Rais Magufuli, Ruhusu usafiri (Mabasi) yasafiri usiku

nickag

Member
Jan 2, 2016
64
29
Ndugu za Watanzania ajira ni nyingi sana iwapo tutaruhusu uchumi wetu ufanye kazi masaa 24 kwa kuanzai na usafirishaji.

Mfano mzuri ni wenzetu wakenya, vijana wanafanya kazi masaa yote na wananchi hawapotezi muda kusafiri kwani unaeza safiri muda uliotakiwa kuwa kitandani na asubuhi ukaendelea na shughul zako.

Sasa hapa kwetu ni majanga, safari Dar - Kigoma hadi ulale barabarani sababu gari hazitembei, kitu cha kufanya siku moja unatumia siku tatu sababu gari hazitembei usiku na matochi bararabani kero tupu.
 
Hapana,siungi mkono hoja, usiku huwa kuna madhara mengi!Hata nami huwa nina haha mno kwa baadhi ya madereva nyakati wa usiku wanapopishana kwa kuwasha fulllight na wengineo hukuwashia sportlight, hii ni chanzo kikuu cha ajali nyingi.
 
Zipo Baadhi Ya Barabara Kama Dar-Arusha.
Dar-Dodoma.
Dar-Moro
Na Baadhi Ya Sehemu, Lakn Kuna Barabara Hazifai Kupita Usiku Hata Kama Ni Lami, Hata Hivyo Kutembea Usiku Kucha Sio Kukuza Uchumi.

Maroli Yanaruhusiwa Kwa Baadhi Ya Sehem Ambazo Hazifungamani Na Hifadhi Ya Wanyama Lakn Kwa Mabasi Ya Abiria Ni Hatari Coz Mnaweza Kupata Tatzo Njiani Gari Ikaharibika Halafu Mwisho Wa Siku Mnailaumu Serikali Kutowapa Msaada Kwa Wakati
 
Naona mmejipanga kuteka
 
Hii kusafiri mchana tu, iliamliwa kwa lengo zuri tu ajari baba, madere wetu ukiwapa uhuru Sana, roho zetu huziamria Wao. wakati gani tufe hebu angalia hii picha hapo chini, iliyowahi kuwekwa na member mmoja hapa, tena hii mchana kweupe je usiku.
wp_ss_20160501_0001.png
 
Ndugu za Watanzania ajira ni nyingi sana iwapo tutaruhusu uchumi wetu ufanye kazi masaa 24 kwa kuanzai na usafirishaji.

Mfano mzuri ni wenzetu wakenya, vijana wanafanya kazi masaa yote na wananchi hawapotezi muda kusafiri kwani unaeza safiri muda uliotakiwa kuwa kitandani na asubuhi ukaendelea na shughul zako.

Sasa hapa kwetu ni majanga, safari Dar - Kigoma hadi ulale barabarani sababu gari hazitembei, kitu cha kufanya siku moja unatumia siku tatu sababu gari hazitembei usiku na matochi bararabani kero tupu.
Unajua ni kwanini walisitisha safari za usiku?
 
Mkuu nakuelewa sana serikal inampango mzuri wa kuokoa maisha na kutulinda dhidi ya ujambazi...lakin self displine ndo dawa ya kila kitu istoshe kuna spid gavana..ambazo hazgaguliwi vizur kwenye mabas wakihakikisha zinafanya kaz hakuna ajir za spid mchana hata usiku.
Suala la ujambaz kuna vyombo vya usalama mfano mzur n jeshi la wananchi na jkt hawana kazi ya moja kwa moja kwanini wasiweke kambi barabarani na kufanya patrol usiku kuhakiki ujambaz wa mabasi unadhibitiwa na ukitokea mkuu wakizuizi anawajibishwa tunatakiwa kufanya kaz na kupunguza muda wa kusafir tanzania
 
Kweli kabisa dunia ya leo kuweka mwisho wa muda kusafiri usiku ni kujiweka nyuma kimaendeleo, na kupoteza muda. Muda unapaswa kuthaminiwa kama tunataka kuenendelea kwa kiasi kinachotakiwa.
 
Zipo Baadhi Ya Barabara Kama Dar-Arusha.
Dar-Dodoma.
Dar-Moro
Na Baadhi Ya Sehemu, Lakn Kuna Barabara Hazifai Kupita Usiku Hata Kama Ni Lami, Hata Hivyo Kutembea Usiku Kucha Sio Kukuza Uchumi.

Maroli Yanaruhusiwa Kwa Baadhi Ya Sehem Ambazo Hazifungamani Na Hifadhi Ya Wanyama Lakn Kwa Mabasi Ya Abiria Ni Hatari Coz Mnaweza Kupata Tatzo Njiani Gari Ikaharibika Halafu Mwisho Wa Siku Mnailaumu Serikali Kutowapa Msaada Kwa Wakati
Kenya ya abiria unatoka Mombasa kwenda Nairobi saa MOJA na nusu usiku unafika alfajiri
 
Nivyema serikali ikaliangalia upya swala la usafiri wa mabasi mikoani mda wa usiku ni aibu kuona nchi yenye amani na utulivu kutokua na huduma muhimu kama hii kwa kigezo cha usalama. Usafiri usiku una faida kubwa sana kiuchumi na hasa kwa wafanya biashara wadogo. Hivyo basi ombi kwa serikali irudishe huduma ya usafiri wa mabasi nyakati za usiku.
 
Kenya ya abiria unatoka Mombasa kwenda Nairobi saa MOJA na nusu usiku unafika alfajiri
Kweli kabisa kama mtu unashughul ya kufanya mombasa kesho asubuh unaondoka usiku asubuhi unafanya kaz ako jion unarud huna haja ya kukaa kwenye basi siku nzima..
 
Na wazo zuri sana ila sio njia zote ni salama kupia usiku wa manane!!

Duc In Altum.
Usalama wa nchi ni rahis sana tuna jeshi kuna polisi wafanye patrol barabara kuu miji mikubwa mfano mwanza to dodoma dodoma dar arusha dar kahama mwanza
 
Hapana,siungi mkono hoja, usiku huwa kuna madhara mengi!Hata nami huwa nina haha mno kwa baadhi ya madereva nyakati wa usiku wanapopishana kwa kuwasha fulllight na wengineo hukuwashia sportlight, hii ni chanzo kikuu cha ajali nyingi.
Tunasafir mchana lakin ajal ni nying mno..kwa kusafir usiku magar ni machache barabara ni tulivu watembea kwa miguu waendesha baiskel na boda ni wachache ni salama zaidi..madereva wanapewa utaratib tu kwa mfano kenya bas linatakiwa kuwa na madereva wawil kubadilishana ukisafir usiku mchana unapumzika..
 
Kuzuia mabasi kusafiri usiku si kwa sababu ya Usalama isipokuwa nitokana na ajali muda wa usiku. Kwani dereva anachoka
 
Back
Top Bottom