Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,196
- 25,515
Kwa miaka mingi,Tanzania imekuwa na wanasiasa waongo,walaghai,matapeli na wanaojali matumbo yao. Mzizi wa uongo,ulaghai na utapeli ni kutozungumza ukweli. Tumempata Rais tuliyemtaka kwa miaka mingi.
Rais Magufuli si mbadilishaji au mchezeaji wa maneno. Daima amekuwa akiusema ukweli anaouamini na kuuishi hata kama ukweli huo unachoma,unauma,unakera au unachukiza. Kusema moja kwenye mbili hana. Moja anaiita moja.
Katika hotuba zake,anapotaka kuufikisha ujumbe wake kupitia ukweli,huwataja wanaomkwaza,kumuangusha au kumfurahisha. Humsifia anayestahili na humkemea au kumpa rai anayemwangusha au anayemkwaza. Ni mkweli tu hufanya hivyo.
Daima,Rais haonyeshi uanasiasa wake kwenye mambo ya msingi kwa kuyasema asiyoyaamini. Wanasiasa wamezoea kusema na kutenda tofauti. Wamezoea kuficha ukweli na kuwaaminisha wanaowaamini kisicho cha kweli. Rais hayuko hivyo.
Nitatoa mfano. Angekuwa mwingine angeweza kutuaminisha kuwa punde tutapata Katiba mpya. Angepiga danadana kwa maneno. Rais amesema wazi msimamo wake. Ni kuwa hana mpango wa kuendelea na mchakato kwa sasa,ni heri reli ikajengwe.
Ameanika ukweli wake kuhusu mikutano ya kisiasa;watoto wanaopata ujauzito kuendelea na masomo;uzazi wa mpango;uhaba wa chakula na kadhalika. Uzuri wa kusema ukweli ni kuwa hakuna kujali mjadala unaofuata. Siasa za kitapeli ambazo zilizaa ufisadi hazina nafasi kwasasa. Hakika,we have the President we wanted!
Hapa kazi tu!