Rais Magufuli: Nawaambia TCRA makampuni ya simu yasiyotaka kulipa kodi, Futa kabisa hiyo kampuni!

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,251
Rais kashafika eneo la tukio na anakagua jengo na mfumo wenyewe.

Tayari rais kaingia ukumbini; Pia yupo Makamu wa rais Mama Samia Suluhu Hasan, Rais wa Zanzibar Dr Shein, Waziri wa Mawasiliano Prof Makame Mbarawa, Waziri wa Fedha Dr Philip Mpango.

Sasa ni kamishna mkuu wa TRA akisoma ripoti kuhusu mfumo huu mpya wa ukusanyaji wa mapato.



Dokta Shein: Serikali haziwezi kuendesha nchi bila kulipa kodi. Nazipongeza wizara ya fedha ya JMT na Wizara ya Fedha ya Zanzibar.
=>Uchumi unajengwa na wananchi wenyewe, uchumi unajengwa na serikali kukusanya kodi

Rais Magufuli anakaribishwa kuongea na kuzindua mfumo

Rais Magufuli: Leo nina furaha kubwa kwasababu ninapenda kukusanyiwa kodi. Inawezakana isiwe furaha kwa wakwepa kodi.

=>Baada ya kutembelea kituo hiki kwa hakika nimeridhika, nawapongeza wote waliobuni na kutengeneza kituo hiki

=>Taasisi za serikali na makampuni binafsi watakaotunza taarifa zao katika kituo hiki watakuwa na usalama.
Kituo hiki kitakuza teknolojia katika nchi yetu pia kitasaidia kukuza uchumi wa nchi yetu.

Kituo hiki kimeanza kufanya kazi toka Oktoba lakini mpaka sasa ni taasisi tatu zimejiunga.
=>Pamekuwepo na baadhi ya wadau kufanya udanganyifu. Fedha ya serikali inatakiwa ikae mikoni mwa serikali.
Kumekuwepo na watu wanaolalamika kuonewa kubambikiziwa kodi na wanaokwepa kodi

=>Nimefurahi wakuu wa makampuni na mabenki mpo hapa maana ninyi ni walipaji kodi.
Mwaka 1992 TTCL ilikuwa haipati faida sana lakini ilikuwa inaweza kutoa divident serikalini kwa mwaka huo waliweza kulipa divident ya milioni 1.

=>Baada ya kubinafsisha na kuuza share ya asilimia 40 hatukupata divident hata siku moja. Baada ya kuona hatupati chochote tumeamua kuchukua na kununua hisa zote.

=>Ethiopia wana kampuni moja tuu ya telecommunication. Na kwa mwaka jana wametengeneza faida ya zaidi ya bilioni moja point tano dola za kimarekani.

=>Fedha walizokusanya Ethiopia ndizo walizotumia kujenga reli. Biashara yoyote lazima iwanufaishe wahusika wa nchi.
Tulitoa muongozo kwa makampuni ya simu wawe registered kwenye soko la hisa la Dar es Salaam na wamesuasua mpaka sasa.

=>TCRA wanatoa faini ndogo na inawafanya makapuni ya simu yaendelee na ukwepaji kodi.
Mimi nawaambia TCRA makampuni yasiyotaka kulipa kodi, Futa kabisa hiyo kampuni.

=>Ni lazima kila mmoja alipe kodi; awe anataka au hataki.
Niwaombe makampuni muingie katika hii data centre. Kama mtu unalipa kodi unaogopa nini kujiunga na mfumo huu?

=>Wale walio chini yangu wala siwaombi na naomba makamu wa Rais ukasimamie hili.

Mtu anaponunua vocha au kufanya transaction ya pesa ameshalipa kodi, Peleka hiyo VAT kwa serikali.

=>Ethiopia ina kampuni moja ya simu ila sisi Tanzania tuna kampuni zaidi ya saba za simu.

=>Nitolee mfano mdogo tuu, Tanzania tungekuwa na senta moja ya kupima na ku-lebel dhahabu tungepata mapato mengi sana.

=>Tungeanzisha hata vitambulisho vya machinga na tukaviuza kwa shilingi elfu kumi tungepata mapato mengi sana.

Kodi za nyumba watu hawalipi kwasababu hamna utaratibu mzuri

=>Hata hivyo nawapongeza sana vijana waliobuni mfumo huu, japo mmesema wanamefanya bure lakini najua wanalipwa mshahara. Jinsi mfumo huu utavyoendelea kusaidia kukusanya mapato tutawafikiria kuwaongeza mishahara.

=>Najua tuna data centre nyingi. Sasa nisione wizara au idara ikijenga data centre nyingine

=>Niwaombe makampuni, wafanyabiashara mjiunge na mfumo huu.
Naomba nimshukuru sana Rais wa Zanzibar Dr Shein, Makamu wa rais, waziri wa fedha, waziri wa mawasiliano

=>Narudia wito wangu kwa kuwaomba sana sana, ndugu zangu wenye makampuni ya simu muwe wa kwanza kujiunga na mfumo huu. Mimi mwenyewe namiliki laini ya Vodacom, Airtel, Tigo na TTCL.

Niwashukuru sana , Mungu Ibariki Tanzania
 
Sasa hivi kodi imekuwa kama adhabu, yaani kodi ya chini kwa biashara ndogo ndogo ilikuwa 150,000/= mwaka jana mwaka huu wa fedha imepanda mpaka 318,000/= daaah! maisha haya ni shida yaani bila kufanya ukaguzi wala nini wao wamepandisha tu, duka saloon kweli hii ni kusoma namba.
 
Sasa hivi kodi imekuwa kama adhabu, yaani kodi ya chini kwa biashara ndogo ndogo ilikuwa 150,000/= mwaka jana mwaka huu wa fedha imepanda mpaka 318,000/= daaah! maisha haya ni shida yaani bila kufanya ukaguzi wala nini wao wamepandisha tu, duka saloon kweli hii ni kusoma namba.
Hii ni kweli mkuu ?
 
Sasa hivi kodi imekuwa kama adhabu, yaani kodi ya chini kwa biashara ndogo ndogo ilikuwa 150,000/= mwaka jana mwaka huu wa fedha imepanda mpaka 318,000/= daaah! maisha haya ni shida yaani bila kufanya ukaguzi wala nini wao wamepandisha tu, duka saloon kweli hii ni kusoma namba.
Hahahaaa,this is dangerous!
 
Na yeye mapato yake Magufuli ni kiasi gani? Asikae kusumbua wanaume wanaumiza kichwa kwenye biashara alafu yeye mamilioni zake katunza benki,yeye mwenyewe keshazeeka mamilioni hayo anayopokea mshahara anamtuzia nani ? Yeye mwenyewe mkwepa kodi
 
Back
Top Bottom