Rais Magufuli: Nia aibu kwa Taifa lenye watu milioni 55 kuwa na walipa kodi milioni 2.2 pekee. Kenya ina watu milioni 46 na walipa kodi milioni 3.9

Ntaipigia debe TRA siku ikabadilika ikaona watanzania ni wadau halali wa kulipia kodi halali
TRA hawajazaliwa na kushushwa kutoka mbinguni, ni hao hao watoto, kaka, dada na wazazi wetu. Usiwalaumu wao tujilaumu sisi kwani unaweza ukadhani tatizo ni wao kumbe ni uvivu wetu.

Kipimo cha wapi lilipo tatizo, linganisha idadi ya walipa kodi wa Tanzania dhidi ya majirani zake. Tusikwepe madhaifu yetu na kuwasingizia wengine. TRA ni mfumo uliotenfenezwa kutokana na aina ya uchumi tuliyo nayo. Ni TRA hiyo hiyo iliyokuwepo wakati wa Kikwete na sheria ni hizo hizo sema TRA ya wakati huo haikuwa strict na kuachia mianya ya ukwepaji kodi.
 
Well done Mr. President.
Kila siku unajidhihirisha kuwa wewe ni Raisi unaewajali wanyonge. Umefanya jambo la kiungwana sana, Lakini pia umeliongezea Taifa mapato bila figisu figisu.
Wewe ni mwenye maono, unatoa maono, na umewabebesha wasaidizi wako maono yako ili wakusaidue katika utekelezaji wa hayo maono. Naomba Wakuu wa mikoa yote, wakasimamie utekelezaji wa maono yako ili wafanyabishara wadogo wadogo wakawe na vitambulisho halali ambavyo vitawapa uhuru wa kufanya biashara zao bila uoga wowote.

I am so proud to be called a Tanzanian today, simply because of the kinds of decisions and directives you are giving in oder to move forward "Gurudumu la Maendeleo".

Mungu akuongezee Hekima na Maarifa katika kipindi chako cha Uongozi wa Taifa hili la Tanzania.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
Mmeshindwa kuwatoa watu kutoka kwenye umasikini wa kutupwa waje miďdle class, unategemea nini? Hamna ubunifu hili siyo la TRA la serikali kuu ndiyo tatizo
 
Haya unayo ongea ni rhetoric za mtandaoni tu mkuu,hayana uhalisia wowote on the ground.In reality wawekezaji wanazidi kuongezeka.
Namshukuru Mungu ni wananchi wachache sana wanaosoma habari za mitandaoni ambazo ni very misleading indeed.
Wanaongezeka kwa data zipi? Ndio maana unafurahi wengi hawawezi kuingia mitandaoni maana kuna direct relationship na kiwango cha elimu yao ambayo ndio mtaji wenu.
 
Kumbe population yetu inakaribiana sana na ya SA.
Yes, kutoka kuzidiwa na South Afrika mwaka 1978 wakati ikiwa na watu milioni 34 na Tanzania milioni 17, leo hii tuko at par na SA but kwa mwaka huu kuisha inawezekana tukawa tumeshawapita.
Kumbuka mwaka 1978, Nchi hizi zilikuwa zinaizidi Tanzania kwa watu lakini Leo hii tumeshazila tayari kichwa: Algeria, Sudan, Morocco na sasa South Africa.
Sasa, tumebakiza Nigeria, Egypt, Ethiopia na DRC pekee, hivyo Tanzania ni Nchi kubwa barani Afrika sema tu watu sio wazalishaji na hawajitumi kama majirani zetu.
 
Hakuna kitu kipya hapo ambacho kimeanzishwa na Serikali ya Magufuli bali sheria zake zilikuwepo lakini hazikusimamiwa kwa sababu ya utamaduni wetu wa kijinga wa oil kuita kerosene na kerosene pia kuita petroli. Magufuli anatufubdisha Watanzania tujifunze kusema ukweli kwamba hii ni rangi ya njano na siyo ya kijani, ama haya ni mafuta na siyo maji.

Usitake kujilinganisha na Kenya, ambaye ana uchumi usiotegemea uchuuzi bali bidhaa za viwandani. Tanzania imekuwa Nchi ya kutegemea uchuuzi kana kwamba ni Nchi ndogo kama Visiwa vya baharini ama Nchi masikini zenye mafuta zilizobadilika kuwa tajiri kwa kutegemea mafuta.

Kipimo kama tulikuwa na mfumo feki wa kiuchumi, ni namna uchumi wa vijijini ulivyokuwa ukizorota kila mwaka na kutoka kutegemea uuzaji wa mazao ya biashara na bidhaa za viwandani, hadi kutegemea mahindi na mpunga ili kuuza nje ya Nchi, kweli?

Magufuli ni kichwa ndiyo maana anaogopwa na kuchukiwa na waovu kwa kuwa, fursa zao zimekufa.
Ni kama tunazungumza lugha moja na wewe, nilibishana na yule aliyetaka kubadiri topic; Mhe hapa kaonesha kitu kile kile tulicho kua tunakilalamikia wengi kwamba Tanzani KODI ipo juu sana, leo katufungua masikio, kumbe tunalipishwa kodi kubwa kwasababu TAX payers ni watu 2.2Milion only out of 55 Milion, ndio maana kalinganisha na Kenya ambayo wewe hutaki kulinganishwa nao but ok, kaweka Zambia, Msumbiji na of course kaenda mbali zaidi hadi South Africa ameitaja, zaidi pitia kwenye gazeti la Mwananchi, wameandika vizuri, link hi hapa Magufuli apiga 8 nzito
 
TRA hawajazaliwa na kushushwa kutoka mbinguni, ni hao hao watoto, kaka, dada na wazazi wetu. Usiwalaumu wao tujilaumu sisi kwani unaweza ukadhani tatizo ni wao kumbe ni uvivu wetu.

Kipimo cha wapi lilipo tatizo, linganisha idadi ya walipa kodi wa Tanzania dhidi ya majirani zake. Tusikwepe madhaifu yetu na kuwasingizia wengine. TRA ni mfumo uliotenfenezwa kutokana na aina ya uchumi tuliyo nayo. Ni TRA hiyo hiyo iliyokuwepo wakati wa Kikwete na sheria ni hizo hizo sema TRA ya wakati huo haikuwa strict na kuachia mianya ya ukwepaji kodi.
Wakiwa nje ni kaka na Dada zetu. Wakiajiriwa TRA wanageuka miungu watu. That is the reason They have lost a plot. Kazi yao inaonyesha kabisa wamefeli.

Tusianze kuwabembeleza kama wanachofanya ni rocket science
 
Ni kama tunazungumza lugha moja na wewe, nilibishana na yule aliyetaka kubadiri topic; Mhe hapa kaonesha kitu kile kile tulicho kua tunakilalamikia wengi kwamba Tanzani KODI ipo juu sana, leo katufungua masikio, kumbe tunalipishwa kodi kubwa kwasababu TAX payers ni watu 2.2Milion only out of 55 Milion, ndio maana kalinganisha na Kenya ambayo wewe hutaki kulinganishwa nao but ok, kaweka Zambia, Msumbiji na of course kaenda mbali zaidi hadi South Africa ameitaja, zaidi pitia kwenye gazeti la Mwananchi, wameandika vizuri, link hi hapa Magufuli apiga 8 nzito
Mbona Kenya aliitaja jana kuwa ina watu milioni 46 na walipa kodi milioni 3.9? Tena wanavyolipa kodi ni kubwa hadi inafikia asilimia 18% ya Pato lao la Taifa (GDP)?

IMG_0369.JPG
 
Mbona Kenya aliitaja jana kuwa ina watu milioni 46 na walipa kodi milioni 3.9? Tena wanavyolipa kodi ni kubwa hadi inafikia asilimia 18% ya Pato lao la Taifa (GDP)?

View attachment 964388
We jamaa sijui kichwani mwako sijui hua kuna HAJA kubwa tu; hebu angalia hizo takwimu za Kenya uliza type wewe na jedwali uliloweka mwenyewe kama zinafanana!? Mbaf.u, umekaa kibashite bashite tu!
 
Kuna madalali kibao wasio rasmi hapa nchini,lazima wasajiliwe ili walipe kodi.
Wenye nyumba za kawaida pia ni wengi sana hapa nchini,serikali za mitaa ndio wenye data sahihi maana ni rahisi kuwafikia,hawa wenye nyumba pia nyumba zao zisajiliwe na walipe kodi.
Wasafirishaji wenye malori wengi mfumo wao wa ulipaji kodi haueleweki,pia madereva wao hawana ajira rasmi ili TRA iweze kupata PAYE,SDL ,nk.
 
Wewe una lako jambo,alaumiwe ki vipi,nchi ilikuwa inaendeshwa kwa mfumo wa uchumi ulioonekana unafaa kutokana na hali halisi ya maisha yalivyokuwa kipindi hicho.
Unahitaji muda wa kutosha kufahamu kwa nini tuliamua kwenda state owned economy.
Si kitu kilichotoka hewani,ni mfumo katika maisha.Wa Tz ni mabingwa wa kukosoa lakini ukimpa afanye yeye ni kuboronga tu.
Niambie China imeanguka?
Urusi imeanguka?
Mabeberu ndio wamevuruga mfumo wa uchumi wa dunia hii kwa kuwaaminisha nyie watoa lawama kwamba ujamaa ndio shida,shida ni nyinyi,fanyeni kazi.
 
Yes, kutoka kuzidiwa na South Afrika mwaka 1978 wakati ikiwa na watu milioni 34 na Tanzania milioni 17, leo hii tuko at par na SA but kwa mwaka huu kuisha inawezekana tukawa tumeshawapita.
Kumbuka mwaka 1978, Nchi hizi zilikuwa zinaizidi Tanzania kwa watu lakini Leo hii tumeshazila tayari kichwa: Algeria, Sudan, Morocco na sasa South Africa.
Sasa, tumebakiza Nigeria, Egypt, Ethiopia na DRC pekee, hivyo Tanzania ni Nchi kubwa barani Afrika sema tu watu sio wazalishaji na hawajitumi kama majirani zetu.
..plus wewe kutofikiri sawa sawa!
 
Back
Top Bottom