Rais Magufuli, ni vyema ukaacha kulaumu mitandao ya kijamii. Yaliyopo kitaa ni zaidi ya mitandaoni

Zero Hours

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
12,943
18,665
Mtukufu Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ningependa kuchukua nafasi hii kukujulisha kuwa huku kitaa ndyo tunazungumza sana kuliko mitandaoni. Kila mara unapohutubia Taifa, unasikika ukilalama juu ya mitandao ya kijamii lakini ukweli ni kuwa, tukishazungumza mitaani, ndiyo tunaingia mitandaoni kujadili kitaifa zaidi.

Tena bora hata ya mitandaoni maana kuna mitandao mingine kuna Moderators. Kitaa hakuna cha Moderators. Kila mtu anasema atakavyo. Yani kule kitaa ndio kuna "pure ..we dare to talk openly".

Kwahyo mheshimiwa usilaumu sana kuwa watu wanachonga sana mitandaoni. Fanya hata ziara za kushtukiza kitaa ndio utajua watu wanasema nini mitahani.

Halafu pia Mtukufu, punguza basi kushinda mitandaoni. Piga kazi mzee. Hii mitandao itakupa presha bure. U still have a long way to go boss.
 
kama rais anasitua kiki kwa kuwapiagia wasanii, unategemea nini, yeye mwenyewe anashinda kwenye mitandao
 
..anajuaje watu wanamsema mitandaoni kama yeye hashindi mitandaoni??......yeye anafikiri kuzuia watu wasitazame shughuli za bunge ndio kukomesha kukosolewa...amesahau kuwa watanzania wanatumia social media kama mbadala wa yeye kuminya uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kutoa mawazo....anasahau kuwa hizi social media ndio zilipindua hata serikali za tunisia na egypt....na bado.....kila kona akifungua sasa anasemwa...hadi bungeni ambako amezuia watanzania wasiangalie....yeye azidi kumkumbatia bashite...atasemwa mpaka.....hadi huko vijijini sasa wanamsema na bashite wake.....
 
Yaani huyu bashite ndio anazidi kuharibu kila leo watu wanamtaza tu tuone mwisho wake
 
Sasa iv wanahangaika Ku hack account ya yule mmarekani
Na kwa hatua alizo chukua atawachukue hack China awawezi tena
 
Angesikia ya huku mitaani nadhani angetamani dunia ipasuke azame na hasa wanapojadili maisha yake binafsi na ya ndoa yake
 
Sasa mkuu kwa hii thread unataka tuje kung'olewa kucha huku kitaa?

Maana ni bora huku JF na social networks nyingine tunakopiga ngenga kwa fake ID,kitaa ukikamatwa umekamatwa.
 
Back
Top Bottom