kweli umeshtukia kama jiwe ni stupid, so you trying to play his rhythm to get on to the blues. kweli his is stupid but he is not a fool, ukuu wa wilaya haupatikani hivi, na kitu kizuri anakujua aliwahi kukwambia Mayalla means NJAAA.Wanabodi,
Hili ni bandiko la kuhamasisha uzalendo wetu kwa sisi Watanzania wazalendo wa kweli wa taifa hili ambao tusingependa kuona uhuru wa taifa letu unaingiliwa na taifa jingine lolote au mtu mwingine yoyote. Huu ni wakati wa sisi Watanzania wazalendo wa kweli wa taifa hili kusimama as one kulitetea taifa letu against mabeberu, wakoloni mambo leo na vibaraka wao, dhidi ya maslahi mapana ya taifa letu.
Najua rais wetu Dr. John Pombe Joseph Magufuli atalihutubia taifa next week kujibu vitisho vya EU na US, sisi wazalendo wa kweli wa nchi hii, tunamsisitiza,
Never bow down to anyone, nether US, nor EU or anybody else, he should tell them that Tanzania is a Sovereign state, hatupangii nchi nyingine cha kufanya, hivyo na sisi hatupangii cha kufanya.
Kama hoja ni kufifisha democracy na ukiukwaji wa haki za binaadam, nchi ngapi zina bad democracy zaidi yetu na mmenyamaza, nchi ngapi zina worst human rights records kuliko sisi na mmenyamaza?. Tanzania tunafuata African democracy na Tanzania democracy, kama tumeamua mikutano ya siasa ni wakati wa kampeni tuu za uchaguzi mkuu, na baada ya uchaguzi ni wakati wa kufanya kazi, watu wote tufanye kazi ya kuijenga nchi, then hii ndio demokrasia yetu na hizi ndio human rights zetu, wasituingilie kwa kuimpose demokrasia modal yao na human rights standards zao kwetu!.
Watetezi we ubeberu watasema kwa vile sisi ni nchi masikini, na bajeti yetu inategemea misaada na mikopo ya nchi tajiri, hivyo ni lazima tuwapigie magoti kufuata wanachotaka, this time tuwagomee kuulinda uhuru wetu na sovereignty yetu, kama vipi bora waende tuu, ni heri tubaki masikini jeuri huru kuliko utumwa wa mabeberu kwa uhuru wa bendera, huku tukipangiwa kila kitu na mabeberu hawa.
Kama hoja ni umasikini, Tanzania ya leo sio masikini kivile hadi tuuze uhuru wetu kwa kuwanyenyekea mabeberu hawa. Kama tumeweza kununua ndege kwa cash tena fedha zetu wenyewe za ndani, sasa tunajenga reli ya SGR na mradi wa Stigle Gorje kwa fedha zetu wenyewe za ndani, then tukiamua kuijenga Tanzania bila misaada ya wazungu, tunaweza, tunaweza kupanga bajeti ya kile tuu tunachokusanya, ili tusiwategemee wafadhili katika bajeti zetu ili tusidhalilishwe kama sasa na hawa US na EU hadi kutuingilia uhuru wetu, kumpangia rais wetu.
P
Rejea za kuhamasisha uzalendo
Hata Nyerere alikataa, Rais Magufuli usikubali, shikilia msimamo. Tz tusikubali misaada na mikopo yenye masharti kuingilia sovereignty yetu - JamiiForums
Kumbe watu wa Nyerere bado wapo na wana misimamo kama Nyerere. Hongera MFA, Dr. Mahiga kwa msimamo, tusikubali kuyumbishwa - JamiiForums
Uzalendo wa Ajabu wa Watanzania, Nchi Yako Inatukanwa!, Rais Wako Anatukanwa!, Tumenyamaza!. Huu Ni Uzalendo Gani?!. - JamiiForums
Serikali yetu Kuitwa "Sinister" na "Authoritarian": Je, ni kweli? Kama si kweli, Tusiukubali Uongo huu, Tuukanushe! - JamiiForums
Tusikubali udhalilishaji wa Jarida la The Economist, lamwita Rais wetu "Dinasauria wa Dodoma” na "bullheaded socialist" - JamiiForums
Huku sio kudhalilishwa kwa Rais wetu na Media za Nje? Je, watanzania tukubali, Tukae kimya? - JamiiForums
Watanzania kwanini tunakubali Rais wetu adhalilishwe na media za nje kwa kuitwa "The 'Bulldozer' Tanzanian President"? - JamiiForums
Serikali ikanushe uongo huu wa SABC kumsema vibaya Rais wetu Magufuli kuwa ni Dikteta! - JamiiForums