Rais Magufuli: Si wanafunzi wote wa vyuo vikuu watakaopewa mikopo Tanzania

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
6,825
9,532
Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema serikali ya nchi hiyo haiwezi kutoa mikopo ya kimasomo kwa wanafunzi wote wa vyuo vikuu nchini humo.

Kiongozi huyo alisema serikali yake imekuwa ikiongeza fedha za mikopo na kuwakopesha wanafunzi wengi zaidi lakini akasisitiza kuwa sasa haitaweza kutoa mikopo kwa wanafunzi wote wa vyuo vikuu.

Alidokeza kwamba watakaopewa kipaumbele ni wale wanaosomea udaktari, ualimu na uhandisi.
_101150189_2a2ea6a9-5ae2-43ec-a093-f08d94934202.jpg

Magufuli: Si wanafunzi wote watakaopewa mikopo Tanzania
 
Kwa sasa namsomesha mwanangu Primary Private School sababu mimi ni mwajiriwa nalipwa mshahara kila mwezi. Najibana bana hivyo ili dogo aweze kupata msingi mzuri wa Elimu.

By he time ana-apply chuo kikuu nitakuwa nimesaafu; sasa kigezo kipi anyimwe mkopo? sababu mimi nitakuwa nimestaafu na kama mnavyojua wastaafu wanalipwaje hapa kwetu.

Ufafanuzi, hili ni jambo muhimu sana maana linagusa wau wengi mno.
 
Madaktari, waalimu na wahandisi. Kwa hiyo hatuhitaji watu wa misitu, kilimo, wanyama pori, nyuki, uchumi, wanasheria, hali ya hewa, wahasibu, na wengine?
Pesa inataka kukatwa kijanja.

Zingekuwa ni scholarships ningemuelewa ...........!!
 
Alipo kuwa anaomba ridhaa ya Watanzania alituaminisha atatoa mikopo kwa wote tena bila ubaguzi... Akarudia mara nyingi akisema kwamba oesa zenyewe ni za mkopo kwani Watanzania wasipewe wakasoma.
Amepewa ridhaa ya kuwa Rais sasa kabadilika sio kila Mtanzania atapewa mkopo.
Ila tumuombee asiwe na kiburi ...
This is politics bhana....
 
Pesa inataka kukatwa kijanja.

Zingekuwa ni scholarships ningemuelewa ...........!!
Hii mikopo watoto wanalipa through the nose! Wanakatwa vibaya sana. Na makusanyo ya loan board yameongezeka sana mwaka huu. Sababu ya kukataa kuwakopesha haieleweki.
 
lazima mkome na bado, si wengi mnajofanya hamjali nani anakuwa kiongozi mnaendeshwa na mihemko tu wakati wa uchaguzi na si kufuatilia taarifa ili mfanye "informed decisions", matokeo yake hata sisi wengine tunajikuta tunapata shida sababu ya watu kama nyinyi.NASEMA MKOME TENA BADO NA MKOME ZAIDI NA ZAIDI HADI MUWE NA AKILI NEXT TIME!
 
Nani ana clip yake kuhusu mukopo ya elimu ya juu aloitoa wakati wa kampeni atuwekee hapa!!!
 
Hapa mlitaka aseme kila mtu atapata mkopo 100%,japokuwa mngemnanga lakini mngefurahi.
Hapa koleo ni koleo tu,siyo kijiko kikubwa.!
 
Kwa sasa namsomesha mwanangu Primary Private School sababu mimi ni mwajiriwa nalipwa mshahara kila mwezi. Najibana bana hivyo ili dogo aweze kupata msingi mzuri wa Elimu.

By he time ana-apply chuo kikuu nitakuwa nimesaafu; sasa kigezo kipi anyimwe mkopo? sababu mimi nitakuwa nimestaafu na kama mnavyojua wastaafu wanalipwaje hapa kwetu.

Ufafanuzi, hili ni jambo muhimu sana maana linagusa wau wengi mno.
Anza kumfungulia genge akirudi likizo auze
 
Back
Top Bottom