Rais Magufuli njoo Mtumba Dodoma usikilize kero kutoka kwa wananchi

Jacobo John

Member
Apr 5, 2020
19
2
Napenda kutoa vielelezo vya madai yetu ambayo tunaambiwa ni batili. Ardhi Jiji la Dodoma kuna watu wafuatao sio waadilifu. Mwakasitu, Piusi hawa ni wadhamini pamoja na Mafuru Mkuu wa Idara amabye yupo hapo kwa manufaa ya Mkurugenzi wa Jiji lanapiga fedha za dili balaa.

Hawa ni baadhi ya wanaodai tumeandika barua nyingi Mhe. Rais lakini tunahisi zinaficha hazikufikii, tumafanya jitihada za kukusimamisha kwa mabango lakini Mkurugenzi was Jiji anatuma watu ambao Ni po polisi wanatukamata na kutunyang'anya mabango.
IMG_20200406_143513_0.jpg
IMG_20200406_144144_2.jpg
IMG_20200406_144139_1.jpg
1586177371257.png
1586177511404.png

IMG_20200406_144059_1.jpg
1586177615309.png
1586177721255.png
IMG_20200406_143800_1.jpg
IMG_20200406_143636_9.jpg
1586177876235.png
IMG_20200406_143741_9.jpg
1586177936600.png
IMG_20200406_143513_0.jpg
IMG_20200406_143447_9.jpg
IMG_20200406_143401_4.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu naona umeamaua kujilipua ......wenzio huwa wanaficha majina humu..sasa kuataja kabisa kuwa Watumishi hao ni wapiga deal huogopi !??
 
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma na huyu Ndugu Mwakasitu ni MAJIPU.

Mkurugenzi hafanyi Kazi kabisa, yaana kama una suala pa Muhimu Bora kukimbilia kwa Mh. Mkuu wa Wilaya. Ila huyu Mkurugenzi ni too much ceremonial.

Mwakasitu anawasumbua sana Wazee fulani kule Msalato. TANESCO walichukua maeneo yao lakini RIPOTI YA TATHMINI hadi leo hajaipeleka TANESCO tangu Septemba 2018 hadi leo.

Mheshimiwa Raisi nashauri siku akienda Dodoma ajaribu kutembelea maeneo ambayo Miradi Mikubwa ya Serikali inawekwa ili KUSIKILIZA WANANCHI.

Watu wana vitu vingi vya kumwambia Mh Raisi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mhe. Rais wapiga dili Bado wapo Dodoma mji wa Mtumba tunakuomba uje usisikilize taarifa ya Mkurugenzi anazokupatia Ni za uongo njoo kwa wananchi na Kambi ya Jeshi Ihumwa utaujua ukweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii habari inaweza kuwa muhimu sana lakini imewasilishwa vibaya sana kwa kudhani documents pekee ndizo zenye umuhimu.Elezea vizuri background ya huo mgogoro kwa kituo kama vile unayemwandikia hajui kabisa na hajawahi kusikia hilo suala..Baada ya kuweka maelezo yanayojitosheleza ndipo sasa weka hizo attachment zako huku ukizilink na maelezo uliyotoa...

Hivyo inakuwa rahisi hata kupata msaada kwakuwa MTU anakuwa anajua unachoeleza
 
Mji wa Serikali umejengwa Mtumba, sehemu ya eneo ya mji huo ilikuwa Ni eneo la Jeshi na sehemu ya mji huo ilikuwa Ni eneo la wananchi wa Mtumba. Wataalamu wa uthamini kutoka JWTZ kambi ya Ihumwa walihusika katika zoezi la uthamini mwaka 20/6/2016 na walitushirikisha kwa kusema kuwa Serikali imeagiza litengwe eneo la Mji wa Serikali katika eneo la Jeshi. Kutokana na eneo lililokusudiwa kutolewa na Jeshi kuwa dogo iliwalazimu kuingia ktk eneo la wananchi na kumega eneo la wananchi.

Wakati wananfanya hivyo, JWTZ alizingatia Sheria zote na miongozo ya utwaaji was Ardhi na walishirikisha wananchi ipasavyo na wananchi tuliridhika kwa uwazi ulikuwepo na uliosimamiwa na JWTZ.

Wataalamu hao walifanya uthamini huo kwa sababu ilitarajiwa kuwa wait ndio wangelipa fidia ya eneo walilolionheza kutoka kwa wananchi ili eneo hilo liwe la umma na baadae walikabidhi Serikali kwa matumizi ya ujenzi wa mji wa Serikali zikiwemo Wizara, taasisi, barozi, Makazi ya barozi baadhi ya huduma za jamii na Nyumba za viongozi.

Mwaka 2017 Mhe. Waziri wa TAMISEMI kipindi hicho Mhe. Simbachawene alikuja kukabidhiwa eneo hilo Mtumba, makabidhiano hayo yalifanywa na JWTZ mbele ya Mkurugenzi was Jiji, Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa na baadhi ya viongozi wa Wizara ya Ardhi.

Katika makabidhiano hayo, JWTZ alikuwa wamechonga barabara kuzunguka eneo lote la Mji wa Serikali, walikuwa wamemaliza zoezi la uthamini. Jeshi hilo lilimkabidhi Mhe. Simbachawene eneo hilo na orodha ya wananchi wanaodai fidia mbele ya wananchi. Walisema sehemu ya eneo hilo limetokana na eneo la wananchi ambao hawajalipwa fidia, hivyo wanatakiwa kulipwa fidia. Kwa kuwa Jeshi sio walipaji wa fidia kwa sasa TAMISEMI wanapaswa kulipa fidia kwa mujibu was Sheria ili eneo liwe huru.

Mhe. Simbachawene aliwashukuru wananchi na kusema kuwa Serikali italipa fidia hiyo. Wananchi tuliambia tutunze fomu zetu na uthamini na taratibu za malipo zilianza kwa wananchi kufungua akaunti benki hakukuwa na shida Hadi hapo.

Tatizo lilianza baada ya kuanza kulipa fidia, waliliowa watu wachache na watu ambao hawana hata kipande cha mita moja na ambao zio wakazi wa eneo la Mtumba. Wananchi waliobaki wanaodai fidia waliambiwa wao hawana haki ya kulipwa fidia kwa kuwa maeneo wananyosema Ni yao yamo ndani ya eneo la Jeshi.

Baada ya wananchi kusikia majibu hayo walianza kudai malipo na walifika kwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma wakaambiwa wanahaki ya kulipwa isipokuwa wanasubili majina kutoka Jiji hiyo ilikuwa mwaka 2018 mda wowote tutalipwa. Tulipo kwenda Jiji tukaambiwa kuwa tulisahaulika kufanyika uthamini turudi eneo la Mji wa Serikali Kila my asimame ktka eneo lake tufanyiwe uthamini kwa kuwa check ya malipo hayo ipo.

Tukawauliza tumesahaurika vipi kwani uthamini was mwanzo tulikuwa na majina yetu tulihakiki baada ya jedwali la malipo kirudi kutoka kwa Mthamini mkuu wa Serikali (rejea viambatanisho vya uthamini tulivyoambatanisha). Ukisoma hizo fomu zinaonyesha kuwa jeshi walikuwa wanalitwaa wao kwa matumizi ya kupanua kambi Ni kwa sababu walitaka eneo lote watakalo likabidhi lionekane limetoka jeshini Ni la umma ndio maana Serikali ilitangaza kuwa mji huo utajengwa eneo la Jeshi. Hapo naomba muelewe msielewe vibaya.

Tukakubali kurudi kuthaminiwa upya majina yakaenda tukaambiwa tunahaki na tutalipwa, uthamini wa mara ya pili ulifanywa na wataalamu wa Jiji ambao ni Mwakasitu na Pius. Baada ya hapo tukaambiwa Mthamini ameshaidhinisha jedwali la malipo yetu.

Mwaka 2019 Mwishoni takribani mwezi wa 10 kulifanyika kikao cha wananchi wote kilichoitishwa na Mhe. Lukuvi (Waziri wa Ardhi) akasema kuwa, ametumwa na Mhe. Rais aje kuwaomba wananchi ambao Bado wanadai fidia wawe wavumilivu Serikali italipa malipo hayo lakini Mhe. Rais pia anaomba ujenzi uendelee kufikia mwezi wa 12, 2019 wadai wote watakuwa wamelipwa.

Mji ukaanza kujengwa na siku unazinduliwa Mhe. Rais alikuja kuzindua tulikuwa tumejiandaa kumwuliza Mhe. Magufuri juu ya ujumbe ulioletwa kwetu kutoka kwake. Wakati tunasogea hapo tulikamatwa na kufungiwa katika jengo lililokuwa stoo ya Wizara happy Mtumba nyuma ya eneo ulipofanyikia uzinduzi. Lakini tulisikia Mhe. Rais akitamka kuwa Kuna watu ameambiwa Bado wanadai fidia wawe wavumilivu tukafurahi sana na tukapata imani na taarifa ya Lukuvi.

Wananchi tukaelewa siku zikapita tukaenda kwa Waziri wa Ardhi kumwuliza vipi? mbona kimya akatuambia tuende kwa Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma atamaliza suala letu. Tukaenda tulipofika tukaambiwa sisi ni waongo eneo hilo Ni Mali ya Jeshi kwa barua baada ya kuzunguka hapo miezi 3. Siku barua inatoka ya majibu tulikuwa tumeoma kuondoka hapo na tulilala kwenye korido za Ofisi ya RAS. Kipindi chote hicho tunachokwenda kwa RAS tulikuwa tunamwomba afike eneo la tukio kujiridhisha kabla ya kutoa majibu.

Majibu tuliyopata kutoka kwa RAS yalitokana na majibu ya wathamini wa Jiji amabao wamekuwa wakituzungusha na kutukimbia pindi tunapokwenda Ofisi kwao (rejea barua ya RAS tulioambatanisha).

Baada ya kupewa barua hiyo tuliamua kuwaomba Jeshi kambi ya Ihumwa majirani zetu wema wasema enee Hilo halikuwa lao ila lingelipwa fidia lingekuwa Mali yao. Tulijibiwa kwa mdomo na wkasema hawawezi kuja hadi wapate barua kutoka taasisi yoyote ya Serikali itakayokuwa inashughulikia mgogoro huo ili wao wasimame kama mashahidi tu.

Baada ya maelezo ya Jeshi, tukaamua kwenda Wizarani tukaonana na Naibu wa Ardhi tukiwa na mabango yetu. Tukafanya kikao nae na tulikubaliana kuwa tusubili uchaguzi wa Serikali ya Mtaa upite ndipo tuende (rejea tangazo la Wizara kupitia gazeti la mwananchi). Tukasubili hatukuitwa tukaamua kujiongeza kwenda Wizarani tukaambiwa imeundwa tume ya kubaini ukweli wa jambo hilo. Tukakabidhiwa kwenye time hiyo tukakutana na tume hiyo.

Tulipofika eneo la mgogoro siku ya Kwanza wataalamu/ timu ya tume iliyokuwa inawataalamu wa Ardhi wa Ofisi ya RAS, Jiji na Mkuu wa Wilaya pamoja na wananchi tukatoka bila majibu na waliishia kubishana wenyewe kwa wenyewe. Wengine wakasema mbona mipaka ipo wazi wananchi Hawa wanahaki watu wa Jiji wakapinga kuwa hatuna haki. Swali likaja Kama hawakuwa na haki mbona uliwathaminishia kwa mara ya pili, jibu likakosekana tukasambaa.

Tukaamua kurudi Wizarani baada ya wiki 3 tukiamini tume imeandika taarifa na Naibu Waziri atakuwa na majibu sahihi. Tulipofika huko hakukuwa na taarifa Bali tuliambiwa sisi hatukuwa na haki kea sababu ni wavamizi wa eneo la Jeshi. Tukasema kuwa Kama ni wavamizi mbona Jeshi walituthaminisha Mali zetu jibu likakosekana. Naibu Waziri akasema ila kunauwezokano mkawa mnadai kutokana na maswali yenu. Tukamshauri tuunde timu nyingine ya watu wakiwemo na wanajeshi wa Ihumwa waliopima eneo la mji wa Serikali, Mhe. akakubali timu ikaundwa na kukutana eneo la tukio

Tulipofika eneo la tukio, mtu Jeshi safari hii alikuwepo akaonyesha mpaka wa Jeshi na sisi mpaka wetu. Mpaka wa eneo la Jeshi ulioonyeshwa upo sahihi na mipaka ya wananchi. Wataalamu wa Serikali wakiwemo walikuwa wanasema Ni eneo la Jeshi wakabutwaa na kuanza kuangalia a wao kwa was lakini Hadi sasa hatujapewa majibu. Jana tumerudi Tena Wizarani wakasema wanaandaa ramani tunajiuliza ramani za nn tena. Tumeshindwa kuelewa tatizo nini? .

Wataalamu wanaongea tu kwa kusikiliza watu na kuwashauri viongozi kwa kuwapotosha. Vitendea kazi wanavyo, kuwezeshwa wanawezeshwa kalini ni ujanja ujanja tu. Sasa Kama Ni lamani kwanini isingeandaliwa toka mwanzo?. Mbona wengine wamelipwa katika eneo hilo Hilo tena waliopo karibu na mpaka kabisa wa Jeshi tulionyumba yao kutoka mpaka wa Jeshi hatulipwi. Sisi tunaamini kuna ufisadi umefanyika happy sio bure. Katka eneo hilo Kuna ekari zaidi ya mia hazijalipwa fidia ambazo kwa bei ya 2000,000 ni zaidi ya 200,000,000. Lakini pia kunaenei jingine limekuwa likihamishwa mipaka na watu wa mipangomiji

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii habari inaweza kuwa muhimu sana lakini imewasilishwa vibaya sana kwa kudhani documents pekee ndizo zenye umuhimu.Elezea vizuri background ya huo mgogoro kwa kituo kama vile unayemwandikia hajui kabisa na hajawahi kusikia hilo suala..Baada ya kuweka maelezo yanayojitosheleza ndipo sasa weka hizo attachment zako huku ukizilink na maelezo uliyotoa...

Hivyo inakuwa rahisi hata kupata msaada kwakuwa MTU anakuwa anajua unachoeleza
Napenda kutoa vielelezo vya madai yetu ambayo tunaambiwa ni batili. Ardhi Jiji la Dodoma kuna watu wafuatao sio waadilifu. Mwakasitu, Piusi hawa ni wadhamini pamoja na Mafuru Mkuu wa Idara amabye yupo hapo kwa manufaa ya Mkurugenzi wa Jiji lanapiga fedha za dili balaa.

Hawa ni baadhi ya wanaodai tumeandika barua nyingi Mhe. Rais lakini tunahisi zinaficha hazikufikii, tumafanya jitihada za kukusimamisha kwa mabango lakini Mkurugenzi was Jiji anatuma watu ambao Ni po polisi wanatukamata na kutunyang'anya mabango.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Napenda kutoa vielelezo vya madai yetu ambayo tunaambiwa ni batili. Ardhi Jiji la Dodoma kuna watu wafuatao sio waadilifu. Mwakasitu, Piusi hawa ni wadhamini pamoja na Mafuru Mkuu wa Idara amabye yupo hapo kwa manufaa ya Mkurugenzi wa Jiji lanapiga fedha za dili balaa.

Hawa ni baadhi ya wanaodai tumeandika barua nyingi Mhe. Rais lakini tunahisi zinaficha hazikufikii, tumafanya jitihada za kukusimamisha kwa mabango lakini Mkurugenzi was Jiji anatuma watu ambao Ni po polisi wanatukamata na kutunyang'anya mabango.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wananchi wengi tunakosea sehemu ndogo sana..nimesoma maelezo yako kuna kitu kikubwa sana sijakielewa..issue yako ni madai ya fidia au issue yako ni hao watumishi uliowashutumu...na kupiga dili kwao kuna husiana vipi na madai yako..ni kwamba hizo pesa wanatakiwa kukulipa kutoka mifukoni mwao??,

Badala ya kujikita kwenye hoja ya msingi wewe unajikita kwenye majina ya watu...mfano kama sio waadilifu kama unavyodai kutokuwepo kwao kutafanya ulipwe hiyo fidia ata mtu mwingine akiwepo??? Sijui umeelewa point yangu..maana kama mliambiwa ni eneo la jeshi wao wanapaswa kuwalipa toka mifukoni kwao?

Ungefanya busara kama ungeomba mh raisi aingilie kati ili mlipwe fidia na kuweka wazi kwamba eneo mnalodai fidia ni eneo la jeshi ambalo mlivamia zamani ili atumie huruma yake sasa na sio matakwa ya kisheria...maana kama kuna wengine walilipwa kwa nini nyie 23 mliambiwa ni wavamizi wa eneo la jeshi??? .

Ninachoamini hao watumishi wamefuata matwaka ya kisheria na miongozo......cha kuomba hapa ni huruma kwa kukaa hayo maeneo muda labda na kuyafanyia uendelezaji kama mliendeleza.
 
Tuambatanishie na fomu za uthamini namba 1,na namba 3 ,maana hapo nimeona fomu namba 69 tu
 
Napenda kutoa vielelezo vya madai yetu ambayo tunaambiwa ni batili. Ardhi Jiji la Dodoma kuna watu wafuatao sio waadilifu. Mwakasitu, Piusi hawa ni wadhamini pamoja na Mafuru Mkuu wa Idara amabye yupo hapo kwa manufaa ya Mkurugenzi wa Jiji lanapiga fedha za dili balaa.

Hawa ni baadhi ya wanaodai tumeandika barua nyingi Mhe. Rais lakini tunahisi zinaficha hazikufikii, tumafanya jitihada za kukusimamisha kwa mabango lakini Mkurugenzi was Jiji anatuma watu ambao Ni po polisi wanatukamata na kutunyang'anya mabango.
View attachment 1410343View attachment 1410344View attachment 1410345View attachment 1410431View attachment 1410435
View attachment 1410348View attachment 1410441View attachment 1410447View attachment 1410351View attachment 1410352View attachment 1410451View attachment 1410354View attachment 1410456View attachment 1410356View attachment 1410357View attachment 1410358

Sent using Jamii Forums mobile app
Magufuli ni kipenzi cha Wagogo.

wacha waisome akili ziwarudie shubamit!!
 
Wananchi wengi tunakosea sehemu ndogo sana..nimesoma maelezo yako kuna kitu kikubwa sana sijakielewa..issue yako ni madai ya fidia au issue yako ni hao watumishi uliowashutumu...na kupiga dili kwao kuna husiana vipi na madai yako..ni kwamba hizo pesa wanatakiwa kukulipa kutoka mifukoni mwao??,

Badala ya kujikita kwenye hoja ya msingi wewe unajikita kwenye majina ya watu...mfano kama sio waadilifu kama unavyodai kutokuwepo kwao kutafanya ulipwe hiyo fidia ata mtu mwingine akiwepo??? Sijui umeelewa point yangu..maana kama mliambiwa ni eneo la jeshi wao wanapaswa kuwalipa toka mifukoni kwao?

Ungefanya busara kama ungeomba mh raisi aingilie kati ili mlipwe fidia na kuweka wazi kwamba eneo mnalodai fidia ni eneo la jeshi ambalo mlivamia zamani ili atumie huruma yake sasa na sio matakwa ya kisheria...maana kama kuna wengine walilipwa kwa nini nyie 23 mliambiwa ni wavamizi wa eneo la jeshi??? .

Ninachoamini hao watumishi wamefuata matwaka ya kisheria na miongozo......cha kuomba hapa ni huruma kwa kukaa hayo maeneo muda labda na kuyafanyia uendelezaji kama mliendeleza.
Ndugu watu hao ndio wamekuwa kikwazo Cha sisi kutolipwa ndio maana tunaomba Mhe. Magufuri atanye ziara Mtumba atauoata ukweli mtupu yeye anajua atambana nani na Nani tutapata majibu kama sisi tunasema uongo taasisi tulizozitaja zipo na sisi tupo mtumba. Huku kuna mengi zaidi atayapata

Wandugu hadi kufikia hatua hi kwa kweli hatuna jinsi kama kunasehemu hujatumia busara tunaomba msaada ndio maana tumeomba Mhe. Rais na Mhe. Waziri Mkuu waje tuonane nao kitajulikana kama sisi waongo ama la. Tumetumia busara toka mwaka 2016 Hadi leo tulikuwa tunafuatilia taratibu sasa uvumilivu umetushinda wakati mwingine kusema ukweli kunasaidia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu watu hao ndio wamekuwa kikwazo Cha sisi kutolipwa ndio maana tunaomba Mhe. Magufuri atanye ziara Mtumba atauoata ukweli mtupu yeye anajua atambana nani na Nani tutapata majibu kama sisi tunasema uongo taasisi tulizozitaja zipo na sisi tupo mtumba. Huku kuna mengi zaidi atayapata

Sent using Jamii Forums mobile app
Sisi Leo hatuna busara wao wanatuzungusha miaka you hiyo Kila ukienda majibu tofauti wao wabusara tusijaribu kuwabeba watu tumeongea nao kea upole Sana mufa mrefu. Tunaomba kesho tuongozane Wizara ya Ardhi saa tatu ukasikilize harafu utakuja kutoa maoni humu. Mhe. Rais tafadhali sana tunakuomba Mtumba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma na huyu Ndugu Mwakasitu ni MAJIPU.

Mkurugenzi hafanyi Kazi kabisa, yaana kama una suala pa Muhimu Bora kukimbilia kwa Mh. Mkuu wa Wilaya. Ila huyu Mkurugenzi ni too much ceremonial.

Mwakasitu anawasumbua sana Wazee fulani kule Msalato. TANESCO walichukua maeneo yao lakini RIPOTI YA TATHMINI hadi leo hajaipeleka TANESCO tangu Septemba 2018 hadi leo.

Mheshimiwa Raisi nashauri siku akienda Dodoma ajaribu kutembelea maeneo ambayo Miradi Mikubwa ya Serikali inawekwa ili KUSIKILIZA WANANCHI.

Watu wana vitu vingi vya kumwambia Mh Raisi.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mhe. Rais Magufuri tunapokwenda ufanye ziara katika kata ya Mtumba tunamaanisha. Madai yetu Ni ya fidia ya eneo lililoongezwa katika mji wa Serikali bila ya kulipwa fidia. Toka mwaka 2016 Hadi leo tunapigwa danadana tu. Ilifika wakati tukaambiwa hatustahili kulipwa kwa kuwa madai eneo tunalodai limo ndani ya eneo la Jeshi.

Tulipohoji kwanini tulithaminiwa ingali wanatambua tupo ndani ya eneo la Jeshi majibu yalikosekana. Ndipo tulipoambiwa kuwa tulisahaulika mara majina yetu hayakurudi kutoka kwa Mthamini mkuu wa Serikali hivyo malipo yetu tutalipwa (rejea kiambatanisho A barua kutoka Jiji ya tarehe 4/2/2019 iliyoandikwa na Mafuru). Hadi leo fidia haijalipwa.

Tarehe 15/8/2019 tulimwandikia Mkuu wa Mkoa barua ya malalamiko ya kutolipwa fidia. Mkuu wa Mkoa alimwandikia Mkurugenzi wa Jiji barua tarehe 12/9/2019 akimtaka atoe ufaganuzi was madai hayo (rejea kiambatanisho B barua kutoka kwa Katibu Tawala Mkoa kwenda kea Mkurugenzi Jiji).

Tulipokuwa tukifuatilia majibu yetu Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kutaka kuonana na Mkuu wa Mkoa ama RAS wataalamu wa Ardhi katika Ofisi hiyo kwa muda wa miezi 2 walikuwa wanatuzungusha na kutuambia Viongozi hao hawapo. Siku moja mtumishi mmoja katika Ofisi hiyo alituuliza mbona huwa mnakuja mara kwa Mara hapa mnamtafuta nani?. Tukamjibu Mkuu wa Mkoa ama RAS akatujibu mbona kila mkija huwa wapo ofisini kwao huwa mnapelekwa wapi? Tukamjibu wataalamu wa Ardhi huwa wanatupeleka katika Ofisi zao na kutuambia hawapo. Ndipo mtumishi yule akatuonyesha Ofisi ya RAS kukaingia na kumkuta.

Tulipoongea naye akashangaa na kusema barua yenu sijawahi kuiona, tukamwambia tuliikabidhi masjala ghafla akaingia afisa wa masjala na jalada lenye barua yetu. RAS akashangaa akaamuru wataalamu wa Ardhi waje kutupa majibu. Wataalamu hao wakasema wanaomba wamwandikie Mkurugenzi wa Jiji ili atoe majibu. Tukaambiwa turudi baada ya mwezi tukakubali.

Tuliporudi tena tukaambiwa Mkurugenzi hajajibu barua ikabidi tugome kuondoka ilikuwa saa 2 asubuhi Hadi saa 11 jioni ndipo RAS akawa mkali baada ya kuendelea kutuona pale Ofisi kwake tukiwa tumelala chini ya sakafu. Akaagiza tupewe majibu ndipo ikaandikwa barua inayoeleza kuwa Ofisi hiyo imepokea majibu kutoka kwa Mkurugenzi wa Jiji ikionyesha kuwa hatustahili kulipwa kwa kuwa maeneo tunayodai kuwa Ni Mali yetu yanamilikiwa na Jeshi. Barua hiyo imepingana na barua ya Bw. Mafuru ya tarehe 4/2/2019.

Baada ya kuopata barua hiyo tunajiuliza mbona tumethaminiwa mara 2 Mara ya kwanza tulithaminiwa a mali na JWTZ Mara ya pili na wataalamu wa Jiji. Kulikoni leo tunaambiwa maeneo hayo ni mali ya Jeshi. Ndipo tulipoambiwa kwenda Wizara ya Ardhi kupeleka malalamiko yetu. Jibu la kwanza tulilopewa tuliambiwa wao watamwandikia barua Mkurugenzi wa Jiji hivyo tusubili majibu.

Tulishangaa sana kwani malalamiko yetu tuliyapeleka Wizarani yakiwa na kiambatanisho ambacho Ni barua ya RAS akitoa majibu kwa kunukuu barua ya Mkurugenzi wa Jiji kuwa tumo ktk eneo la Jeshi. Tukamshauri Naibu Waziri kuwa hakuna haja kwani wao walishatoa majibu hawatakuwa na jipya Tena isitoshe wameshatoa barua mbili zinazokinzana. Tukamshauri aunde timu ya kutafuta ukweli wa madai yetu na majibu ya RAS kwa kuzingatia majibu aliyopata kutoka Jiji.

Mhe. Naibu Waziri alikubali na tulimwomba wananchi na Jeshi kila.mmoja akaonyesha mpaka wake wakati huo wataalamu wa Mkoani, Jiji na Wizarani wawe pembeni wakitazama mipaka hiyo.kisha kila mdai asimame eneo lake ili kubaini yumo ndani ama nje ya eneo la Jeshi. Mhe. Alikubali na aliagiza hivyo.

Kilichotokea Ni kinyume chake, kwanza walikuja wataalamu wa Mkoani, Wizarani na Jiji tu, anayeambiwa kuwa eneo lake ambaye Ni Jeshi hakuhusishwa zoezi likashindikana Mara ya kwanza, Mara ya pili alikuja mtu aliyejitambulisha kuwa Ni Askari Jeshi tukamtilia mashaka ikabidi kuongozane timu nzima hadi jeshini Ihumwa tulipofika wakasema hawana taarifa yake ila wakasema Jeshi wao hawana mgogoro wa mipaka na wananchi isipokuwa Mkurugenzi wa Jiji ndiye anayesingizia kuwa eneo Ni la Jeshi huku eneo la wananchi ndio maana wananchi walithaminiwa.

Jumatatu ya 6/4/2020 tulitika Tena Wizarani kudai majibu yetu kulikuwa na kikoa pale hivyo tukasubili. Mungu si Athumani kikao kikamalizika na kwa bahati nzuri alikuwepo afisa jeshi aliitwa na kupewa na kuambiwa kuna wananchi wanadai fidia lakini inasadikika eneo wanaodai ni mali ya Jeshi. Afisa wa Jeshi alianza kumwuliza Mthamini wa Ardhi alitumia kigezo gani kutambua kuwa watu hao wapo ndani ya eneo la Jeshi akasema Ni ramani ya eneo la Jeshi. Afande akasema haiwezekani, ndipo tukadakia kwa kumwonyesha fomu za uthamini alipoziona akatuuliza mara 3 kuwa wote mnaodai mnahizi fomu tukamjibu ndio, akamwambia Mthamini mkuu wananchi hawa wanahaki ya kulipwa na malipo yao yapo Ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji. Mtaminikuu akakosa jibu akabaki kimya afande akaondoka. Tukaahidiwa tukutane Leo tarehe 8/4/2020 ili twende kwenye eneo tukiwa na askali Jeshi kutoka Ihumwa.

Kituko Cha leo sasa tumefika pale tukaambiwa twende eneo la tukio. Sisi tulifika Wizarani saa 2 asubuhi wenzetu wamefika saa 8 mchana wakasema twendeni kwenye mpaka kila mtu akasimame kwenye eneo lake ili tujue anaeneo kiasi gani. Tukawauliza wanajeshi wapo wapi kwani Hadi sasa shida iliyopo Ni kujua sisi tupo ndani ya eneo la Jeshi ama nje. Kama tupo nje ndipo kila mtu atasimama kwenye eneo lake.

Tukajibiwa na Bw. Mtima akasema kuwa ameruhusiwa na Jeshi kuingia eneo la Jeshi, tukamwambia barua waliyokupa akasema wamemwambia leave mdomo tukasita. Tukamwambia tulikubaliana tutatue suala mpaka kwanza ili ijulikane madai yetu sahihi ama batili Kama ambavyo Mkurugenzi wa Jiji alivyojibu. Na ili tupate suruhisho Ni lazima Jeshi lishiriki wenzetu hawatakuwa Jeshi washiriki. Tukamwambia miaka yote mmeshindwa kulipa fidia mkisema eneo ni la jeshi tunaomba Jeshi waonyeshe mipaka tukiwa nao ili tujiridhishe namipaka yetu. Wenzetu hawataki isipokuwa Jeshi walisema wao wapo tayari mda wowote wapigiwe simu watakuja na askali Jeshi wa kuonyesha mipaka tulionyeshwa lakini Wataalamu wa Mkoa, Jiji na Wizara hawataki Jeshi kuja kuonyesha mipaka tukiwa pamoja.

Leo tumeamini Mhe. Rais kazi anayo kwa wataalamu Kama hawa wanaolazimisha kuendelea migogoro. Pia, tunawashangaa wataalamu wa Ardhi, Wizara kila siku inajinadi inashughulikia migogoro kwa kuitatua, Mtumba inashindikana vipi? Je? uwezo wa wataalamu tuliopewa Ni mdogo ama wanamaslahi na fidia ya eneo hilo?.

Ndio maana tunakuomba Mhe. Rais uje Mtumba tutakupa mengi zaidi ya haya . Aidha, tunakuomba kwa mamlaka uliyonayo umwagize Mkuu wa Kambi Ihumwa akupe taarifa sahihi juu ya suala hili. Ila tutafurahi sana ukija mapema sana tunamengi ya kukwambia juu ya fidia hii na maeneo mengine ikiwepo utendaji wa watumishi hawa.
IMG_20200408_215234_8.jpg
IMG_20200408_220145_3.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Attachments

  • IMG_20200408_214846_2.jpg
    IMG_20200408_214846_2.jpg
    61.7 KB · Views: 1
  • IMG_20200408_214846_2.jpg
    IMG_20200408_214846_2.jpg
    61.7 KB · Views: 1
Back
Top Bottom