Mr pianoman
JF-Expert Member
- May 22, 2019
- 2,548
- 6,102
Kabla ya yote mtanisamehe katika uandishi wangu, lakini huu ndio ujumbe wangu kwa Mheshimiwa Magufuli.
Mheshimiwa Rais, popote usomapo ujumbe huu nakusihi chukua hatua stahiki kwani siku zote neno la Rais ni sheria.
Mheshimiwa Rais, corona sio tena kaugonjwa kama ulivyo uita hapo awali kwani mpaka saivi tayari imesha kuonyesha rangi yake halisi.
Mheshimiwa Rais, jitokeza sasa utoe japo tamko dogo tu la watu kuvaa japo barakoa (facemask) kwa nchi nzima, kwani kwa kufanya hivyo itasaidia kupunguza maambukizi ya virusi hivi. Acha kuwaachia wakuu wa mikoa kwani kuna wakuu wa mikoa tayari wamesha poteza muelekeo hawajui cha kufanya.
Mheshimiwa Rais, nchi saivi haina tena amani kama ulivyo zoea kulitamka hili neno kwenye mikutano yako kwani tumevamiwa na adui asiye onekana hivyo inahitaji akili kubwa kumshinda.
Mheshimiwa Rais, najua zoezi la kuwaweka wananchi wote ndani ( lockdown) ni ngumu kwako kutokana na maswala ya kiuchumi (na mimi kwa hili nakuunga mkono kwa asilimia mia). Ila jaribu kuweka mazingira salama ya wananchi wako huko wanapo jitafutia liziki zao ili tusiendelee kuongeza tatizo juu ya tatizo.
Mheshimiwa Rais, ni vitu vidogo tu vya kuwekea mkazo kupambana na ugonjwa huu kama:
- Uvaaji wa barakoa (facemask) kwa kila mwananchi.
- Vyombo vya usafiri kuzingatia sheria za usafi na kupunguza mibanano ndani ya gari. Hii izingatiwe nchi nzima hata kule vijijini
- Kuwe na timu za unyunyiziaji dawa kila sehemu inayo kaliwa na watu wengi kama stendi za mabasi na sehemu nyingine kama hizo (hapa nahisi lile jeshi lako pendwa la JKT litafaa zaidi katika operesheni hii kwani halijawahi kushindwa katika operesheni zake )
- Weka muda wa mwisho wa watu kufanya kazi ili kupisha operesheni hii ya kupiga dawa sehemu husika ili lifanikiwe zaidi.
- Panapo wezekana watu kunawa mikono naomba hilo suala lifanyike kwa usimamizi mkali sana. Sehemu kama kuingia masoko makuu na stendi kubwa kubwa inawezekana kabisa zoezi hili kufanyika kwani sehemu hizi huwa na sehemu zake maalum za kuingia na kutoka.
Mheshimiwa Rais, huu ndio muda muafaka sasa wa kutumia jeshi la polisi kulinda raia wake. Inawezekana polisi wakawa wachache katika kusimamia hili jukumu kutokana na nchi yetu ilivyo kubwa Lakini hili sisi wananchi halituhusu sana maana jukumu la kuajiri polisi kila mwaka ni lako kama ulifanya uzembe ndio ujifunze sasa kuwa nchi inahitaji polisi wa kutosha.
Mheshimiwa Rais, nimekueleza hayo kwani ukitamka wewe litatekelezwa kwa asilimia kubwa kuliko kuwaachia hao watendaji wako ambao matamko yao yanapishana kila kukicha.
Kwa kukukumbusha tu mheshimiwa Rais usijiaminishe sana na amani iliyopo kwenye nchi kwani siku zote kutoka kwenye amani kuja kwenye vita huwa ni kasi ya 5G. Na kutoka kwenye vita kurudi kwenye Aman huwa ni spidi ya kobe.
CHUKUA HATUA MAPEMA.