Rais Magufuli, please don't bow down kwa hawa mabeberu wa US na EU, waeleze Tanzania ni nchi, a sovereign state

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,468
113,583
Wanabodi,

Hili ni bandiko la kuhamasisha uzalendo wetu kwa sisi Watanzania wazalendo wa kweli wa taifa hili ambao tusingependa kuona uhuru wa taifa letu unaingiliwa na taifa jingine lolote au mtu mwingine yoyote. Huu ni wakati wa sisi Watanzania wazalendo wa kweli wa taifa hili kusimama as one kulitetea taifa letu against mabeberu, wakoloni mambo leo na vibaraka wao, dhidi ya maslahi mapana ya taifa letu.

Natoa wito kwa rais wetu Dr. John Pombe Joseph Magufuli never bow down to anyone, nether US, nor EU or anybody else, he should tell them that Tanzania is a Sovereign state, hatupangii nchi nyingine yoyote kitu cha kufanya, vivyo hivyo na sisi hatupaswi kupangiwa na yeyote kitu chochote cha kufanya nchini mwetu, kupangiwa chochote cha kufanya na yeyote wa nje ya nchi yetu ni kuingiliwa mambo yetu ya ndani.

Kama hoja ni kufifisha democracy na ukiukwaji wa haki za binaadamu, nchi ngapi zina bad democracy records kuliko sisi na wamekaa kimya, why we?. Nchi ngapi zina worst human rights records kuliko sisi na mmenyamaza?. Tanzania tunafuata African democracy na Tanzania democracy, kama tumeamua mikutano ya siasa ni wakati wa kampeni tuu za uchaguzi mkuu, na baada ya uchaguzi ni wakati wa kufanya kazi, watu wote tufanye kazi ya kuijenga nchi, then hii ndio demokrasia yetu na hizi ndio human rights zetu, wasituingilie kwa kuimpose demokrasia modal yao na human rights standards zao kwetu!.

Watetezi we ubeberu watasema kwa vile sisi ni nchi masikini, na bajeti yetu inategemea misaada na mikopo ya nchi tajiri, hivyo ni lazima tuwapigie magoti kufuata wanachotaka, this time tuwagomee kuulinda uhuru wetu na sovereignty yetu, kama vipi bora waende tuu, ni heri tubaki masikini jeuri huru kuliko tajiri utumwa wa mabeberu kwa uhuru wa bendera, huku tukipangiwa kila kitu na mabeberu hawa!.

Kama hoja ni umasikini, Tanzania ya leo sio masikini kivile hadi tuuze uhuru wetu kwa kuwanyenyekea mabeberu hawa. Kama tumeweza kununua ndege kwa cash tena fedha zetu wenyewe za ndani, sasa tunajenga reli ya SGR na mradi mkubwa wa umeme wa Stigler Gorje kwa fedha zetu wenyewe za ndani, then tukiamua kuijenga Tanzania bila misaada ya wazungu na mabebe hawa, tunaweza, tayari tumeisha anza kukusanya trilioni kwa mwezi kwenye makusanyo yetu ya ndani, hivyo tukiamua, tunaweza kupanga bajeti ya kile tuu tunachokusanya, ili tusiwategemee wafadhili na mabeberu katika bajeti zetu ili tusidhalilishwe kama sasa na hawa US na EU hadi kutuingilia uhuru wetu, kumpangia rais wetu nini cha kufanya!.

P
Rejea za kuhamasisha uzalendo
Hata Nyerere alikataa, Rais Magufuli usikubali, shikilia msimamo. Tz tusikubali misaada na mikopo yenye masharti kuingilia sovereignty yetu - JamiiForums

Kumbe watu wa Nyerere bado wapo na wana misimamo kama Nyerere. Hongera MFA, Dr. Mahiga kwa msimamo, tusikubali kuyumbishwa - JamiiForums

Uzalendo wa Ajabu wa Watanzania, Nchi Yako Inatukanwa!, Rais Wako Anatukanwa!, Tumenyamaza!. Huu Ni Uzalendo Gani?!. - JamiiForums

Serikali yetu Kuitwa "Sinister" na "Authoritarian": Je, ni kweli? Kama si kweli, Tusiukubali Uongo huu, Tuukanushe! - JamiiForums

‪Tusikubali udhalilishaji wa Jarida la The Economist, lamwita Rais wetu "Dinasauria wa Dodoma” na "bullheaded socialist" - JamiiForums

Huku sio kudhalilishwa kwa Rais wetu na Media za Nje? Je, watanzania tukubali, Tukae kimya? - JamiiForums

Watanzania kwanini tunakubali Rais wetu adhalilishwe na media za nje kwa kuitwa "The 'Bulldozer' Tanzanian President"? - JamiiForums

Serikali ikanushe uongo huu wa SABC kumsema vibaya Rais wetu Magufuli kuwa ni Dikteta! - JamiiForums
 
Endeleeni tu kumlisha matango pori.
Huyu hatumii fake ID(anafahamika) hivyo ni lazima awe mjanja(sometimes atalazimika ku-balance) katika kuwasilisha mada zake ili awe salama.

Nina wasiwasi anaweza kuja kumtaja either kimafumbo au waziwazi lakini kwa kumsema kwasababu kamshikia sana bango kuhusu hii issue na ninasema hivi nikiamini JPM anapita humu na kusoma yanayoandikwa.

Alll in all,sisi ni masikini sana kujaribu kushindana na hawa mabwana na tunachokifanya ni sawa na kukimba mbio za sakafuni.
 
Ni aibu Wazungu waje wakukumbushe, kulinda haki za wasichana waliobakwa wakazaa wakiwa wanafunzi, Ni aibu kusubiri Wazungu waje wakuhoji kwanini watu wanaokukusoa wanauawa, wanatekwa, wanalemazwa, Ni aibu kusubiri Wazungu waje wakuambie heshimu katiba ya nchi yako uliochaguliwa kwayo na kuahidi kuilinda, Ni aibu kusubiri Wazungu waje wakuambie unalo Bunge, liheshimu etc

Ni aibu aibu aibu.
 
Mkuu mambo haya yanahitaji hekima zaidi kuliko huu ushabiki wako wa kutaka kujulikana na mheshiwa rais au kwa manufaa unayoyajua wewe mwenyewe. Kama mhe. rais anapitia haya mawazo ya watu wa mtandaoni basi Hekima ya Mungu imuongoze sana sana..naamini kuna watu hamumpendi mh. rais na kwa hiyo mnataka mumuingize mkenge ili mumcheke pembeni. Mheshimiwa rais, nakuombea kwa Mungu ktk hili uipitishe Tanzania salama.

Kuna watu hawaipendi Tanzania kwa namna ya ushauri wanaotoa na nashawika kusema mtoa post anaweza kujumuishwa. Ktk zama kama hizi za mfumo bepari unaotawala dunia huwezi kuivimbia Western world hata mara moja. China wenyewe wamewekewa vizuizi na kampuni yao ya Huawei sisi ni akina nani kiuchumi mpaka tuivimbie EU/ USA kwa staili ya mtoa mada anavyobainisha.

Pasko, jitafakari ushauri unaompa mheshimiwa rais kwa kisingizio cha wewe kuwa mzalendo saana kuliko wengine.
 
Back
Top Bottom