Uchaguzi 2020 Rais Magufuli: Nataka Mwigulu ashinde hapa na Kitila Mkumbo ashinde Ubungo. Wote nawapenda

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
55,416
85,844
Mgombea wetu wa Chama chetu aliwahi kusema kuwa hana Mgombea na wala hajawahi kutuma mtu agombee, video hii hapa



Leo kabadilika anasema kwakuwa Mwigulu na Kitila wote ni Wadogo zake basi ameona mmoja abaki Huko na mwingine aende Ubungo na anataka wote washinde. Angalia attachment.

Tusiwe wasahaulifu, kuna maisha baada ya siasa. Tunakumbushana hatujatukana, yule ni Mzazi, Baba, na kiongozi!

"Mwigulu ninamfahamu na ninampenda sana, lakini Mwigulu ni kama mdogo wangu maana amesoma Chuo Kikuu na mdogo wangu na Prof Mkumbo naye nampenda ndiyo mana nikasema huyu agombee hapa na yule akagombee Ubungo na nataka wote washinde" - Rais Magufuli

1599116426607.png
 
Hiyo ni lugha ya kuombea kura.

tatizo watu hawajui kutofautisha hotuba ya kuomba kura na hotuba za kawaida za kimkakati.

Muwe basi mnafuatilia chaguzi za nchi nyingine hasa zilizo endelea, mtajifunza mengi na kujua kuwa, unatakiwa uchague cha kupost kutoka kwa yanayoongewa huko kwenye kampeni na sio kupost kila kitu.
 
HIYO NI LUGHA YA KUOMBEA KURA
TATIZO WATU HAWAJUI KUTOFAUTISHA HOTUBA YA KUOMBA KURA NA HOTUBA ZA KAWAIDA ZA KIMKAKATI.
MUWE BASI MNAFUATILIA CHAGUZI ZA NCHI NYINGINE HASA ZILIZO ENDELEA, MTAJIFUNZA MENGI NA KUACHA KUPOST YANAYO ONGEWA HUKO KILA DAKIKA...
Kumbe, basi sikujua!
 
Nimegundua Rais kukosa “consistency” kwenye maneno yake ni kitu kinachokosolewa na watu wachache sana, wengine ni kama hawaoni na hata kama wanaona hawaelewi kama ni tatizo, Nadhani sababu kuu ni “kufanana naye”, Watanzania wengi ni waongo, vigeu geu na hawawezi kusimamia maneno yao. Huu umegeuka kuwa ni utamaduni wa mtanzania. ( M-bongo)

Consistency ni moja kati ya interpersonal skill ambayo mtu anaweza kufundishwa, kwanini wasilifanyie kazi hili suala? Ni jambo la kufedhehesha Rais kila mara ananukuliwa akitoa kauli zinazokinzana, kila mara anakula matapishi yake, aibu kubwa.
 
Back
Top Bottom