johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,860
- 141,794
Kwanza napenda kumshukuru aliyekuwa Meya wa Dsm Isaya Mwita kwa kutolea ufafanuzi namna miradi wa ujenzi wa stendi mpya Mbezi ulivyoratibiwa.
Mwita amekubaliana na Rais Magufuli kwamba thamani ya mradi ni sh 51 bilioni na kwamba hadi yeye anaondolewa ofisini kulikuwa hakuna ongezeko lolote.
Hii maana yake ni kuwa thamani ya mradi iliongezeka baada ya meya wa CCM kuchukua madaraka.
Nikuombe sana Rais Magufuli ambaye ndio mwenyekiti wetu wa CCM kama ulivyoahidi leo uchunguzi wa jambo hili ufanyike kwa haraka.
Hii itawapa wepesi wenzetu walioko Ubungo na Kibamba wanaopigania kukomboa majimbo kwani kwenye ufisadi hakuna swala la huyu ni " mwenzetu"
Kama madiwani wa CCM waliongeza hizo sh bilioni 20 kiujanja ujanja basi sheria ichukue mkondo wake, kwani ukitaka kuuwa tumbili usimuangalie usoni.
Maendeleo hayana vyama!