Rais Magufuli ndiye aliyeanzisha tatizo la msingi la ukomavu wa kisiasa ndani ya Tanzania

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,555
35,874
Kwanza kabisa naomba niseme kuwa tatizo hili ninaloenda kuliainisha hapa chini ndilo hasa hutumiwa na madikteta wote wa Africa ili kujiimarishia nafasi ya kiutawala na sifa ambazo kimsingi ni za kupumbaza.

Hivi tujiulize, enzi za Kikwete haukuonekana utendaji wake wa miundombinu kiasi cha kuwavuta wanasiasa wa upinzani wahamie CCM?

Sisasa za kipuuzi zinazofanywa na Humphrey Polepole, kijana asiye na nidhamu katika siasa huku zikiungwa mkono na rais Magufuli kwa mamlaka aliyonayo zinadumaza ukuaji wa demokrasia na kuzaa wanasiasa njaa, wasio na weledi wa kisiasa zaidi ya kukaba "vitonge" vinavyopita mbele yao. Namshukuru sana mzee Kikwete na Nape Nnauye kwani siasa za aina hii hawakuzipa nafasi.

Huu ujinga anaofanya Humphrey Polepole wa kumuahidi rais Magufuli kuwa kila kwenye mkutano muhimu atamletea vigogo kadhaa kutoka upinzani kwa makubaliano kuwa asimuangushe kwenye kuwapatia "Asante" ndiyo hasa upuuzi ninaouzungumzia huku nikimuona Polepole kama mwanasiasa mufilisi asiyejua maana ya siasa safi na yenye afya.

Kumrubuni Katambi kisha kumuomba rais Magufuli asimsahau kama "asante" ya fadhila na au kuwarubuni wanasiasa wengine ambao tunajua mchakato mzima wa mazungumzo kati yao na Polepole kwa kuwahadaa na vyeo ambavyo wao kwa wao wameahidiana kuwa viende kwa wana CCM ni siasa za kiwango cha chini zinazoenda kuzaa "wajinga" ambao siku si nyingi watakuja kuwageuka.

Yote kwa yote, aina hii ya siasa imehasisiwa na rais Magufuli mwenyewe pale alipoamua kugawa nafasi za utendaji kwa makada "njaa" wa CCM.Magufuli kama kiongozi mkuu wa nchi, kwa hili alianza kutoa uelekeo mbaya kwa nchi na hatimaye limeanza kuwalevya watu kama kina Polepole, Mnyeti, Gambo na wengine wanasiasa hovyo wa aina hiyo.

Tunataka waelewe kuwa tunajua wanayoyafanya, pia tunawapa taarifa kuwa muda muafaka ukifika watajikuta vinywa wazi na hapo ndipo watakapouona "utupu" wao katika siasa.

Leo tunasema, kesho tutatimiza azma yetu....Wao waendelee na ujuha wao wa siasa za kijinga, zilizokosa afya!
 
Hivi mtu akitoka ccm na kuja cdm ni hero! Akitoka cdm kwenda ccm nongwa hapa JF why?
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom