Rais Magufuli: Nitahamishia Serikali yangu Dodoma - Waziri Mkuu aanzisha safari..

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,179
2,940


Habari wakuu,
Leo tarehe 25 mwezi Julai ni siku ya Mashujaa hapa nchini Tanzania. Tunawakumbuka mashujaa wetu waliopoteza maisha wakiipigania nchi yetu.

- Rais Magufuli leo atakuwa mgeni rasmi katika shughuli ya leo, tuwe sote pamoja kujuzana kinachojiri.

======
PM Kassim Majaliwa: Natoa maagizo kwa Mawaziri wote, wahakikishe wanahamia mara moja.

Wageni wengi wameshawasili na mgeni rasmi pia amefika, kinachoendelea kwa sasa ni dua na sala kutoka madhehebu ya dini mbalimbali nchini.

Rais Magufuli anasalimia wageni mbalimbali na mashujaa waliofika kwenye shughuli ya leo.

Waziri Mhagama amemkaribisha Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kuwasalimia wananchi wa Dodoma na sasa anaezungumza ni Rais Magufuli.

CoNLURvWgAASYCL.jpg:large


------



 


Akihutubia ktk kumbukumbu ya Siku ya Mashujaa nchini, Rais Magufuli amesisitiza uamuzi wake wa kuhamishia shughuli zote za serikali kwenye Makao Makuu ya nchi, Dodoma ifikapo 2020.

Ni wazi kuwa Magufuli ameamua kufanya kile ambacho kimekuwa kikihubiriwa miaka yote na serikali ya Chama cha Mapinduzi kivitendo.

CoNLURvWgAASYCL.jpg:large

============

WAZIRI MKUU: Nahamia Dodoma mwezi wa tisa, mawaziri mnifuate

Waziri Mkuu wa JMT, Mhe Kassim Majaliwa, akiwa katika sherehe ya Kumbukumbu ya Siku ya Mashujaaa amesema atahamia Dodoma ifikapo mwezi wa 9 mwaka huu na kuwataka mawaziri wote wamfuate.

Aagiza ukarabati wa nyumba yake iliyopo Dodoma uanze mara moja.

Uamuzi huu wa Waziri Mkuu unaakisi makusudio ya Rais Magufuli kuhamishia shughuli zote za serikali katika Mji Mkuu wa nchi Dodoma kufikia 2020.
 
Back
Top Bottom