Rais Magufuli: Nikihamia Dodoma nitauza nyumba zote za Serikali Dar es Salaam

Miezi minane kila akipewa jukwaa ni kauli tata tuu jee miaka mitano? Mugabe anapoteleza tunasema ni uzee na huyu "mpendwa" wetu jee?
Nahisi ndio maana JK juzi kasema asiombwe ushauri wa chama au serikali tena! Hataki kuja kuhusishwa na maajabu
JK yupo very cautious, anajua kinachokuja kutokea mbeleni, alisema mtanikumbuka, miezi nane tu, kila kitu utata mtupu
 
Mimi ningemshauri Rais kama kweli anao huo mpango wa kuuza baadhi ya nyumba za serikali basi aangalie zile zinazoweza kugeuzwa matumizi na kufaa kuwa ni taasisi za elimu yaani vyuo iwe ni kwa ngazi za cheti, diploma au hata degree basi ajaribu kukaa na kushauriana na wanaohusika na masuala ya elimu wazipitie wakaguwe kuona kama itafaa kutumika kwa kazi hii kulingana na mahitaji ya wataalam wanaohitajika kulingana na vipaumbele vya Taifa letu kielimu. Hili la kuuza mimi naona kama halijakaa vema na kwa kupangisha kwa kushirikiana na NHC inaweza kuleta tija japo nimekuwa nikishangaa nyumba nyingi za NHC zenye ghorofa hasa zilizoko katikati ya miji hasa DSM ghorofa hizi zimezaa gjorofa tena juu yake kwa kuongezewa vibanda vya mabati na watu kuishi na sijui kama nao wanajuwa kuwa watu wanaishi ktk hivyo vijumba vilivyojengwa juu ya hizo ghorofa na je zinalipiwa kodi? Japo zinchafua mandhri na uzuri wa mji. Pia tawala zinabadilika anawez kuja kiongozi mwingine akaona baadhi ya idara za serikali zirudi DSM je tutajenga mpya tena? La kama nimekurupuka basi tusameheane maana kipindi kigumu sana hiki.
 
Jamani eeeh! Kwa hili kama kweli kasema hivyo, namuunga mkono tena huyu jamaa. Msije mkasema; Wewe Punainen siku zote unampinga tuuuu baba Jeesca! Nilimuunga mkono kwa lile la kuhamia kule kwa wala viwavi, na jana tu kwenye uzi mmoja hapa nilisema ikibidi majengo yaliyokuwa makao makuu ya wizara na idara mbalimbali za serikali hapa Dar yabadilishwe umiliki (siyo kiufisadi lakini!) Ili huko mbeleni asije akatokea mhuni mwingine kwa kuimiss tu Dar, akaamua kuirejesha serikali hapa Dar tena. Ila nasisitiza kuwa kwa sababu hawa jamaa walishazoea kuharibu maeneo mbalimbali ya kihistoria katika nchi yetu, lile jengo jeupe pale karibu na soko la samaki libomolewe, halafu ile sehemu iwe beach ambayo itakuwa wazi bila mizengwe kwa wakaazi na wageni wooote ambao kwa sababu moja au nyingine watajikuta hapa Dar.
 
JK yupo very cautious, anajua kinachokuja kutokea mbeleni, alisema mtanikumbuka, miezi nane tu, kila kitu utata mtupu
Yani wewe ndo hata nashindwa nikujibu vipi. Yaani unasahau matatizo yote Tanzania tuliyokuwa nayo kama nchi wakati wa JK? Ikiwemo dola kufika mpaka 2500?

Kweli binadamu tuna sahau haraka duu...
 
Back
Top Bottom