Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Ombeni Sefue anapobadilishwa na balozi John William Kijazi katika ofisi ya katibu mkuu kiongozi, maana yake ni kwamba Rais Magufuli anafikia hatua za mwisho za upangaji wa safu ya uongozi anayoiamini yeye. Sidhani kama Rais Magufuli na Ombeni Sefue walikuwa hawaivi kikazi, wote ni wasomi wakubwa, wenye kujua ni namna gani watu wawili hupaswa kuishi kikazi. Ninachoamini ni kwamba Balozi Kijazi anao ukaribu zaidi na Rais kuliko Balozi Sefue. Kunaweza kuwepo kwa chemistry kubwa kati ya JPM na balozi Kijazi.
Rais Magufuli anayehakikisha kuwa watu wake muhimu wapo karibu naye kikazi, bado hajamaliza kujipanga ili aingie kazini kwa asilimia 100. Ipo minong'ono kwamba Rais hakitaki cheo cha uenyekiti wa CCM, inasemekana hapendi ule "uswahili" unaombatana na shughuli nyingi za chama. Lakini siku alipokabidhiwa cheti pale diamond jubilee na kwenda kuhutubia Lumumba, aliongelea kwa ukali kabisa suala zima la unafiki ndani ya chama. Hivyo hata akiukwepa uenyekiti wa CCM, bado hawezi kuukwepa ushawishi wa CCM katika utendaji kazi wa serikali yake. Hulka zake za kupenda uwazi katika ufanyaji kazi ni lazima zingizwe kwenye chama.
Ni lazima CCM ikombolewe kutoka kwenye siasa za majungu, kificho na kupigana vijembe. Ni lazima ikombolewe kutoka kwenye maisha ya mizengwe. Uhusiano wa CCM na serikali umeweza kuingiza tabia nyingi mbaya katika mfumo wa serikali, huu ukweli rais anaufahamu kuliko mimi. Vyama vya siasa (CCM ikiwemo) vimekuwa na tabia ya kutokuwa na uwazi wa matumizi na mapato ya fedha, matokeo yake hata zile report za CAG zinakuwa zinakosa kutazamwa kwa jicho lenye uchungu na mali ya taifa zima. Rais ambaye ameifumua TAKUKURU na ofisi ya DPP, anayo kila sababu ya kuingiza ushawishi wake ndani ya CCM, kama chama chenye nguvu nchini.
Kuharibika kwa siasa kwenye suala la maadili, kuna uhusiano na uharibikaji wa maadili kwenye maisha ya kisiasa, kijamii na kiuchumi. Rais Magufuli anayo kila sababu ya kujiweka karibu na chama ili kukirudisha kwenye zile zama za nitasema kweli daima fitina kwangu ni mwiko. Fitina itatoka CCM kama rais Magufuli akiweza kusimamia katika imani yake kwenye uwazi na kutokuwepo kwa unafiki ndani ya CCM.
Rais Magufuli peleka ushawishi wako ndani ya CCM, baada ya kuwa unakaribia kupanga kikosi chako cha kazi serikalini.