Rais Magufuli: Nitaheshimu ukomo wa miaka 10 ya Urais kulingana na Katiba ya Tanzania

Mwanzilishi wa kampeni za Magufuli Baki anawatakia nanenane njema!
 
Nadhani upeo wetu wa kufikiria unaelekea kusiko..hili sio wazo la CCM ninauhakika ni mawazo ya wapambe wake huyo aliyetoa wazo. JPM ni muumini wa utawala wa Katiba na Sheria pia. Hawezi lizingatia hilo kabisa. Hatahivyo tumpime kwa hali za wananchi maendelea yanayoonekana na sio tu ukali wa kuongea au kukemea japo nao huo ni UTHUBUTU. Tutampima kwa ubunifu na utekelezaji..
 
Nilidhani unasema sasa ni wakati wa wananchi kutaka rasimu ya katiba ya warioba kumbe mwenzetu unawaza miaka mengine na kwamba ni muhimu kubadili katiba!
 
Ni mapema mno ingekua kamaliza miaka mitano akagombea tena na kushinda ndipo tungesema aongezewe kwani katiba hairuhusu zaidi ya miaka kumi. Tunaweka kiraka kwenye katiba kinachoruhusu kwani ni yetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mswada uende bungeni kupinga marufuku wabunge wa std 7 ni majanga! msikilize huyu na upuuzi wake, nenda msikilize na kibajaj yaani ni sheedah!
kama dereva anatakiwa awe form 4 kweli mbunge anaetunga sharia awe std 7?
 
Mswada uende bungeni kupinga marufuku wabunge wa std 7 ni majanga! msikilize huyu na upuuzi wake, nenda msikilize na kibajaj yaani ni sheedah!
kama dereva anatakiwa awe form 4 kweli mbunge anaetunga sharia awe std 7?
Vipi kuhusu Madj nao wapigwe marufuku? Maana hawa wanatekeleza kwa vitendo kabisa kuondoa vipengele vya ukomo wa madaraka katika katiba zao za vyama. Hawa wakiingia madarakani katiba ya nchi haitabaki salama.
 
HOJA ZA KUONGEZA MUDA WA URAIS ZIKEMEWE NA ZIPIGWE MARUFUKU KABISA!
Katiba ya nchi ni kama msahafu kwa nchi husika, ni nadra sana kufanya mizaha na misahafu mitakatifu.
Hivi karibuni wamezuka watu ambao kwa maono ni walevi wa mchana ambao kila kukicha wanazidi kuongezeka.
Leo huko korogwe bila aibu amezuka Mbunge na kudai kuwa Rais aliyeko madarakani aongezewe muda atawale miaka 20!
Siku za karibuni aliwahi pia kuibuka mmojawapo wa Rais mstaafu naye akatoa hoja kuwa Rais aongezewe muda .
Labda tukumbushane, hoja hizi dhaifu hazikuanza leo wala si ngeni, kule zanzibar zilizuka wakati wa Dr.Salmin au wao wanamwita komandoo, walevi wa mchana wakapaza sauti aongezewe muda.
Ni mwaka 1990 wakati Rais Mwinyi anazindua kipindi chake cha mwisho cha utawala aliibuka mshairi mmoja pale jangwani, akaghani shairi lililorushwa mubashara na RTD mchi nzima, huku akitoa rai kuwa hakuna haja ya msururu wa wastaafu kuwa Mwinyi apewe muda wa nyongeza.
Ni Julius Nyerere aliyekata mzizi wa fitina kwa kukemea kwa uwazi kuwa hakuna haja ya kubadilisha katiba kutengeneza masultani na wafalme.
Ikumbukwe kuwa kama Mwinyi angebadilisha katiba na kusalia madarakani basi tusingekuwa na waluomfuata yaani Mkapa, kikwete na sasa JPM
Ni wazi kuwa wanaovimbiwa kwa sasa na kutaka katiba ibadilishwe wasingekuwepo.
Kuna habari kuwa JPM amekemkea Mbunge aliyetaka katiba ili atawale miaka kumi, iwe ni fundisho kwa wale wote wanaojikomba ili kuidhaliisha katiba yetu, tuwajatae mchana kweupe!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Namuona akiistaafu 2025! Sinatatizo na hilo cha msingi Tanzania mpya iwe kipaumbele chake!
 
Back
Top Bottom