Rais Magufuli, pamoja na ukali wako bado kuna wanaokutania huku Mtwara

ngongoti2000

JF-Expert Member
Nov 20, 2017
1,308
2,000
Katika mkoa huu nimefanikiwa kutembelea Halmashauri za Wilaya mbili Newala na Masasi. Kwa mshangao wangu bado nimekuta kuna makaburi ya miaka ile bado hayajafukuliwa kama ifuatavyo;

1.Newala
Mpaka leo hakuna maji, ukiuliza sababu eti viongozi wana miradi yao binafsi ya maji wakiongozwa na Mbunge ambaye anasema yeye ni Mbunge wa maisha. Wananchi wamechoka kabisa sababu jamaa ana maguvu siyo ya nchi hii hivyo hawana pa kusemea wanasota ile mbaya na shida ya maji. Hutakiwi kuongelea jinsi ya kutatua shida ya maji katika Wilaya hii.

2.Masasi
Mpaka leo hakuna umeme wa uhakika, hili ni tatizo la miaka mingi iliyopita. Nimejaribu kuulizia japo kupata maelezo ya kitaalam lakini nimeambulia maelezo ya kisiasa. Mheshimiwa Rais, viongozi wa kule bado wanaishi style ya miaka ile ya michakato. Hebu fanya kama umepotea halafu uende kuongea na wananchi wa kule.

Au kama vipi huwa kuna kipindi cha TBC kinachoelezea maendeleo ya miaka mitatu ya awamu ya tano kwa kila mkoa. Wajaribu kwenda kuwahoji wahusika wa kule
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
4,266
2,000
Nchi hii kila kitu anahusishwa Rais kuamua! Kwani hana wasaidizi na wawakilishi wake huko Mtwara? mfano Dc, Rc, nk!

Hamuoni kumtwishwa kila jambo alifanyie maamuzi itafikia wakati atachoka! Hivi hao wasaidizi wake wanafanya shughuli gani huko!! Anyway wasalimie sana jamaa zangu 'makangomba' na uwape pole nyingi kwa mkasa uliowakuta mwaka uliopita kwenye ishu ya koro-show!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom