ng'ombe huwezi kuwaona wakikosea ile sehemu...Wachungaji si mpo hapa mmewahi kuwaona mbuzi wakikosea au ng'ombe wakikosea"....aliongeza Magufuli.
 
Habari wanaJF,

Leo akiwahutubia wakazi wa Bagamoyo, Mkoani Pwani. Rais Magufuli amesema hakuna Mwanafunzi aliyebeba ujauzito atakayerudi shule katika utawala wake. Akaongeza kuwa hawezi kufanya kazi ya kusomesha wazazi.

" Inaweza kufika kipindi darasa zima linawatoto, Mwalimu akifundisha wao wanatoka nje kwenda kufundisha".

Wakati huo huo, Rais amesema kuwa anawaomba msichukue maeneo ya Magereza, hata mimi nikifungwa siku moja nipate sehemu ya kulima

Atakayefanya kama alivyosema RAIS atakuwa MZAZI mpumbavu.Kuna shule za private,kama anauwezo ampeleke mtoto wake private.

Huu ujinga ati mtoto sababu amepata Mimba asisome aupeleke Lumumba na Chato
 
Ameyasema hayo leo akiwa Bagamoyo kwenye uzinduzi wa barabara.

"Kwenye utawala wangu siko tayari kuruhusu ujinga kama huu, kama wanaona inafaa basi wafungue shule za wazazi ili huku wakiendelea na masomo waendelee kunyonyesha watoto wao."

Ameongeza kuwa hizo NGOs ndio zimeleta mambo ya ajabu ajabu hadi wanaume kwa wanaume kuingiliana, wanawake kwa wanawake kuingiliana.

"Hata wanyama hawafanyi hivyo mbuzi Ng'ombe huwezi kuwaona wakikosea ile sehemu...Wachungaji si mpo hapa mmewahi kuwaona mbuzi wakikosea au ng'ombe wakikosea"....aliongeza Magufuli.

Kuna siku ataujutia MDOMO wake
 
Mheshimiwa Raisi amesema katika kipindi chake cha utawala, mwanafunzi wa shule ya msingi hadi sekondari atakayepata mimba, hataruhusiwa kurudi shuleni.

"Awe kaipata kwa raha zake, awe kaipata kwa bahati mbaya, akishapata mimba, elimu ya serikali basi"
 
Back
Top Bottom