Rais Magufuli: Niliwahi kuwa dereva wa teksi bubu

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Rais Magufuli ametoa siri hiyo leo wakati akizindua daraja la la Ubungo lililopewa jina la Kijazi Interchange.

Rais Magufuli amedai kuwa alipokuwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam alikuwa akipiga kibarua cha kuendesha teksi bubu ili ajipatie chochote kitu. Na kituo alichokuwa anapaki ni jirani na lilipojengwa daraja hilo la juu mahsusi kupunguza foleni.

Rais Magufuli amesema kazi ya urais ni ngumu sana maana pamoja na kuwa na hamu ya kuendesha gari lakini huwa anakatazwa na kuzuiliwa.

Mbali ya hayo rais wa JMT amesema kuwa maendeleo huwa wakati mwingine yanakuja na vikwazo sababu wakazi wa maeneo ya Ubungo mpaka Mbezi mwisho walichukia kubomolewa nyumba zao pamoja na kuwa zilikuwa ndani ya hifadhi ya barabara.

Rais Magufuli amesema sheria ni Msumeno ndio maana hata jengo la Serikali ambalo ni mali ya Tanesco lilivunjwa japokuwa aliyekuwa waziri mkuu kipindi cha awamu ya nne ndugu Mizengo Pinda hakuamini kama litakuja kuvunjwa.

My take: Wakazi wa Dar es Salaam waambieni watoto wenu wasichague kazi. Kutwa wanashinda vijiweni wanajadili habari za Simba na Yanga,Diamond na Zari huku wakibweteka. Miaka ya nyuma mtu unapiga deiwaka ya udereva teksi huku unasoma.
 
Hawana uwezo wa kuishi nje ya ajira hawa watakufa mapema.
Kupewa na kujitafutia ni vitu viwili tofauti
Kama alivyokimbia kujitafutia mr Lema na kuona aende kupewa vi pesa vya ukimbizi, maana wizi wa magari kwa sasa ni mgumu sana 😁😁😁😁
 
Back
Top Bottom