Rais Magufuli: Nimeamua maisha yangu nitaishi Karagwe na siyo Chato

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,099
Akihutubia maelfu ya wananchi wa Misenyi, Rais Magufuli amesema yeye maisha yake ataishi Karagwe na ndivyo alivyopendekeza na sio Chato

Akiwa na tabasamu na furaha kubwa kuhusu Karagwe sina shaka kwa maoni yangu mimi Gussie wa JF mazingira ya Karagwe hasa hali ya hewa ni safi na inavutia ukilinganisha na wakazi wa Dar es Salaam wanaovuta hewa ya ukaa mchanganyiko wa Petroli, majitaka na uozo wa uchafu wa samaki kila kona.

Kwa mujibu wa ile Sheria ya kuwajengea makazi viongozi wetu ni dhahiri Rais Magufuli atajengewa nyumba sehemu anayoipenda yaani Karagwe.

Amesisitiza kauli yake kuwa yeye kama mkazi wa Karagwe amefurahi kuishi na wafugaji hivyo mbunge wa hapo atatue kero za maji na umeme ili yeye atapokuwa Raia ataungana na Raia wa hapo kufanya shughuli za maendeleo kupitia mbunge atayekuwepo yeye atapokuwa Raia wa kawaida.

Hii kauli imekuwa mwiba kwa watu ambao sio wazalendo wanaoshinda kutwa nzima kutunga uongo kumuhusu Mheshimiwa Rais wetu Dkt John Pombe Magufuli wakimuhusisha na mambo ya Chato wakati yeye ataishi Karagwe.
 
Mkuu ukiwa unaripoti maneno ya wanasiasa ni bora sana kutunza akiba ya maneno!

Ushauri tu nakupa. Ni hiari yako kuupokea au kuuacha, hakuna dhambi yoyote.
Samahani hakuna akaunti Benki yoyote Tanzania ya kutunza akiba ya maneno

Kama unayo au una taarifa niambie nitapata riba kiasi gani kwa mwaka ili nifungue akaunti ya kutunza akiba ya maneno

Mimi najua akiba ni Fweza, Pesa yaani money na vitu vyote ambavyo unaweza kuvigeuza pesa haraka kama dhahabu, Almasi

Sasa akiba ya maneno kama unayajaza moyoni yatakuletea presha kiongozi
 
Back
Top Bottom