Rais Magufuli ni chaguo la Mungu amebeba maono ya nchi siyo CCM ni vema Chadema na wapinzani wamuunge mkono

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
50,897
2,000
Kiukweli kila nikimtazama Rais Magufuli naona dhahiri amevuka level ya siasa za vyama na sasa anaitumikia nchi katika mustakabali mpana.

Kwa namna anavyoenenda ni ukweli ulio wazi Rais Magufuli anatumikia maslahi ya nchi japo kwa kuongozwa na Ilani ya CCM lakini kwa ubunifu binafsi wa kuleta maendeleo kwa haraka.

Nimetoka kuzipitia ilani za uchaguzi za ACT wazalendo, NCCR Mageuzi, TLP, Chadema na CUF ni dhahiri malengo yote ya maendeleo yaliyoainishwa kwenye ilani hizo yameshafikiwa.
Kwa upande wa ilani ya CCM ambayo imebeba mambo makubwa zaidi yenyewe imetekelezwa kwa takribani 99%

Sasa kwenye ubunifu binafsi hapo mwenye macho haambiwi tazama, miradi yote imeshika kasi na hapa ndipo wabunge wengi hata kama hawaipendi CCM lakini Juhudi za Rais Magufuli wameziona na kwa hiyari yao wameamua kumuunga mkono ama kupitia hiyo hiyo CCM au NCCR Mageuzi na hata TLP.

TLP wao wameshamteua Dr Magufuli kuwa mgombea wao wa urais.

Nawatakia Sabato yenye baraka.

Maendeleo hayana vyama!
 

Bia yetu

JF-Expert Member
Apr 14, 2020
6,925
2,000
Chadema wanampenda sana Rais Magufuli
Sema wanamuogopa Mbowe kukiri hadharani
 

Magezi

JF-Expert Member
Oct 26, 2008
3,340
2,000
Kiukweli kila nikimtazama Rais Magufuli naona dhahiri amevuka level ya siasa za vyama na sasa anaitumikia nchi katika mustakabali mpana.

Kwa namna anavyoenenda ni ukweli ulio wazi Rais Magufuli anatumikia maslahi ya nchi japo kwa kuongozwa na Ilani ya CCM lakini kwa ubunifu binafsi wa kuleta maendeleo kwa haraka.

Nimetoka kuzipitia ilani za uchaguzi za ACT wazalendo, Nccr mageuzi, TLP, Chadema na Cuf ni dhahiri malengo yote ya maendeleo yaliyoainishwa kwenye ilani hizo yameshafikiwa.
Kwa upande wa ilani ya CCM ambayo imebeba mambo makubwa zaidi yenyewe imetekelezwa kwa takribani 99%

Sasa kwenye ubunifu binafsi hapo mwenye macho haambiwi tazama, miradi yote imeshika kasi na hapa ndipo wabunge wengi hata kama hawaipendi CCM lakini Juhudi za Rais Magufuli wameziona na kwa hiyari yao wameamua kumuunga mkono ama kupitia hiyo hiyo CCM au Nccr mageuzi na hata TLP.

TLP wao wameshamteua Dr Magufuli kuwa mgombea wao wa urais.

Nawatakia Sabato yenye baraka.

Maendeleo hayana vyama!
Vitu vingine Mungu mnamsingizia bure
 

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
14,027
2,000
Si kila chaguo la Mungu ni zuri, kuna mengine uyaleta kama somo, au adhabu kwa nchi husika,

Mungu anaweza kuwa kawapa watanzania adhabu
1.Kupata Kiongozi katili
2.Mnyang'anyi
3.Mwenye kibri
4.asiye na huruma moyoni bali mdomoni
5.Wa kuvuruga amani na umoja wa kitaifa

Nitashangaa kama ziwadi ni kupatiwa kiongozi
A.ambaye ndani ya uongozi wake ndo watu wanapigwa risasi
B.watu wanapotea na kupotezwa
C.Watu wana uana kwa interest ya kuwafurahisha walio wachagua
D.Watu wan an yang'anywa mali kwa kisingizio cha uhujumu uchumi
E.Wawekezaji wanachukuliwa mali zao
F.Wahitimu hawana ajira
G.Huduma za afya zimezorota
H.Waandishi wa habari wanasingiziwa
I.Viongozi wastaafu wanatukanwa
J.Kwakweli tunatengwa na dunia


Labda kama ni adhabu toka kwa Mungu

Britannica
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom