Rais Magufuli: Polisi kamateni hata gari la Rais

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,172
23,974
Wakati akizungumza na Maafisa wa Jeshi la polisi aliowapandisha vyeo vya Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli alisema kipindi cha nyuma jeshi la polisi lilikuwa linaweka historia mbaya.

Kuna baadhi ya polisi waliowahi kuumizwa siku za nyuma kutokana na kusimamia sheria. Kuna magari au mabasi ya wakubwa ndani ya polisi ambayo ilikuwa ukiyakamata unapata msukosuko kikazi na kimaisha.

Rais akatolea mfano akisema kulikuwa na mabasi yanayoitwa Buffalo, Happy Nation au Happy Tanzania ambayo ukiyagusa lazima utaondolewa kwenye cheo ulichopo.

Rais akawaomba Makamishna kwenda kufanya kazi bila woga na wahakikishe pia hawawabughudhi Maaskari walio chini yao wakati wanatimiza majukumu yao ndani ya sheria na Kanuni za utumishi wao.

‘’Hata kama askari atakamata gari la IGP, RPC, Waziri au Rais, mwacheni atimize majukumu yake ili wahusika wa hayo magari wakajieleze wenyewe mbele ya sheria. Sheria ni msumeno’’. Rais alisema.

Rais aliendelea kusema, ‘’tunawanyima nguvu hawa Maaskari wa chini wanapotimiza wajibu wao kwa mujibu wa sheria halafu tunawaambia liachie hilo gari. Akishatoka pale yule aliyekuwa amekamatwa huanza kutamba kweli kweli huku askari akiwa amevunjika moyo na nguvu katika kusimamia sheria. Niwaombe sana, Vyeo vyetu tuweke pembeni na sheria tuziweke pembeni’’.
 
Happy Nation kuna mkono wa Said ..............ma. Ila Bufalo ilikuwa kampuni ya Mpare fulan sijajua kama kuna wakubwa waliingiza mikono yao huko.

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
Thanks.

Ninaamini comment yako itasaidia wengi katika uelewa pamoja na kwamba huna uhakika kuhusu Buffalo.
 
Waimbaji wimbo wa "ni Dikteta, ni Dikteta" hutawasikia wakinukuu haya. Hawatasema Dikteta anataka watu watendewe kwa mujibu wa sheria. It doesn't fit their twisted narrative.
Kilicho cha muhimu ni kwamba, hawa wenye twisted narrative ukizifahamu motives zao, huwezi kusumbua fikra.

Itikadi za kisiasa kwa sasa zimewanya baadhi ya watu kuwa wajinga zaidi.
 
Waimbaji wimbo wa "ni Dikteta, ni Dikteta" hutawasikia wakinukuu haya. Hawatasema Dikteta anataka watu watendewe kwa mujibu wa sheria. It doesn't fit their twisted narrative.
Hivo hivo, anapopigia chapuo "hela ya kubrush viatu" ya trafik hatuwasikii waimbaji wa Wimbo wa "ni mtukufu ,ni mtukufu" mkinukuu hayo.

"Amlipaye mpuliza zumari,ndiye ........" - by unknown
 
Hivo hivo, anapopigia chapuo "hela ya kubrush viatu" ya trafik hatuwasikii waimbaji wa Wimbo wa "ni mtukufu ,ni mtukufu" mkinukuu hayo.

"Amlipaye mpuliza zumari,ndiye ........" - by unknown
Ulikuwa unawasikia waimbaji wa wimbo gani?

Wewe unalipwa na nani kupuliza zumari?
 
Wote wana twisted narrative. Huyo mwanakijiji huibuka yakitajwa yasiyokinzana na norms. Hakutokea kwenye sukari, ajira nk. Huyo si mwanakijiji tena bali mwanamji
Wewe ulitokea kwenye ajira, sukari, nk?

Kwa nini unataka atokee?
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom