Rais Magufuli, nilisikia ukiahidi kuimarisha demokrasia. Tunaomba utuachie Katiba Mpya

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,389
2,000
Mheshimiwa Rais nilipokuwa kidato cha pili katika somo la fizikia nilifundishwa kwamba mwendo wa gari anayeuona vizuri vizuri ni yule aliyeko pembeni na sio yule aliyeko ndani ya gari linalotembea kwani huyu anaweza kuona miti ndiyo inatembea kumbe gari alilolikalia ndilo linatembea na miti imesimama.

Mheshimiwa Rais nimekuwa nikifuatili siasa za nchi yetu na ki msingi mimi kama mtazamaji wa pembeni nadiriki kusema zina matatizo makubwa. Lakini kinachonisikitisha mweshimiwa raisi ni kuona wale waliojaribu kutatua matatizo haya walikuwa ndani ya gari lenyewe linalotembea na hawakuona vizuri. Matokeo ya hawa ni kutoa mapendekezo ya kushangaza na kuacha kiini cha matatizo.

Eti wanapendekeza wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya ama wachaguliwe na wananchi au waondolewe? Kwa uelewa wangu mdogo wa mambo ya siasa mimi naamini macho, masikio, mdomo na miguu ya mweshimiwa raisi katika mkoa au wilaya ni hawa wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa. Unapopendekeza kuwatoa kwa raisi maana yake ni sawa na kupendekeza kukata masikio, mikono, macho na miguu ya mweshimiwa Rais katika maeneo haya yaliyo karibu na wananchi na raisi viungo vyake hivi vibaki ikulu tu, hivi kwa mapendekezo haya tulikuwa tunatafuta kuboresha au kumdhoofisha Rais.

Kilichokuwa kikitafuta katika mapendekezo haya mimi naona kipo tayari labda tungetafuta tukiboresheje? Kipo kwa maana Halmashauri zinaendeshwa na Mameya au wenyeviti ambao hawa huchaguliwa na wananchi wenyewe kupitia mfumo wa uwakilishi kama wa marekani. Kwamba wananchi wanamchagua diwani na huyu ndiye anayekwenda kuchagua meya.

Sasa tatizo liko wapi?

Mfumo wetu wa wabunge ndilo tatizo kubwa la nchi hii. Unapokusanya watu wasiofanya kazi unawaleta sehemu wanaongea na kisha unawalipa wanarudi kwao hawa wataanza kufanya mambo ya ajabu na hawa daima wataishi kwa kugombana. Lakini ukiwaweka watu pamoja kila mmoja unamuonyesha wewe chimba mtaro mpaka pale ukimaliza ujira wako huu, wewe kunja hizi nondo ukimaliza ujira wako huu, ni nadra sana kukuta hawa wanaambiana maneno ya ajabu au kugombana. kila mtu yuko bize na kazi yake.

Mweshimiwa Rais kazi ya wabunge ni kusimamia na kushauri serikali lakini mfumo tunaoutumia kwa hawa ni ule wa "debate" za sekondari. Kwamba kila mwanafunzi alikuwa kwao huko akifanya mambo yake wakikutana kwenye debate basi ukiwa upande wa kupinga basi utatafuta namna upinge hoja na ukiwa upande wa kusapoti basi jukumu lako na kutunga maneno kusapoti hoja.

Hili ni tatizo kubwa na ambalo linaharibu mantiki ya siasa, linaharibu majukumu ya bunge.

Mabadiriko ya Katiba Yenye Tija ni kuleta mfumo wa wabunge wakaazi.

Mbunge awe ni bungeni na akitoka bungeni anaenda jimboni kwake na mwananchi yeyote mwenye shida iliyoshindikana kutatulika ofisi za watumishi wa umma anaenda kumuona mbunge ofisini kwake.

Mbunge anachukua shida za watu na kwenda kuzitafutia majibu kwa viongozi kwenye jimbo au halmashauri yake. Umeenda hospitali haukupewa dawa unaenda kuuliza kwa mbunge kama huo ndiyo utaratibu.

Lakini wabunge wetu wakitoka bungeni wanaenda kununua mahindi na kuuza, kwenye majimbo yao dawa zinatoka MSD zinauzwa juu kwa juu hazifiki kwenye hospitali, hazifiki zahanati na wao wako kwenye maduka ya nguo na viatu kariakoo. Muda wa bunge ukifika ni kwenda bungeni kuhoji unanunuaje ndege wakati watu wana njaa.

Watumishi wa umma kama walimu, madaktari hawahudhurii makazini lakini mbunge yuko kwenye biashara zake na akienda bungeni ni kutengeneza general statement zisizo na ushuhuda. Unawezaje kusimamia serikali kwa staili hii.

Mbunge ni lazima akusanye takwimu za kila kitu kutoka katika jimbo lake na huo ndiyo usimamizi. Kuna vituo vya afya vina madaktari wanalipwa mishahara lakini mgonjwa akifika ndiyo mganga anatafutwa.

kuna mahospitali watu wa bima wanateseka kweli, wanakaa daktari hayupo mbunge yuko kwenye biashara zake na wakitoka huko wakienda kujadili ama ni kutengeneza fitina ili wengine wachukiwe au kuchangia ili kujipendekeza.

Mweshimiwa raisi utaitendea vyema nchi hii kama utaondoa mfumo mbovu wa ufanyaji kazi wa wabunge. mbunge akienda bungeni ni lazima awasilishe takwimu za utendaji kazi katika jimbo lake na mjadala wake ni lazima uwe na ushahidi wa katika takwimu zake.
 

Mac Alpho

JF-Expert Member
Aug 5, 2019
1,758
2,000
Nimekuelewa zaidi kwenye hiyo aya ya mwisho, juu ya uwasilishwaji wa taarifa za utekelezaji wa majukumu ya mbunge, katika Jimbo lake👏👏
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
37,353
2,000
Nimecheka, eti awaachie katiba mpya, yaani yeye aikatae kisha wakati anatoka awaachie wenzake? Ccm inajua katiba mpya ni kwa ajili ya kuwatoa madarakani yeye akiwa ni mmoja wa wenye imani hiyo. Katika Mazingira hayo unategemea yeye akubaki haya matamanio yako ya katiba mpya?

Hapo alipo anajiuliza atapata wapi 10t+ ndani ya hii miaka mitano, ya kumalizia miradi miwili ya SGR &SG. Katika vitu ambavyo haviko kwenye akili yake ni demokrasia hasa mambo ya katiba.

Anachojua ni ujenzi wa miundombinu tu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom