Rais Magufuli: Ningejua kama Urais ndio hivi, nisingegombea

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
Wakati Muheshimiwa JPM akiwa mapumzikoni kule Chato aliwasiliana na Kardinal Pengo kwa njia ya simu, muheshimiwa JPM inaonekana alifunguka mambo mengi sana ambayo Pengo ameyaminya, ila kubwa alilomueleza ni kuwa kama angejua kazi ya Urais ilivyo ngumu hivi, wala asingethubutu kugombea.

Kardinali Pengo aliishia kumtuliza kwa kumwambia kuwa ni afadhali mtu mmoja afe lakini taifa lisiteketee.

Swali ni, kuna nini kinaendelea nyuma ya pazia huko Magogoni??
Nini maana ya maneno "ni afadhali mtu mmoja afe kuliko taifa kuteketea"??
================================================

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo amedokeza sehemu ya mazungumzo yake na Rais John Magufuli, yanayoonyesha mkuu huyo wa nchi anapitia katika kipindi kigumu hivi sasa.

Kadinali Pengo alidokeza hayo juzi wakati wa misa maalumu ya kumuombea aliyekuwa Waziri Mkuu, Hayati Edward Sokoine iliyofanyika kwenye kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kwenye misa hiyo, Kardinali Pengo alisema waliwasiliana na Dk Magufuli kwa simu wakati akiwa mapumzikoni Chato mkoani Geita na Rais alimueleza maneno ambayo yanaonyesha kuwa kazi ya urais si rahisi, na jinsi kiongozi huyo wa kiroho alivyompa moyo.

“Sijui ni vizuri nikisema Mheshimiwa Rais, lakini kwa vile uliyataja maneno hayohayo hata kule Chato. Napenda kusema yale uliyosema kwangu binafsi kwa njia ya simu,” alisema Kadinali Pengo.

“Ulisema ‘ningelijua kwamba kuwa Rais ndiyo hivi, wala nisingeligombea urais’ … na mimi nilisema afadhali mtu mmoja afe kuliko Taifa liteketee. Kwa hiyo endelea mbele.”

Kadinali Pengo, aliyeonekana awali kusita kuweka bayana mazungumzo hayo, alisema kwa kuwa Rais Magufuli alishaeleza hayo akiwa Chato, basi angependa aeleze sehemu ya mambo aliyowahi kuzungumza naye kwa simu.

Ingawa Kadinali Pengo hakueleza kile alichozungumza Rais akiwa Geita, Dk Magufuli amekuwa akieleza jinsi kazi ya urais ilivyo ngumu na kila mara kuomba wananchi wamuombee na kumsaidia kutekeleza majukumu yake.

Akiwa kwenye ibada iliyofanyika katika Kanisa la Bikira Maria, Parokia ya Chato, Rais aliwataka Watanzania wote kuendelea kuliombea Taifa ili liendelee kuwa na amani.

“Niwaombe Watanzania wote tuendelee kushirikiana na kushikamana kwa umoja wetu na siku zote tumtangulize Mungu mbele. Wakati tunaadhimisha wiki moja baada ya kufufuka kwa Bwana wetu Yesu Kristo,” alisema Rais Magufuli katika ibada hiyo.

“Yesu Kristo alikufa kwa sababu ya dhambi zetu. Sisi wote tujitahidi kufuata matendo ya Yesu Kristo ya kusameheana, kupendana, kushirikiana na tusibaguane.”

Hata hivyo, haijaeleweka mazungumzo hayo baina ya Rais na mtumishi huyo wa Mungu yalifikia hatua gani kiasi cha Kadinali Pengo kumtuliza kwa kumwambia “ni afadhali mtu mmoja afe kuliko Taifa zima liteketee”.

Akiwa Chato, Rais Magufuli pia alitangaza kwamba atapunguza mishahara ya watendaji wakuu wote wa Serikali wanaolipwa hadi Sh40 milioni, akisema chini ya utawala wake hakuna mtu atakayelipwa zaidi ya Sh15 milioni.

Rais Magufuli amejikita katika kupambana na ufisadi, ukwepaji kodi, matumizi mabaya ya fedha za umma, uzembe na wizi, huku akisimamisha kazi, kutengua uteuzi na kutimua watumishi wa umma wanaotuhumiwa au kujihusisha na wizi wa fedha za umma.

Zaidi ya watumishi 160 wa umma wameshasimamishwa au kutenguliwa uteuzi wao tangu Rais Magufuli aapishwe Novemba 5, 2015, huku akinasa wafanyabiashara wakubwa na wadogo waliokuwa wakipitisha bidhaa bandarini bila ya kulipa kodi na ushuru.

Kadinali Pengo alitoa dokezo hilo siku ya kukumbuka kifo cha Sokoine, ambaye amejijengea sifa ya kuwa mpambanaji katika vita dhidi ya uhujumu uchumi, uvivu, wizi wa fedha za umma na matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi.

Alieleza katika misa hiyo kuwa watu wanamfananisha Rais Magufuli na waziri mkuu huyo wa tatu tangu nchi ipate uhuru.

Alisema kuna ming’ono kuwa sura ya Rais Magufuli inafanana na ya Sokoine, akisema maneno mengi ya mtaani ni ya ukweli zaidi ya yale yanayoandikwa na vyombo vya habari.


Chanzo: Mwananchi
 
Kwa jinsi alivyokuwa akilaumu na kutoa majibu mepesi juu ya changamoto za nchi hii ni wazi ilionesha haufahamu urais vilivyo!!

Aliposema ikiwa watu watakosa maji basi waziri wa maji atageuka maji ni wazi hakujua ugumu wa kazi yake!!

Urais ni mzigo mzito tena wamisumari!!!
 
nadahni pamoja ya ugumu wake mr president ni Mr perfect...hakubali kuona kasoro ndogondogo na hizo zina uwezo wa kulmaza macho wazi 24/7..

cha msingi tumuombee Mungu....ila kama akitaka uraisi uwe kazi rahizi haraka haraka aandike katiba mpya
 
Ni kweli huyu mzee ana wakati mgumu sana na ni wa kuhurumia, kubalance ukweli na matakwa ya wananchi sio kazi ndogo, lakin kikubwa zaid ni kufanya kazi chin ya CCM halafu ukawa fair ni kitu kigumu sana. Kikwete mwenyew alitoka amezeeka pamoja na magumashi mengi. Kuwa na ulinzi wa kutosha, uhakika wa maisha ww na familia yako mpaka unakufa, na kuweka rekodi ya moja ya watu mashuhuri duniani ni mambo tunayoyapenda lakin nyuma yake kuna mzigo mkubwa sana wa deni la kulipa wananchi.
 
nadahni pamoja ya ugumu wake mr president ni Mr perfect...hakubali kuona kasoro ndogondogo na hizo zina uwezo wa kulmaza macho wazi 24/7..

cha msingi tumuombee Mungu....ila kama akitaka uraisi uwe kazi rahizi haraka haraka aandike katiba mpya
Yap hio ni sababu kuu, maana kile anachokiita madudu kinamsononesha sana aiseeee
 
Hapo bado Wananchi wanamsubiria tu atoe maamuzi kuhusu katiba yao waliyoipendekeza.

-Keshokutwa Bunge linaanza na issue ya ESCROW lazima iwekwe mezani.
 
Rais ana wakati mgumu sana. Binafsi nimeamua kumsaidia. Maana kuna ushenzi mwingi sana ulishajengwa humu nchini na kuwekewa himaya.
Ila sharti langu ni moja tu...na yeye apambane, habari za kuchwza mchezo wa 'kula tumbakishie baba' siutaki..yaani unapoteza muda kukizunguka kijiti badala ya kukidondosha.
 
Back
Top Bottom