Rais Magufuli ni kama anakimbia kuoga mtoni kwenda bafuni eti mtoni hakuna maji mengi!

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,555
35,880
Nilimuona rais Joseph Kabila akipata mapokezi ya kifalme pale alipokaribishwa kuja nchini kwa mwaliko wa rais Pombe John Magufuli, nikajiuliza kuwa huyu siye Joseph Kabila ambaye enzi za rais Kikwete tulikuwa tukipishana naye ikulu huku ujio wake nchini ukiwa wa kimyakimya kuliko kawaida? Huyu siye Kabila ambaye unaweza kwenda ikulu asubuhi na kumkuta katia timu bila hata ya tangazo lolote?

Jana kaja ndugu Lungu naye mapokezi yake ni ya kufana hapo bado yule kiongozi wa Morocco aljvyopokelewa kishujaa.

Ghafla bin vuu rais Magufuli amepoteza uwekezaji kiasi cha kuwakumbatia viongozi ambao enzi za JK walionekana kama sehemu tu ya wananchi wa Tanzania "kifikra"? Sikujua kwa nini Kikwete alikuwa akimuona mtu kama Bill gate ni muhimu kwenye uwekezaji kuliko hawa kina "pangu pakavu patie mchuzi ambao tunawakumbatia sasa" mpaka hapo nilipoona jinsi walau tunavyohaha hata kuwatafuta kina Kabila ambao kwa sasa kwetu ni lulu(? ) Hapa ndipo ninapogundua hasa ni nini maana ya kipaji kwa kila mmoja wetu.

Ukweli ni kuwa hata yeye mwenyewe yule niliyekuwa nikipishana naye pale ofisini atajiuluza sana huu ululu kwa sasa unatoka wapi? Mimi wakati yeye akijiuliza hivyo nina jiuliza tena kwa mashaka makubwa "ama tumerudi nyuma sana" leo tunamvuta Kabila kwenye kutumia bandari ileile aliyotumia miaka nenda rudi kwa kumpa "ofa ya kupitisha mizigo free kwa mwezi mzima"?

Nilitamani sana siku moja niwe kiongozi mkubwa wa nchi lakini kwa sasa nimegundua kuwa uongozi ni kipaji! Kama huwezi ni huwezi tu! Kabla ya kuingia ni lazima nitajitafakari sana.

Nadhani atakayekuwa amenielewa basi amenielewa!
 
Back
Top Bottom