Rais Magufuli nisamehe,nakushauri kwa mara ya mwisho. Tafadhali shaurika!

Mkuu Barbarosa! Rais hajashushwa toka mbinguni ila kawekwa na wananchi. Hivyo Mzee Tupatupa ni Mwananchi na anayo haki ya kumpa ushauri Rais kwakuwa Mamlaka ya Rais inatokana na wananchi. Ni vema ukakaa kimya kwa hoja ambazo huzipendi, kuliko unavyojitoa ufahamu na kuonekana kituko. Ukada cyo kupinga hata hoja za Msingi, jifunze kwa Makada wanaojitambua ambao ni wengi tu humu jukwaani.
Kabisaaa

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
Wewe ni nani Nchi hii hadi utake ushahuri wako Raisi wa Nchi auchukuwe? Kamshauri Mbowe jinsi ya kuishi na Wema na Mamake, kama ukipenda!
Kuna siku utamuelewa mleta mada labda na nitakuja kukumbusha labda JF ipigwe ban tu
 
Wewe ni nani Nchi hii hadi utake ushahuri wako Raisi wa Nchi auchukuwe? Kamshauri Mbowe jinsi ya kuishi na Wema na Mamake, kama ukipenda!
Wewe hutaki Rais ashauliwe au ndiyo wale wapigwa katerero kama alivyosema JONGO PAPAI MKAA.
 
Wewe ni nani Nchi hii hadi utake ushahuri wako Raisi wa Nchi auchukuwe? Kamshauri Mbowe jinsi ya kuishi na Wema na Mamake, kama ukipenda!
Sijawahi kuku-quote, ila nimeamini ww hamnazo!

Kwani huyu sio mtanzania mpk rais asipokee ushauri wake?
Duh,una mambo ya ajabu!

Haya na huyo mbowe sijui hapa kaingiaje?

Hivi hamuwezi kujadili bila kuwataja wasiohusika?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Dongo la Kinana kwa malaika mkuu.




Kila ugonjwa una tiba au kinga au vyote. Rais wangu na Mwenyekiti wangu wa CCM Taifa,Dr. J. P. J. Magufuli,tafadhali niwie radhi nikushauri kwa mara ya mwisho. Shaurika.

Mimi sikuwahi kuwa Rais. Mwenzangu ndiwe Rais. Lakini,mimi nimekuwa mwanasiasa mwandamizi na hata mtumishi mwandamizi wa idara nyetinyeti Serikalini kuliko wewe. Najua jambo moja kubwa:mgawanyo wa majukumu na kuwa ukomo wa jukumu fulani

Kiserikali,kuna mambo ya Rais;ya Makamu wa Rais;ya Waziri Mkuu;ya Waziri na kadhalika na kadhalika. Kila kiongozi Serikalini ana majukumu na mipaka yake. Ndiyo kusema,si kila jambo lamhusu Rais. Si kila jambo halimhusu Rais. Si mambo yote yanayomhusu Rais kuyashughulikia.

Mhe. Rais,wewe kuandikwaandikwa kwenye media kila uchao si jambo jema sana. Kuandikwa kwako kwa kila litokealo Serikalini ni mchoro wa kutia kihoro. Mchoro huoneshao kuwa unafanya au kusemea kila jambo-hata yale ya Mawaziri,Makatibu Wakuu wa Wizara na kuendelea. Hoja ya jeshi la mtu mmoja huanzia hapo. Haivutii

Mhe. Rais,nakushauri uwaruhusu wasaidizi na wateule wako wafanye kazi zao ulizowaamini wazifanye. Wakizifanya zao,kazi zako zitapungua na kuonekana vyema. Yapo mambo ya kutendwa au kuzungumziwa na wasaidizi au wateule wako. Hata Wasemaji wa Wizara wangetosha na kutisha!

Ushauri wangu unalenga kukupunguzia kazi. Tafadhali epuka kuona kila jambo Serikalini ni lako. Ikifika hapo,yote utayatenda wewe. Wengine watatumbua mishahara ya bure. Tena,utaandikwa na kusemwa sana. Utafurahi na kukereka sana. Utaona na kusikia sana. Utafanya kazi sana. Utachoka sana. Utasema sana. Utatutisha sana!

Bastola ya nini tena jamani!?

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Umekua wa kwanza kumjibu Mzee Tupa Tupa. Nadhan umemzidi ujanja Lizabon, hongera yako.
Nikija kwny mada ya Mzee wa Lumumba Tupa Tupa, yeah you have narrated all!
Kwa hivyo kwa akili yako umeamini kabisa huyo tapel. ni wa lumumba??
ama kweli tz bila mabashite haiwezekani!
 
Wewe ni nani Nchi hii hadi utake ushahuri wako Raisi wa Nchi auchukuwe? Kamshauri Mbowe jinsi ya kuishi na Wema na Mamake, kama ukipenda!

Wewe ndiyo mpuuzi wa mwendo kasi, kwani Rais ni Mungu hadi asishauriwe, Nina uhakika kama Mh. Rais amesoma bandiko lako amekudharau kabisa.Na mambo ya Mbowe na Wema yameingiaje kwenye Uzi huu? Au kwa kujipendekeza unafikiri utateuliwa? Mh. Rais hatoi vyeo kijinga, wewe hutoshi hata ujumbe wa nyumba kumi.
 
Bavicha mnasimamia nini? Maana kila siku nyie hamuelezei Sera zenu Bali kusubiri rais amefanya au kusema nini mpate la kuongea

Tunasimamia uadilifu ndiyo maana hatutaki vihiyo kwenye ofisi za umma,mabashite kuleeeee koromije
 
Back
Top Bottom