Rais Magufuli: Njooni wote wenye mizigo nami nitawapumzisha mizigo yenu; CCM ya sasa imeshajisahihisha

Kauli ya Nooni kwangu nyie mnaolemewa na mizigo niwapumzushe, haisadifu yale yanayotokea kwenye chaguzi hizi hata kidogo.
Mwenyewe hajaweza kunukuu hayo maandiko.
 
Hivyo, Rais Dk. John Pombe Magufuli amekiri wazi kuwa, CCM iko kwa ajili ya wenye mizigo na wana wapitevu, waliokimbia CCM ikiwa imesongwa na makandokando.
Magufuli anawakumbusha wote wenye nia ya kuhamia CCM: Jitieni nira mioyoni mwenu kwa kuwa Mimi ni msafi.

Anadhani akichukua viongozi wa upinzani ndio atakubalika, ila hizi chaguzi za marudio ndio amefahamu yeye na chama chake hawakubaliki hivyo wanavyojidanganya. Kwanza watu wengi hawapigi kura, na hao wachache wengi wao hawaipi ccm. Na ili kuficha aibu ya kutokukubalika ndio kunafanyika uporaji na ukatili wa wazi ili ccm ishinde. Na huko mbeleni ndio idadi itashuka zaidi.

Jambo hili linamnyima raha kupita kiasi, kwani hamna kitu kibaya kama uone uko sawa na kufanya kika kitu lakoni bado usikibalike. Mapenzi ya kulazimisha hayana nafasi enzi hizi.
 
Mimi naona sio sahihi kuwachukua waliokwambia unamakosa mpaka ukajirekebisha. Makosa ni jambo la kawaida kufanyika kwa mtu mmoja mmoja hata kwa taasisi kubwa km ilivyo ccm. Km ccm imejirekebisha km mwenyekiti anavyosema bado inawezakufanya makosa nahao waliokuwa upande wa pili yaani wapinzani japo sio jina nzuri sana, wataendelea kukusema na utajirekebisha. Si kweli kwamba ccm n serikali yake hatafanya makosa. Makosa ni sehemu ya maisha. Ss wote wakirudi ccm nani atasema umekosea?
 
Ni wakati sasa vyama pinzani kuingia serikalini kipitia CCM na lenu moyoni..
siku moja unakuta serikali nzima ni nyinyi kasoro kipara..
hapo mnamsukumiza tena kwa nyuma kama alivyofanywa kabla !
 




Rais na Mwenyekiti wa CCM, Dk. John Pombe Magufuli, leo baada ya kupitisha majina ya waliopitishwa kugombea ubunge kwa majimbo ya Korogwe Vijijini, Ukonga na Monduli, amewaasa walioko Upinzani kujiunga na CCM kwa kuwa, wameshajisahihisha.

Mwenyekiti huyo amewaita Wapinzani kuingia CCM kwa kusema kuwa:Njooni wote mnaosumbuliwa na mizigo, nami nitawapumzisha.

Dk. Magufuli aliwasifia wanaojiunga na CCM na kusema wanafanya uamuzi wa kishujaa na kuji-sacrifice. Aliongezea kuwa, wanahamia CCM kwa kuwa huko waliko wanakutana na figisufigisu nyingi zaidi.


huyu kilaza atampumzisha nani anatumia maneno ya Mungu kwenye ushetani wa CCM? na alaaniwe mnoo
 
Wananchi mitaani wanaishi kama watu waliokosa mtetezi kwa kupigwa na ugumu wa maisha uliosababishwa na utawala wake,anawaita wapinzani wahamie CCM wakapumnzishwe badala ya kuwapumnzisha mamilioni ya wananchi wanaoteseka.
 
Back
Top Bottom