Zee la kitaa
JF-Expert Member
- Oct 25, 2017
- 403
- 211
Katika historia ya utawala wa taifa hili; kumejitokeza watu wa aina mbalimbali wanaopinga mambo mbalimbali ya utawala na uongozi katika awamu mbalimbali. Hata kipindi cha mfumo wa chama kimoja kuna kundi la watu wengi waliokuwa wakimpinga Hayati Baba wa taifa, akiwemo hayati Kambona. Kupinga utekelezaji wa serikali ni jambo la kawaida lakini je unatumika katika njia sahihi.
Katika kipindi cha rais John Pombe Magufuli; amefanya mageuzi makubwa ya mfumo wa kisiasa uliozoeleka na jamii ya wanasiasa wengi; na amefanyia kazi kero nyingi ambazo wapinzani walikuwa wanalenga kutekelezeka wakipewa ridhaa ya kuongoza. Wengine wanapinga kwa kukosa ajenda na kuona demokrasia ndio kichaka, bila kutambua hakuna demokrasia isiyo na mipaka. Watanzania wanashindwa kuelewa Mheshimiwa Magufuli ni mti wenye matunda ambao kila mmoja anatamani arushe jiwe ili kupata matunda yaliyopo. Watu wanachokonoa kila aina ya hoja ili mradi waone rais atajibuje. Bahati mzuri tumepata rais anayewatumbua watu wake na shida zake na yeye kujikita huko. Si ishu kuona watu wengi wanajitokeza kupinga harakati za magufuli. Kwa kuwa wengine wanapinga kufuata upepo; wengine wanapinga kwa sababu ya vyama vyao na misimamo ya vyama vyao; wengine wanapinga kwa kuona maslahi yao yameminywa na wengine wanapinga kwa nia njema ila wanashindwa kutambua njia sahihi ya kuwakilisha hoja zao.
Mheshimiwa Magufuli endelea kupiga kazi; kelele zisikusumbue piga kazi; sisi watanzania hatutaki porojo; tumeziona porojo katika miaka mingi ya taifa hili. Ulikubali kuongoza taifa hili endelea na mipango uliyokujiwekea na malengo katika miaka ya awali ya uongozi wako. Watanzania wengi tunakuunga mkono kwa jitihada unazozichukua, ni za kuleta mwelekeo mwema. Tambua kitu kimoja; mti wenye matunda ndio unapigwa mawe. Kama ungekuwa hauna matunda; hakuna mtu hata mmoja angethubutu kutupa jiwe.