Rais Magufuli: Nilipata shida sana kumteua Waziri mkuu ila kwa kumuomba Mungu akanionyesha Mchapakazi Kassim Majaliwa

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,780
141,667
Rais Magufuli amewaambia wananchi wa Ruangwa kuwa baada ya kuchaguliwa kuwa Rais wa JMT alipata mtihani mgumu wa namna ya kumpata msaidizi atakayeendana naye.

Ndipo baada ya kumuomba Mungu akanionyesha kijana wenu mchapa kazi, shujaa asiyeogopa chochote mh Kassimu Majaliwa, amesema Rais Magufuli.

Basi niwaombe wananchi wa Ruangwa mumpe ushirikiano waziri mkuu ili kwa pamoja tuijenge nchi yetu, amemalizia Rais.

Chanzo: TBC!
 
Yani yeye kila kitu utasikia nilipata shida oooh nilisukumizwa oooh niliwaza weee ikafika hadi arufajiri oooooh sijui kwa zaidi ya miaka selasini.....Hajawahi kuongea kwa kurahisisha!
 
Kusema ukweli Majaliwa ni jembe, na presidential material ya uhakika kabisa.
 
Kwani Mbowe alimpataje Dr Mashinji?!
Alimuomba mkuu wa malaika yule ambaye tunaambiwa Mungu anatakiwa amshukuru na ilivyofika saa 11 arufajiri akafunguliwa Mashinji. Bwashee siku hizi hatuombi mbali. Mungu wetu tunaye huku huku Tz. Leo amesamehe dhambi zote za Nape!
 
Kwani wewe ulidhani mbinguni ni wapi?........mawinguni?!!!
 
Alimuomba mkuu wa malaika yule ambaye tunaambiwa Mungu anatakiwa amshukuru na ilivyofika saa 11 arufajiri akafunguliwa Mashinji. Bwashee siku hizi hatuombi mbali. Mungu wetu tunaye huku huku Tz. Leo amesamehe dhambi zote za Nape!

Kwani kusaheme ni kosa, au ulijua binadamu mwenzako huwezi msamehe dhambi zake? Au ulijua dhambi ni Mungu tu anasamehe? Nape mwenyewe kakiri kaenda kuomba msamaha kwa makosa yake, sasa ww unatengeneza maneno yako kusema kwamba binadamu hawezi msamehe mwenzie hadi Mungu tu?
 
Baada ya Uchaguzi mkuu wa 2015, Majaliwa, Nape na Saidi Mtanda ambaye alishindwa Ubunge waliongoza moja kwa moja mpaka kwa Mzee Mkapa ili mmoja wao wakumbwuke kwenye uwaziri

Baadae Mkapa katika kuchekecha hapa na pale akaona wabunge wengi wa Kusini ni vilaza akiwemo yule wa Masasi Dkt. Chuachua, hivyo aliwasiliana na Magufuli na kumwambia Kassim Majaliwa atakufaa kwenye cheo cha Waziri Mkuu na wakati huo huo Makamba jnr pia alikuwa aaatamani U-W/M na baadae ndipo alipoteuliwa ndg Majaliwa kwa kufuata pendekezo la Mkapa na sio MUNGU kaaa tunavyoaminishwa.

Mwaka wakati wa sekeseke la kutaka kumuoandoa kwenye nafasi Majaliwa, Mkapa aliwasiliana na JPM na kumuambia aendelee kumuacha.
 
Kwani kusaheme ni kosa, au ulijua binadamu mwenzako huwezi msamehe dhambi zake? Au ulijua dhambi ni Mungu tu anasamehe? Nape mwenyewe kakiri kaenda kuomba msamaha kwa makosa yake, sasa ww unatengeneza maneno yako kusema kwamba binadamu hawezi msamehe mwenzie hadi Mungu tu?

Nape hakuwa na makosa bali hana uwezo wa kupambanua nje ya siasa za mbeleko. Tazama mtu mwenye uwezo kama Mwele Malecela mwenye uwezo nje ya mbeleko anavyojiamini.
 
Back
Top Bottom