Meatu01
Senior Member
- Dec 20, 2016
- 169
- 94
MAGUFULI NI MPIGA FILIMBI WA HAMELIN
Kwa wale waliosoma zamani wataikumbuka hadithi hii murua. Hadithi japo wengi wallichukulia kama kisa cha kubuni ilitokana na tukio la kweli. It was based on a true story!
Katika dokezo mwandishi wa kisa hiki akiitwa Robert Browning aliandika hivi;
'When, lo! as they reached the mountain-side,
A wondrous portal opened wide,
As if a cavern was suddenly hollowed;
And the Piper advanced and the children followed,
And when all were in to the very last,
The door in the mountain-side shut fast'.
Ni kisa cha jamii iliyoishi katika kimji cha Hammelin kukosa uaminifu. Kisa hiki wana historia wanakubali kilitokea mwaka 1284 katika mji wa Hamelin uliopo Lower Saxony, nchini ujerumani. Mji huu ulikumbwa na baa la panya. Mwaka 1284 siku ya Watakatifu John na Paul akatokea mpiga filimbi ambaye alikuwa amevaa koti la rangi nyingi za kung'ara. Akawaahidi watu wa Hamelin kuwa atawaondolea panya wote lakini kwa malipo. Wakazi wa Hamelin wakakubali. Jamaa akaanza kupiga filimbi yake kuelekea pangoni. Panya wote walipoingia pangoni mlango ukajifunga na panya wote wakafia humo. Mpiga filimbi akarejea Hamelin kudai ujira wake. Wakazi wa Hamelin wakajifanya wajanja! Si panya weshakufa? Wakakataa kumlipa na kumwambia nenda zako!
Mpiga filimbi ambaye hakuna aliyekuwa akimjua akajiondokea. Akarudi tarehe 26 Juni ya mwaka huohuo 1284. Hii ilikuwa siku ya watakatifu Joni na Paulo (St John na St. Paul). Akaanza kungurumisha filimbi huku akielekea pangoni! Wana Hamelin wakaanza kumdhihaki! Kwenda zako mapanya yalishaisha! Mara wakashangaa watoto wao ndio wanamfuata mpiga filimbi! Jitihada zote za kuwazuia na kuwaita zikashindikana! Watoto wamepagawa na muziki hawasikii la muadhini wala shemasi! Inasadikika watoto wote 130 waliokuwa kijijini wakaanza kucheza ngololo huku wanamfuata mpiga filimbi kama hawana ubongo! Watoto wakageuka nyumbu aisee! Wakafuata bila kuhoji! Hata wazazi walipopiga mayowe mnaangamia wao mayenu tu!
Kuna kumbukumbu zinaonyesha watoto watatu tu ndio walisalimika! Wa kwanza alikuwa kiziwi hakusikia filimbi hivyo mziki haukumnogea sana akarudi! Mtoto wa pili alikuwa mlemavu wa miguu ikawa tabu kwenda na spidi ya wenzake naye akaamua kurudi. Mtoto wa tatu alikuwa kipofu ikawa kila hatua mbili tatu anajikwaa anaanguka akaona imetosha akarudi.
Kisa hiki kimetafsiriwa kwa aina mbalimbali lakini hii tafsiri ndio imekubalika na wana historia wengi kuwa inawakilisha kilichotokea 1284.
Sasa turudi kwa Magufuli.
Magufuli aliingia madaraka huku nchi ikiwa imejaa mapanya kila kona! Magufuli kaja na filimbi yake! Filimbi imeanza kukusanya mapanya inawapeleka pangoni kuangamia!
Sasa hata kabla mpiga filimbi wetu hajaangamiza mapanya tayari pametokea madhulumati! Yaani hawa ni wabaya kuliko hata wale wa Hamelin mwaka 1284! Walau wale walisubiri hadi mapanya yakaangamia! Hawa wa hamelin wetu wao hata subira hawana! Wameanza kudai mpiga filimbi anayaonea mapanya!
Wanadai mapanya yakibanwa sana yatageuka yatafune nchi kwa hasira!
Tumwambie mpiga filimbi wetu koleza nyimbo! Sisi ukishayamaliza mapanya yetu tutakulipa! Malipo tutakupa oktoba 2020! TOKOMEZA MAPANYA YOTE BILA HURUMA! Na mkazi yeyote wa hamelin atakayehifadhi au kuzuia mapanya kupelekwa pangoni tutakusaidia kuwaadhibu siku ile ile tutakayokulipa ujira wako! Tutakuhuruhusu upige filimbi yakufuate ukayateketeze pangoni kwa mara nyingine!
TANZANIA NCHI YANGU NAKUPENDA!