Rais Magufuli naomba uwashughulikie haraka waliofisadi mradi wa stendi mpya Mbezi, CHADEMA wamekiri mradi ni sh bilioni 51 siyo 71!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
36,637
2,000
Kwanza napenda kumshukuru aliyekuwa Meya wa Dsm Isaya Mwita kwa kutolea ufafanuzi namna miradi wa ujenzi wa stendi mpya Mbezi ulivyoratibiwa.

Mwita amekubaliana na Rais Magufuli kwamba thamani ya mradi ni sh 51 bilioni na kwamba hadi yeye anaondolewa ofisini kulikuwa hakuna ongezeko lolote.
Hii maana yake ni kuwa thamani ya mradi iliongezeka baada ya meya wa CCM kuchukua madaraka.

Nikuombe sana Rais Magufuli ambaye ndio mwenyekiti wetu wa CCM kama ulivyoahidi leo uchunguzi wa jambo hili ufanyike kwa haraka.
Hii itawapa wepesi wenzetu walioko Ubungo na Kibamba wanaopigania kukomboa majimbo kwani kwenye ufisadi hakuna swala la huyu ni " mwenzetu"

Kama madiwani wa CCM waliongeza hizo sh bilioni 20 kiujanja ujanja basi sheria ichukue mkondo wake, kwani ukitaka kuuwa tumbili usimuangalie usoni.

Maendeleo hayana vyama!
 

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
4,516
2,000
Hapo mnyika hachomoki walipata 10% sasa watakiona
 

mugah di mathew

JF-Expert Member
Jul 28, 2018
3,727
2,000
Kwanza napenda kumshukuru aliyekuwa Meya wa Dsm Isaya Mwita kwa kutolea ufafanuzi namna miradi wa ujenzi wa stendi mpya Mbezi ulivyoratibiwa...
Kwani unadhani waliomtoa meya Mwita walikuwa na nia njema zaidi ya ufisadi? Na kwa ongezeko la billion 21 jua kabisa Jafo nae kwa Njia moja ama nyingne alihusika
 

Mzee Chayai

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
218
500
Kwenye tuhuma nzito Kama hii, unaachaje kumhusisha aliyekuwa RC wa Dar kwa kipindi hicho?? Huyu ndiye aliratibu uhuni wote wa kumtoa Isaya Mwita kuwa meya wa jiji ili CCM wafanye huu ufisadi
 

mhanila1

JF-Expert Member
Dec 15, 2017
991
1,000
Lazima wateme ndoano na hapo sasa kampeni za ubungo imekuwa kazi rahisi sana kwa upinzani
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom