Rais Magufuli si rafiki wa vyombo vya habari

Umetumia vigezo gani kuwateua hawa mawaziri nalo ni swali? Ni bora angeuliza hivi "unatarajia nini kwa hawa mawaziri na manaibu uliowateua" au unawaeleza nini kuhusu matarajio ya Watanzania kwa serikali ya awamu ya 5. Samahani lakini. Ila waandishi wa habari tafuteni namna nzuri ya kuframe maswali ili majibu yatolewe kutokana na matakwa ya swali.

Chanzo cha vitu au kitu chochote unacho kiona ni 'wazo. Matarajio unayoyataja wewe ni matokeo yanayo letwa na vigezo.Kama hukuzingatia vigezo flani ili kuleta tija ni kazi bure. Kuteua tu bila ya kuzingatia vigezo ni ujinga unaweza kuongeza idadi ya wezi Serikalini.
 
Leo nimemuona akijibu maswali ya waandishi baada ya kutangaza baraza lake la mawaziri. Pamoja na kwamba aliitisha maswali ni wazi kwamba alikuwa akiwajibu kavu wale waliouliza pamoja na waulizaji kujitahidi kuuliza maswali ya msingi.

Mtu anauliza umetumia vigezo gani kuwateua hao kuwa mawaziri. Jibu lake ni kuwa kwani nilitumia vigezo gani kumteua Majaliwa kuwa waziri mkuu? Sisi tunajuaje? Toa ufafanuzi mkuu.

Kwa mwendo huu waandishi watasusia mambo ya msingi sana na kumwachia Msigwa kutoa habari zote za Magufuli..

He is heading to a big failure. Kichwa kimevimba hana ustaarbu, hekima na anajiona anajuwa kila kitu which is totally wrong.

Magufuli is not a presidential material
 
Safi Magufuli si mlimzoea JK tukisema Kikwete amekuuza uhuru wa habari mnaleta midomo yenu sasa hapa kazi tu!
 
Hivi kulikuwa kuna umuhimu gani wa kuungunisha wizara mbili pamoja halafu Mawaziri wakawa wawili, kwanini asingeweka wizara mbili Ijulikane wazi kuwa wizara zipo mbili?
 
Hivi kulikuwa kuna umuhimu gani wa kuungunisha wizara mbili pamoja halafu Mawaziri wakawa wawili, kwanini asingeweka wizara mbili Ijulikane wazi kuwa wizara zipo mbili?

Mkuu unapozungumzia Mawaziri wawili ndani ya wizara moja ni tofauti na kuwa na mawaziri wawili kwenye wizara mbili. UNapozungumzia Wizara unazungumzia Makatibu wakuu, wakurugenzi , wakuu wa vitengo na wafanyakazi. Ni rahisi sana kuwa na mawaziri wawili kwenye wizara kuliko kutengengeza wizara kuhalalisha uwepo wa waziri.
 
Wandishi wengi ni shida TZ. Unapomuliza ametumia vigezo gani pengine ni pale unapokuwa umeona mapungufu ya msingi kwa wateuliwa lkn unaweza kukuta mwandishi hakujiridhisha kama ndio hi yo akambilia kuuliza swali. Wandishi wengi wanapenda kuliza maswali ya kuvizia/provocating ili waonekane turn wameuliza swali. Kwa uelewa Wang rais isingejibu hilo swali
 
Wengine hatushangazwi na kauli za "rejareja" azitoazo,tumeshamzoea.Mmesahau kauli za dharau alizozitoa Kigamboni alipowaambia wasiotaka kulipa nauli ya kivuko wapige mbizi?Kama yalivyo maamuzi yake,ndivyo kauli zake zilivyo.

Wakazi wa Buziku jimbo la Chato wilayani Chato Mkoa wa Geita hawatamsahau milele pale alipowaambia wanaotaka barabara ya lami wajisaidie haja kubwa barabarani kisha yeye ataleta " buldoza" lishindilie vinyesi vyao na kuwa lami.

Ni mwanzo tu,jiandaeni kusikia yenye ukakasi zaidi.#HapaKaziTu.CCM hoyeeeeee.
 
Kiuhalisia mkuu wetu hakustaili kutoa majibu kama yale,lakini kwa upande mwingine ngoja watanzania waisome namba na bado,ukitaka kujua tabia ya mtu mpe madaraka au pesa ndioo waweza kujua tabia ya mtu ikoje.
 
utafikiri aliwapania waandishi ile si nzuri kabisa nyerere alikuwa na majibu ya aina fulani lakini akiulizwa swali la ajabu atamshushua mtu na kutoa maelezo kwa nini amejibu hivyo na pengine kueleza kwa undani hilo alilohisi lilikuwa si swali la msingi.
JPM ametuonesha wananchi kuwa hatupaswi kumuuliza maswali kwa kumbukumbu zangu jana hakuna jibu swali hata moja ila alikuwa akitoa maelezo kwa vitu alivyovitaka yeye hata kama hajaulizwa.
 
Kwani maswali walio uliza sio ya maana? ulitaka wailize maswali gani ili uone yana maana ikiwa raisi anaulizwa maswali anajibu kavu unategemea nini? aliulizwa umetumia vigezo gani kuteua mawaziri! kajibu kavu. Akaulizwa kwa nini baadhi ya wizara umeweka manaibu waziri wawili kajibu kavu akulizwa ulitoa siku saba kwa wafanya biashara wa kubwa wawe wamelipa kodi je tajari wameshalipa wote ilikuwa ni ufafanuzi tu autoe akiwa kama raisi matokeo yake anajibu kavu kavu kwa kweli raisi wangu leo kachemsha sijapenda.
Hatuna rais tuna Hitler
 
Kweli nyie ni hamnazo,,,,nashindwa kuelewa kati ya nyie na wao waandishe nani ni mjinga zaidi,,,maana baada ya tukio waandishi wote walikuwa wanafarakana kupiga picha na mhe.Rais,,,kama aliwaudhi mbona hawakusita kupiga nae picha???
 
utafikiri aliwapania waandishi ile si nzuri kabisa nyerere alikuwa na majibu ya aina fulani lakini akiulizwa swali la ajabu atamshushua mtu na kutoa maelezo kwa nini amejibu hivyo na pengine kueleza kwa undani hilo alilohisi lilikuwa si swali la msingi.
JPM ametuonesha wananchi kuwa hatupaswi kumuuliza maswali kwa kumbukumbu zangu jana hakuna jibu swali hata moja ila alikuwa akitoa maelezo kwa vitu alivyovitaka yeye hata kama hajaulizwa.

Ni kweli mkuu,alikurupuka.Badala ya kujibu swali la Manyerere,alirukia taaluma yake na kumtaka afanye hesabu mwenyewe.Hakuishia hapo,alichomoa "kablasha" na kuwaonyesha wanahabari kuwa humo kuna mabaraza ya Serikali zote duniani,je mabaraza ya serikali hizo hata yawe na ukubwa kiasi gani yanatuhusu nini Wadanganyika?
 
Pole Sana Kwa Upeo Unao Upaka Rangi,kaulizwa Katumia Vipimo Gani?Unasema Sio Ya Msingi Kwani We Huo Ushabiki Wako Upunguza Hata Bei Ya Nondoo Au Kutoa Hata Ajira 50 Tu Zaidi Ya Mji Kurundikwa Vifusi Vya Taka Hopeless

Mkitaka kuhoji uteuzi wa mawaziri badilisheni katiba ili wathibitishwe na bunge. Kwa sasa mnapiga kelele bure Mwacheni rais na wateule wake wafanye kazi.
 
Safi Magufuli si mlimzoea JK tukisema Kikwete amekuuza uhuru wa habari mnaleta midomo yenu sasa hapa kazi tu!

Kwa Hiyo mtoto wako akidai chakula zaidi ili ashibe wewe unaona ni bora kumpunguzia ili umkomeshe? Mwananchi alikuwa na haki ya kudai haki zaidi ya Uhuru wa habari toka awamu ya NNE na hata sasa.
 
Hivi kulikuwa kuna umuhimu gani wa kuungunisha wizara mbili pamoja halafu Mawaziri wakawa wawili, kwanini asingeweka wizara mbili Ijulikane wazi kuwa wizara zipo mbili?
Julius Mtatiro ni miongoni mwa waumini wa taasisi imara badala ya watu binafsi walio imara.
Haiwezekani kila mtu akawa anaibuka na kuunda au kufuta wizara kadri atakavyo. Tunavyosema taasisi basi kuwepo hata majengo permanent ya wizara hizo kwa maana kwamba hizo wizara ziwepo kikatiba walau kwa 90%.

utafikiri aliwapania waandishi ile si nzuri kabisa nyerere alikuwa na majibu ya aina fulani lakini akiulizwa swali la ajabu atamshushua mtu na kutoa maelezo kwa nini amejibu hivyo na pengine kueleza kwa undani hilo alilohisi lilikuwa si swali la msingi.
JPM ametuonesha wananchi kuwa hatupaswi kumuuliza maswali kwa kumbukumbu zangu jana hakuna jibu swali hata moja ila alikuwa akitoa maelezo kwa vitu alivyovitaka yeye hata kama hajaulizwa.

Nilisikia part ya majibu yake,si mazuri kwa nafasi aliyonayo.Itafika siku atasema wenye maswali hata kama kuna swali la msingi hawatamuuliza.Wataondoka na kuandika magazetini.

Alijitanabaisha kuwa MNYENYEKEVU kwa majibu yale unyenyekevu hakuna.Kama kulewa madaraka basi ni mapema mno.
 
Back
Top Bottom