Rais Magufuli: Nia aibu kwa Taifa lenye watu milioni 55 kuwa na walipa kodi milioni 2.2 pekee. Kenya ina watu milioni 46 na walipa kodi milioni 3.9

Nini kilipelekea ongezeko kuwa rekodi kubwa la usajili wa walipa kodi wa kawaida na wale wa VAT wakati wa utawala wa awamu ya Jakaya Kikwete halafu ktk miaka mitatu ya utawala wa awamu ya tano lawama kedekede kuwa ni watu wachache wanalipa kodi pia awamu ya 5 kushindwa kuongeza usajili mpya wa walipa kodi. Tusome kipengele hiki cha ripoti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania (NBS Tanzania) hapa chini :

3.3 Taxpayers and VAT Vendors Registration

The number of registered taxpayers increased by 10.5 percent from 2.0 million in 2014/15 to 2.2 million in 2015/16. The largest growth of registered taxpayers was 55.6 percent in 2012/13 which surpassed the average growth of 23.2 percent in the period of 2006/07 to 2015/16. Table 3.5 shows
the trend of taxpayers registration from 2006/07 to 2015/16.
Source : National Bureau of Statistics | Statistics for Development - takwimu - tax

Utawala wa Jakaya Kikwete uliweza kuongeza usajili wa walipa kodi kwa asilimia 55.6 kipindi cha mwaka 2012 / 2013 lakini juhudi zote za awamu ya tano hali ya kusajili walipa kodi wenye uwezo zimekuwa kiwango cha chini kabisa kufuatana na ripoti za ofisi za takwimu ya Taifa.

Aina za kodi ambazo serikali inaweza kuziangalia ili kuongeza wigo wa mapato kupitia sera sahihi za kiuchumi na vivutio kwa walipa kodi :

Indirect Taxes
These are taxes based on consumption. Categorically they are divided into consumption taxes, other
domestic taxes and international trade taxes. Examples of such taxes are Import Duty, Excise Duty
and Value Added Tax (VAT). By definition, the legal incidence of the tax falls on the trader who
act as a collecting agent of the Government while the effective incidence falls on the final consumer
of goods or service who eventually pays the tax.
Value-Added Tax (VAT)
It is a consumption tax charged on all taxable goods and services at a standard rate of 18 percent. It
is a multi-stage tax levied on the difference between a commodity’s price before taxes and its
production cost at each stage of production and distribution up to the retail stage. It is also levied
on taxable imports made by a person whether or not registered for VAT.
Excise Duty (Local)
It is levied on certain locally manufactured goods and services such as soft drinks, beer, wines,
spirit, mobile phone services, plastic shopping bags, satellite television services, cigarettes and
petroleum products.
Value Added Tax on Imports
It is levied on all goods and services imported into the country unless such goods and services are
specifically exempted under the VAT law. All importers must pay VAT regardless of whether or
not they are registered for VAT. However, importers who are registered for VAT can claim the
VAT paid on the imported goods as an input tax in their business. However, for VAT on imported
services the input tax is treated as reverse charge hence added to the value of the service.
Other Taxes
Skills and Development Levy (SDL)
This tax is based on the total gross emoluments paid by an employer to employees (currently, at a
rate of 6 percent). The gross emoluments include salary, wage, leave pay, payment in lieu of leave,
subsistence allowance, etc.
Stamp Duty
Refers to the duty paid on certain legal instruments/transactions, affidavit, conveyance and lease
agreements. The duty rate is 1 percent based on the consideration applicable to non business
persons when issuing a receipt whenever they sell their privately owned assets/properties. Stamp
duty on conveyance of agricultural land is TZS 500.
Airport Service Charge
Refers to charges levied on passengers who board an aircraft at any airport in Tanzania.
Port Service Charge
Refers to charges levied on passengers who board passenger shipping vessels at any port in Tanzania.
Source : National Bureau of Statistics | Statistics for Development
TAX STATISTICS REPORT 2015/16
TANZANIA MAINLAND
Gud observation mzee but still ukisema Utawala wa Kikwete uliongeza idadi ya walipa kodi, hiyo haitoshi hata kidogo kusema ilifanya vizuri kwenye ulipaji wa kodi. Kipimo muhimu cha mafanikio ni uwiano wa ulipaji kodi dhidi ya pato la Taifa.

Sasa kama sisi tunachezea chini ya asilimia 12% ya pato la Taifa licha ya Rais Magufuli kufanikiwa kupandisha mapato kutoka bilioni 800 kwa mwezi hadi trilioni 1.3, utasemaje Kikwete alifanikiwa?
Kwa tafsiri ya bilioni 800 dhidi ya bilioni 1,300 ni dhahiri kipindi cha Kikwete, Tanzania ilikuwa more worse - chini ya asilimia 9%, right?
 
View attachment 963387

Rais Dk. John Pombe Magufuli, akiwa katika Kikao Maalum kati yake na Uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ameeleza kuwa, Tanzania haifanyi vizuri katika suala la ukusanyaji wa mapato kulinganisha na Nchi nyingine za kiafrika.
Alieleza kwa kufafanua takwimu za kodi kwa kulinganisha Tanzania dhidi ya majirani zake:
  • Tanzania (milioni 55): walipa kodi milioni 2.2; kodi inayotozwa ni 12% ya GDP.
  • Kenya (milioni 46): walipa kodi milioni 3.9; kodi inayotozwa ni 18% ya GDP.
  • Uganda (milioni 37): walipa kodi milioni 1.2; kodi inayotozwa ni 14% ya GDP.
  • South Africa (milioni 56): walipa kodi milioni 19.9; kodi ni 26% ya GDP.
  • Mozambique (milioni 5.3): walipa kodi milioni 18%; kodi ni 18% ya GDP.
  • Zambia (milioni 16): walipa kodi milioni ?; kodi ni 15% ya GDP.
  • Botswana (milioni 2): walipa kodi milioni 0.7; kodi 14% ya GDP.
  • Burundi (milioni 10): walipa kodi milioni 0.2; kodi 13% ya GDP.
  • Namibia (milioni 2): walipa kodi milioni 0.6; kodi 12% ya GDP.

Hapa Rais Magufuli amepigilia msumari kwenye ukweli. Watanzania wamekuwa wakilalamika kuwa, kodi ni nyingi na kwamba Sera za sasa siyo rafiki kwa mazingira ya kibiashara na uwekezaji nchini. Sasa ukweli umewekwa wazi kuwa, Tanzania ndiyo Nchi yenye wastani mdogo sana wa walipa kodi katika Nchi zote za Afrika Mashariki.
Vilevile, mapato yatokanayo na kodi nchini Tanzania, ni asilimia ndogo sana kulinganisha na Nchi majirani. Tanzania imepigwa na Kenya, Uganda, Zambia, Msumbiji, Rwanda, Burundi, SA, Botswana na Namibia katika asilimia ya Mapato yatokanayo na kodi (kiwango cha kodi kulinganisha na uwiano wa pato la Taifa).

Sasa wewe fikiria, kama Serikali ya sasa imejitahidi kuziba mianya ya kodi na kuongeza walipa kodi lakini bado Tanzania iko nyuma kulinganisha na majirani zake, je kipindi cha kabla ya Magufuli, hali nchini ilikuwaje?

Tatizo liko kwa Watanzania wenyewe. Sera za ovyo za kuwarahisishia maisha watu wavivu ndizo zilizotufikisha hapa. Tuliifanya Tanzania masikini kuwa Nchi inayotegemea consumer goods na kujisahaulisha misingi ya kiuchumi. Leo bado tuko nyuma kwenye kodi but tunalialia, sasa hali ikifika ya kuifanya kodi kuchangia asilimia 15% itakuwaje.

Tuaje uvivu, majirani walikuwa wanatuchora sana kipindi cha nyuma namna tulivyokuwa tunapotea. Sasa hivi tunaifanya Tanzania kuwa Nchi ya kuzalisha bidhaa zetu na siyo kupokea kila kitu kutoka nje.

Rais Magufuli amewakumbusha Watanzania kuwa: Hapa duniani, mambo ya uhakika ni mawili pekee: kifo na kukusanya kodi.

Yaliyojiri kikao cha Rais Magufuli na Mawaziri, Makatibu Wakuu, MaRCs, MaRAS na TRA - JamiiForums
Inakadiriwa kuwa wafanyakazi walioandikishwa katika mifuko ya hifadhi ya Jamii ni watu milioni 2.1. Hawa ndiyo wanaofanya kazi rasmi za kuajiriwa aidha katika sekta binafsi au ya umma. Assume 30% ya idadi ya watu ni vijana na wazee wasioweza kujitegemea na 40% ni wakulima wanaongoja mazao ya mwaka unabakiza 30% ya wafanyakazi na wafanyabiashara ambao wanapashwa kuchangia kodi kila mwezi. Hawa watakuwa ni watu milioni 16.5 ambapo sasa watu milioni 14.3 wanawatwisha mzigo watu milioni 2.2 kwa jalili ya kubeba watu milioni 55!. Kwa picha hii ndiyo maana kodi ni kubwa mno. Hizi ni takwimu za kubuni karibu na ukweli lakini pengine hali ni mbaya zaidi. Wahusika wakifanikiwa kurekebisha hii na kupunguza kodi kwa wafanyakazi( PAYE) na VAT itasaidia maisha ya wananchi. TRA wameambiwa wazinduke nami naunga mkono hoja.
 
Kumbe siku hizi kazi ya rais ni kulalamika…..?!!?….Tumemwajiri miaka mitatu analalamika??!! Anaharibu tu uchumi wa nchi kila uchao
 
Gud observation mzee but still ukisema Utawala wa Kikwete uliongeza idadi ya walipa kodi, hiyo haitoshi hata kidogo kusema ilifanya vizuri kwenye ulipaji wa kodi. Kipimo muhimu cha mafanikio ni uwiano wa ulipaji kodi dhidi ya pato la Taifa.

Sasa kama sisi tunachezea chini ya asilimia 12% ya pato la Taifa licha ya Rais Magufuli kufanikiwa kupandisha mapato kutoka bilioni 800 kwa mwezi hadi trilioni 1.3, utasemaje Kikwete alifanikiwa?
Kwa tafsiri ya bilioni 800 dhidi ya bilioni 1,300 ni dhahiri kipindi cha Kikwete, Tanzania ilikuwa more worse - chini ya asilimia 9%, right?

Tukilinganisha ukusanyaji wa kodi TRA kwa mwezi wa tshs 800 bilioni za Kikwete na tshs 1.3 trilioni za Magufuli in real value terms hakuna tofauti kubwa. Ni tarakimu tu.

Hivyo sera za ukusanyaji wa kodi za Kikwete ni bora zaidi ya Magufuli na wananchi wakati wa Kikwete wameona faida zake zikiwagusa na kuonekana kwa macho.
 
Kama mfumo uliopo ni wa kua biashara kwanini tusiwe nyuma? Biashara nyingi zimekufa kabisa alafu mnaleta mada zenu za kisiasa hapa,,,, mbavvvvvu
Nature ya mfumo hauchochei ukuaji bali udumizi ajenda kuu ni kuzalisha zaidi mashetani ili iwe rahisi kuwatala,mfumo umelenga kuwatawala watu sio kutawala uchumi
 
Inakadiriwa kuwa wafanyakazi walioandikishwa katika mifuko ya hifadhi ya Jamii ni watu milioni 2.1. Hawa ndiyo wanaofanya kazi rasmi za kuajiriwa aidha katika sekta binafsi au ya umma. Assume 30% ya idadi ya watu ni vijana na wazee wasioweza kujitegemea na 40% ni wakulima wanaongoja mazao ya mwaka unabakiza 30% ya wafanyakazi na wafanyabiashara ambao wanapashwa kuchangia kodi kila mwezi. Hawa watakuwa ni watu milioni 16.5 ambapo sasa watu milioni 14.3 wanawatwisha mzigo watu milioni 2.2 kwa jalili ya kubeba watu milioni 55!. Kwa picha hii ndiyo maana kodi ni kubwa mno. Hizi ni takwimu za kubuni karibu na ukweli lakini pengine hali ni mbaya zaidi. Wahusika wakifanikiwa kurekebisha hii na kupunguza kodi kwa wafanyakazi( PAYE) na VAT itasaidia maisha ya wananchi. TRA wameambiwa wazinduke nami naunga mkono hoja.
Gud analysis mzee na natumaini Viongozi wetu wataliona hilo.
Hata hivyo, ni wazi kwa alichokifanya Rais cha kuwatengenezea vitambulisho wamachinga ni uthibitisho wa jinsi alivyoliona tatizo la Tanzania kuwa na base ndogo ya walipaji kodi.
 
TRA fanyeni kazi msimuangushe Rais wetu mzalendo wa kweli.
Nitamchagua tena 2020 hajaniangusha.
Mungu ibariki Tanzania.
Asilimia 99 wanafikiria watapata wapi hela za Xmass, Ada na new year from tax payers. Wizi mtupu
 
Ntaipigia debe TRA siku ikabadilika ikaona watanzania ni wadau halali wa kulipia kodi halali
 
Gud analysis mzee na natumaini Viongozi wetu wataliona hilo.
Hata hivyo, ni wazi kwa alichokifanya Rais cha kuwatengenezea vitambulisho wamachinga ni uthibitisho wa jinsi alivyoliona tatizo la Tanzania kuwa na base ndogo ya walipaji kodi.
Unajua maana ya kitambulisho kweli..sidhani inakusaidia au kusaidia nchi kusifia wazo hilo la kutoa kadi za biashara..limefeli hata kabla halijaanza, Subiri utaona na utomaso wako!
 
Tukilinganisha ukusanyaji wa kodi TRA kwa mwezi wa tshs 800 bilioni za Kikwete na tshs 1.3 trilioni za Magufuli in real value terms hakuna tofauti kubwa. Ni tarakimu tu.

Hivyo sera za ukusanyaji wa kodi za Kikwete ni bora zaidi ya Magufuli na wananchi wakati wa Kikwete wameona faida zake zikiwagusa na kuonekana kwa macho.
Wenye akili ndogo ndio watakaosema Sera za Kikwete zilikuwa bora kuliko za Magufuli. In fact Sera za Kikwete hazioni ndani hata kwenye Sera za Mkapa.
Zingekuwa nzuri, angeondoka madarakani na kuacha fedha za kutosha hazina kama Mkapa alivyoacha kuwa si was kutosha.
Kwenye ukweli uongo hujitenga. Kama Sera za Kikwete zingekuwa nzuri asingeshindwa kuboresha huduma za jamii za muhimu kama anavyofanya huyu wa sasa.
Angalia:
  • Ukarabati mkubwa wa shule kongwe. Hili kwa vilaza siyo kipaumbele coz no one cares!
  • Ujenzi mkubwa wa hospitali na vituo vya afya. Hili kwa wa mijini hawataliona coz no one cares!
  • Elimu bila malipo kiasi cha bilioni 23 kwa Mwezi. Hili wa mijini hawataliona coz no one cares!
  • Upanuzi mkubwa wa Miradi ya umeme vijijini. Hili wa mijini hawataliona coz no one cares!
  • Uundaji wa meli kubwa kwenye maziwa. Hili kwa wale wa Dar hawataliona coz no one cares!
  • Mradi mkubwa wa SGR. Do we really give it the right credit? Not yet coz no one cares!
  • Ufufuaji wa ATCL na ununuzi wa ndege mpya saba. Hili hawalioni coz no one cares!
  • Mradi mkubwa wa Stieglers (Rufiji) Gorge. Hili halionekani coz no one cares!
What they care is just immediate gratification. Hawataki maendeleo ya Nchi bali kwa ubinfasi wao wanataka wawe na majumba mazuri mijini lakini yasiyo na umeme, maji, barabara za lami.

Wanataka wao ndio wawe na hela ili waliliwe na sisi wa vijijini. Wanataka wawe wanatutumia fedha mwisho wa mwezi ili tuwashukuru kwa mioyo yao ya kutujali sisi wenye mlo mmoja vijijini.

Mnampima Magufuli kwa Rula ya ubinafsi ndiyo maana mnamkuta he is not worthwhile. Tuacheni sisi tumpime Rais Magufuli kwa rula ya Utaifa wetu.

We are not after immediate gratification rather we are ready to wait, be it rains or sunshines!!!...
 
Unajua maana ya kitambulisho kweli..sidhani inakusaidia au kusaidia nchi kusifia wazo hilo la kutoa kadi za biashara..limefeli hata kabla halijaanza, Subiri utaona na utomaso wako!
Ninajua ninachoongea. Tutahitaji watu walio committed na kazi. Ukiona umachinga mgumu, rudi kijijini ambako majority ya Watanzania wanaishi. Huko utajilimia mazao yako na kuanza upya. Kama riziki ipo ipo tu lakini haina maana kuwa na wanyonyaji wanaojua kudai haki zao lakini hawawezi kusumbukia juu ya wajibu wao kwa Taifa.

Usifikirie kuwa Nchi yako itakufanyia nini wewe bali fikiria nini utaifanyia Nchi yako.
 
Kitu gani unaelewa..huelewi kitu nani anaona umachinga mgumu? ungekuwa mgumu wangejaa mjini..
 
TRA haina watu wabunifu. Ina watu ambao hawana jipya la kuboresha kulipa kodi. Tukilipa kodi stahiki kwa wingi wetu kodi zitaongezeka. Sio huu utaratibu wa sasa wa kukamua tu sehemu moja bila kujari athari zake
Hilo ndiyo tatizo tulilonalo. Watu walewale wanaolipa kodi 25 years ago ndiyo wanaokamuliwa kodi kila kukicha!!!! Viwango vinaongezwa kwenye PAYE ya civil servants, tunaokunywa ugimbi, wenye magari and the like. Hawaangalii watu wengine ambao wanapata pesa nyingi lakini hawalipi kodi. Wafanyabiashara wenye nyumba za kupangisha, biashara nyingi zisizo rasmi watu hawalipi kodi!!!! TRA wawe wabunifu.

Kuna kipindi Kamati ya Bunge ya Bajeti ilipendekeza vyanzo vipya 13 vya kodi lakini havikupewa kipaumbele sababu nasikia viligusa maslahi ya wenye nchi. Matokeo yake ni kuongeza viwango vya kodi kwa walewale 2.2 million ambao 40% ni wàfanyakaźi wa umma!!!! Ambao wanalipwa kiduchu, kodi (income tax) kubwa na atakapostaafu bado atapewa 25% ya anachostahili ili afe mapema na pesa yake ibaki serikalini!!!! Time will tell
 
Tumekaa kulalamikia utitiri wa kodi, kumbe sisi ndio wavivu, tulikuwa tukifikiriia tu kufanya shughuli za uchuuzi (biashara) na kusahau shughuli kuu ya uzalishaji.

Tulikuwa tumeifanya Tanzania, a rogue state, Nchi inayoishi kiujanjaujanja na kuacha misingi ya kujenga Nchi. Hakuna mtu katika Utawala wa Kikwete aliyejiuliza haya maswali:
Ulikuwa ni mfumo uliooza na it was the matter of time. Matokeo hayo hayakuonekana mapema lakini yamejulikana vyema kwenye Utawala wa Magufuli baada ya Mashirika ya Hifadhi za Jamii kukopwa kushindwa kujiendesha kutokana na mzigo wa madeni. Nani aliikopa NSSF na PPF? Na mashirika kama PSPF na LAPF kwa nini yalikuwa hatarini kufilisika kama mazingira ya kibiashara yalikuwa mazuri - yalipeleka wapi fedha?
Hadithi za wana ccm na wana Magufuli ni kichefuchegu kweli.
Utadhani ccm ndio imeingia madarakani 2015 kumbe ni mbinu yao kubadili shati na kumlaumu mwingine kila baada ya awamu kumbe ni ccm ileile.
Magu kumtangaza utadhani ndio kwanza kaingia kazini akitokea Harvard kumbe ni mtumishi wa serikali hiyohiyo katika ngazi ya juu ya maamuzi Kwa miaka 20 kama WAZIRI.
Ulaghai kila kukicha, mmeshindwa muondoke Kwa hiari wengine wafanye Kwa njia nyingine maana hata uwepo wenu madarakani ni Kwa njia za kulazimisha.
Siasa chafu za ccm zimesababisha wataalamu wazuri wazalendo wamechoka, kukata tamaa au kuishi kinafiki kulinda matumbo yao
 
Alafu angetoa mchanganuo wa hyo mil 55 ya watu.
Maana hapo kuna watoto,kuna vijana ambao hawana kazi,wazee nao hawafanyi kazi.
 
Back
Top Bottom