Rais Magufuli, naomba ubadili mtazamo wako kuhusu wale wanaokuambia maisha ni magumu na uachie Pesa

Mimi ni mjasiria mali wa Private Nilikuwa na watu 108 Sasa Nina watu 12 kima Cha chini kilikuwa Tsh 400000 kima Cha juu 2.4ml nimepunguza watu maisha yaende mbele. Nimewapunguza nawaonea huruma na najionea huruma. Nilikuwa naingiza kontena 28 Kwa mwaka Sasa naingiza kontena 8 Kwa mwaka .Nilikuwa gari na mbili Za matumizi Nina moja na natumia bajaji zaidi .Pamoja na ugumu huu namuunga mkono Magufuli nikiamini maumivu yangu haya ni faida ya Tanzania ya baadae
 
Mimi ni mjasiria mali wa Private Nilikuwa na watu 108 Sasa Nina watu 12 kima Cha chini kilikuwa Tsh 400000 kima Cha juu 2.4ml nimepunguza watu maisha yaende mbele. Nimewapunguza nawaonea huruma na najionea huruma. Nilikuwa naingiza kontena 28 Kwa mwaka Sasa naingiza kontena 8 Kwa mwaka .Nilikuwa gari na mbili Za matumizi Nina moja na natumia bajaji zaidi .Pamoja na ugumu huu namuunga mkono Magufuli nikiamini maumivu yangu haya ni faida ya Tanzania ya baadae
Ukiwa mjinga na pumbavu Kama wewe ku*ma ulivyo unakuwa hujui kuunda hoja, unamuunga mkono kafanya nini na maumivu yako kiuchumi yametokana na nini na kwa nini uishiwe badala ya kusonga mbele, mbwa ku*ma wewe, kuna watu mlikuja kuijaza Dunia, huna faida yoyote punguani wahedi wewe
 
Nadhani watanzania waliomo kwenye sector ya ujenzi au ukandarasi wangekuja na mikakati mizuri ya ku compete au kushindana na makampuni ya nje wangeweza sana kubadili hali hii na isingekuwa mbaya kama ilivyo. Kwanza wangegundua Serikali matumizi yake kwa asilimia nyingi yanaenda wapi? Utagundua ni kazi za ukandarasi. Sasa badala ya wao kuungana waweze kupewa contracts kubwa kubwa bado kila moja anatenda mwenyewe kitu ambacho nafikiri kimepitwa na wakati. Lets them join together and share the BIG cake of the 5th Phase Government Expenditure.
Kama tunaendelea kuzubaa, hii miradi mikubwa tutanufaika tu na mishahara ya makarani na Walinzi kwenye site za ujenzi. Na miradi ikiisha basi ndo nasisi tunashutuka kumeshakucha asubuhi.
 
Kuna mtoto anasoma bure?
Unajua maana ya Elimu bure au unaropoka tu?
Mkuu, tatizo kubwa kwa watu wengi hawaoni uhalisia wa mambo, wao hupenda kuongea kile tu ambacho wameaminishwa, ubure na ubora wa hiyo elimu hata hawana uelewa juu yake.

Na jambo lingine lenye ukakasi mkubwa, ni pale watu wanapopenda kusifia kila kitu tu, hata kama kiongozi anatekeleza wajibu wake alioagizwa kupitia ilani ya chama chake, na tena kwa kutumia kodi za wananchi wenyewe, lkn watu wanaamini anachokifanya ni fadhila kwao na wala si haki kwa wananchi. Kalaghabao!

Jamani ebu tujifunze kutoka kwa majirani zetu, mfano kwa nchi kama Kenya, endapo nao wanasifu ujenzi wa SGR yao, ununuzi wa ndege zao, ujenzi wa bandari kubwa ya Lamu, mpango wa BBI, uchimbaji na na usafirishaji wa mafuta ghafi, na mambo mengine makubwa kuliko sisi kama yametawaliwa na tenzi za kusifu na kuabudu kila uchwao kwa viongozi wao.
 
Ukiwa mjinga na pumbavu Kama wewe ku*ma ulivyo unakuwa hujui kuunda hoja, unamuunga mkono kafanya nini na maumivu yako kiuchumi yametokana na nini na kwa nini uishiwe badala ya kusonga mbele, mbwa ku*ma wewe, kuna watu mlikuja kuijaza Dunia, huna faida yoyote punguani wahedi wewe

Pole kwa maumivu ya maisha, lakini usinishambulie ,ili familia au jamii yoyote iweze kusonga mbele Kuna wakati unahitaji kufunga mkanda Kwa maumivu na kujipa matumaini ili uweze kufikia maendeleo. Ili tufikie maendeleo lazima tujenge barabara na umeme huduma ziwafikie watu kule Ipinda ,Magoma,Kazuramimba,Serengeti.Hatuna njia tuvumilie tutafika
 
Hata kama tukifanikiwa kufanya mabadiliko kwenye nyanja hizi, bado itachukuwa muda kuona nafuu ya maisha:
1. Ongezeko la idadi ya watu
2. Ubora na Uhalisia wa Elimu
3. Afya na ustawi wa jamii,
4. Ustawi wa Sekta Binafsi
5. Uwekezaji wenye manufaa kwenye teknolojia na uvumbuzi, hasa katika sekta ya agro-industries, utafiti, biashara...

Ukijiuliza wengi wao watoto wao wamepita njia zipi na wanafanya nini utaelewa mtenda na mtendwa dunia zao tofauti..
 
Sasa unadhani pesa inaachiwa kama maji kule Ruvu juu na chini?! Kwamba maisha ya huyu mtoto magumu unamwaga pesa barabarani?!
Pesa unaipata kwa kufanya kazi au biashara halali tu, otherwise ucheze michezo ya kubahatisha.
Kwa uelewa wako, unadhani Magufuli anawezaje kuachia pesa?! Au pesa inaachiwaje maisha yako yakiwa magumu?!
Mbona mleta mada ameeleza jinsi ya kuachia katika andiko hili!!? Au wenzangu bongo zimefubaa kwa matatizo ya kifedha kiasi cha kushangilia matusi ya wakubwa!!!?
 
Jiwe ni mmoja ya waathirika wakuu wa nguvu hasi. Mambo yote ya kustaajabisha anayoyafanya yanatokana na negative energy ambayo amekuwa akiipanda miaka na miaka.

Natamani kuona wataalamu wa saikolojia wakianzisha utaratibu wa kuwasaidia viongozi wetu ku manage emotions zao.

Laiti kama wataalamu wa akili ya binadamu wangejitokeza mapema kabla jiwe hajafikia hatua hii ya juu kabisa kiuongozi basi taifa letu lingekuwa kwenye mikono salama ya watawala unlike hali ilivyo hivi sasa.
Hebu mkuu dadavua kidogo juu ya hii "nguvu hasi" inavyofanya kazi. Nafikiri ni aina ya athari ya kisaikologia. Nikiri kwamba hata mimi nina hisia kama wewe kuhusiana na yale niyaonayo kwa jiwe anapokuwa mitaani dhidi ya watu.
 
Kwanza namshukuru Mungu kwa kunipa Wasaa huu muhimu na muafaka wa kuzungumza mambo haya kwa uchache.

Mhe. Rais ni kweli unajitahidi kufanya mazuri kwa kiwango chako kwa kadiri Mungu alivyokujalia. Umefanya mambo mazuri kwa kuyatambua naomba niyataje kwa uchache. Umenunua ndege, Umefanya elimu bure kuanzia elimu ya msingi mpaka Kidato cha nne, Umefufua reli ya Kaskazini, Umeanzisha Channel Maalumu ya TANZANIA Safari, ujenzi wa reli ya Kisasa ya mwendo kasi, miongoni mwa mengine.

Mhe. Rais kwa vile unapenda ukweli kama unavyojinasibu mbele za watu kuwa unasema kweli. Na mara kadhaa umekuwa ukisema kuwa unasema kweli na kuwachana ukweli.

Basi nami kijana wako naomba nikupe ukweli. Najua ukweli unauma. Lakini ni bora kusema Ukweli kuliko kuwa Mnafiki.

Mhe. Rais naomba ubadili mtazamo wako kuhusu wale wanaokuambia maisha ni magumu na uachie Pesa.

Nilikusikia juzi ukiambiwa na kijana mmoja kuhusu suala la kuachia pesa lakini nasikitika kusema kuwa sikutegemea kama ungetoa majibu ya namna ile pale Igunga.

Naomba ninukuu Kauli ya Mhe. Rais pale Igunga.
“Usipofanya kazi hela zitaisha tu. Ukitaka hela fanya kazi. Wapo wanaolima mpunga sasa hivi na baada ya miezi kadhaa watapata hela. Sasa wewe unakaa hapa kijiweni kila siku unalalamika kuhusu hela.”

Mhe. Rais sio kila mtu anayekuambia maisha magumu au pesa hakuna basi mtu huyo hafanyi kazi. Kwa heshima na taadhima naomba ubadili huo mtazamo uachane nao.

Na naomba kama kuna washauri wanaokuambia hivyo basi jua kuwa wanakupotosha na wanakuhujumu.

Mhe. Rais ikiwa itakupendeza unaweza iangalia ile Video inayokuonyesha Ukiwa Igunga na Yule kijana. Utagundua kuwa Wakati yule kijana alipokuwa anaongea kuhusu maisha magumu na kukusihi uachie pesa watu wote walipiga makofi huku wakifurahia kana kwamba wamepata mkombozi wa kuwasemea. Huenda walitegemea jibu la faraja na la maana kuhusiana na hoja ya mwananchi mwenzao. Lakini kwa masikitiko makubwa haikuwa hivyo.
Mhe. Rais nakusihi achana na huo mtazamo kuwa watu wanaosema maisha magumu ni wale wasiofanya kazi. Kuna wakati nilikusikia ukisema ati wanaolia pesa hakuna walizoea pesa za kuiba na za misheni town.

Mtazamo wako huo unafanya uwapuuzie Watanzania wengi wanaoona maisha ni magumu. Huko ni kuwapuuzia hakika. Mtu anakuambia maisha magumu na anatoa mifano alafu unamwambia aache uvivu. Aache kukaa kijiweni. Sijui akalime sijui matikiti na nyanya.

Mhe. Rais. Bila shaka hujui jambo hili. Na kama unajua basi unapuuzia kwa makusudi.

Unajua kuna watanzania zaidi ya maelfu wameajiriwa katika viwanda wanafanya kazi kama punda huku wakilipwa mishahara isiyozidi laki mbili. Tena wanafanya kazi zaidi ya masaa kumi na mbili. Wengine wakifanya usiku kucha. Huku wengine wakifanya kazi mchana kutwa mpaka usiku.

Hao nao huko wanakofanya kazi ndio wanakaa vijiweni. Huko kwenye viwanda vya tumbaku ndio wanapiga umbea wao ndio maana wanalipwa mshahara kidogo.

Mhe. Rais najua hujui jambo hili na kama unajua basi unapuuzia. Hivi unajua kuwa wapo maelfu ya vijana wanafanya kazi bila malipo. Naam wanafanya kazi kwa kujitolea bila kulipwa. Vijana hao wamesoma elimu za viwango vya juu kabisa. Wapo wa degree, wapo wa diploma, na ndugu zetu wa Certificate.

Hao watasema maisha ni rahisi wakati wanayaona magumu. Watu wamesoma wanafanya kazi hawapati pesa bado waseme pesa ipo. Alafu Mhe. Rais unakuja unasema wafanyekazi. Kazi zipi hizo zenye pesa ili wakafanye.

Wapo vijana maelfu elfu wamejiingiza kwenye Kilimo. Wapo kina Mama na wababa walikopa kwenye Mabenki ili wakalime matikiti na nyanya. Wengine wakalima Pamba na Korosho lakini kilichowatokea hakuna ambaye hafahamu. Ni Kilio na maombolezo kila mahali.

Leo watu hawa unawaambia hawafanyi kazi. Sasa kama mtu analima hapati na akipata bado soko linatikisika, mtu anafanya kazi analipwa mshahara kidunchu huko viwandani na kwenye mataasisi mbalimbali. Alafu unawaambia hamfanyi kazi. Looh! Masikhara haya Mhe. Rais.

Mhe. Rais vipi kuhusu Watumishi Waumma. Miaka minne sasa hakuna nyongeza ya mishahara. Badala ya serikali yako tukufu unayosema ni serikali ya wanyonge badala iwaongezee mishahara na posho lakini matokeo yake inawaongezea makato ya kila namna. Sijui bodi ya mikopo imeongezwa makato na sasa mwakani huko Bima ya Afya mnataka makato yaongezwe.

Hivi watu hao watasema maisha marahisi kweli. Au huo ndio urahisi wenyewe katika serikali ya awamu hii. Badala ya kuongeza mishahara Matokeo yake inaongezwa Makato kwa kale kale kamshahara kadogo.

Watumishi wa Umma watasema maisha ni marahisi kweli. Au watasema hujabana pesa. Au nao hawafanyi kazi. Au nao wanakaa vijiweni. Au ni jambo gani sasa.

Mhe. Rais hata kama wengine hawatasema lakini ukweli utabaki pale pale. Maisha umeyafanya kuwa magumu sana tofauti na awali.

Kama kuna kundi linanufaika na awamu hii basi kundi hilo halifiki watu laki moja. Kundi kubwa la watu mambo ni moto.

Vijana wengi wanalipwa mishahara kidogo sana mpaka uwezo wao wa kufikiri umefubaa. Ndio maana kila unapoongea hata ukiwatukana wanakupigia makofi wakikushangilia.

Mhe. Rais nakusihi usipuuzie Watanzania kwa kile wanachokuambia. Vaa viatu vyao hata kama soli za viatu vyao zimepinda.

Mtu analipwa laki moja kwa mwezi. Embu nambie mtu huyo hako kamshahara anakafanyia nini. Mtu ana mke na watoto. Amepanga chumba bado pesa ya kula hivi laki mbili inatosha nini.

Mhe. Rais huenda umesahau shida. Lakini Watanzania wengi wana ari ya kufana kazi lakini pesa hakuna. Na pesa haipo katika miktadha niliyoielezea hapo juu.

Labda kwa ufupi nikuelezee pesa haipo katika namna ifuatayo

● Mishahara ya watu wengi ni midogo. Huko kiwandani wanalipwa chini ya laki mbili. Tena Wanafanya kwenye makampuni ya watu matajiri wa taifa hili.

● Hujaongeza mishahara zaidi ya kuongeza makato katika mishahara hiyo hiyo midogo kwa Watumishi wa umma.

● Soko la Mazao ya kilimo ni janga. Tumeona kwenye Korosho, pamba, kahawa n.k.

Mhe. Rais nakusihi badili mtazamo kuhusu Watanzania wanaokuambia maisha ni magumu na hakuna pesa. Wanahoja ya msingi sana.

Sasa unapowaambia na kuwananga huku ukiwapiga vijembe unakuwa unakosea kwa kiasi kikubwa sana.

Usione wanakupigia Makofi lakini ukweli wanaomoyoni.

Ushauri,
●Ongeza watumishi mishahara kuingiza pesa mtaani.
●Ajiri vijana wasomi waliokata tamaa na awamu yako ambayo wanaiona haina maana. Yaani vijana hawa nakuambia kuwa wakisikia umejiuzulu hata kesho wataweka muziki. Vijana hawa wanakuona wewe ndio adui wa ndoto zao. Hilo ndilo ukweli.

●Sekta binafsi wasimamie waongeze mishahara wa wafanyakazi wao. Walipwe angalau kima cha chini laki 3.5.

Ni matumaini yangu nasaha zangu utazipokea na kuzifanyia kazi kwa kadiri itakavyompendeza Mungu.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
hana ujanja wa kuachia hiyo hela nchi imemshinda na haina kitu!
 
Ukiwa mjinga na pumbavu Kama wewe ku*ma ulivyo unakuwa hujui kuunda hoja, unamuunga mkono kafanya nini na maumivu yako kiuchumi yametokana na nini na kwa nini uishiwe badala ya kusonga mbele, mbwa ku*ma wewe, kuna watu mlikuja kuijaza Dunia, huna faida yoyote punguani wahedi wewe

Duh..!
Mkuu kunywa juisi ya ukwaju.
 
Hebu mkuu dadavua kidogo juu ya hii "nguvu hasi" inavyofanya kazi. Nafikiri ni aina ya athari ya kisaikologia. Nikiri kwamba hata mimi nina hisia kama wewe kuhusiana na yale niyaonayo kwa jiwe anapokuwa mitaani dhidi ya watu.
katika maisha yetu ya kila siku , kuna mambo ambayo tunayajaza kwenye akili zetu/mioyo yetu. Haya mambo yanaweza kuwa tunayachukua kwa kuangalia, kuwaza au hata kusikia.

Sasa katika taarifa unazozijaza kwenye ubongo nyingi ikiwa sio nzuri kuna uwezekano mhusika akawa affected katika utendaji wa mambo yake. Mara nyingi atatenda mambo ya ovyo ovyo kwa sababu moyo wake umejaza taarifa za ovyo ovyo. Hiyo tunaita nguvu hasi.

Inapotokea mtu akaujaza ubongo wake na taarifa nzuri zenye kuleta amani faraja upendo na matumaini hata matendo yake yatadhihirisha uwepo wa mambo hayo. Na hiyo tunaita nguvu chanya.

Ili uwe mtu wa nguvu chanya unatakiwa kujiepusha na kishawishi chochote kinachokuletea nguvu hasi akilini mwako.
 
Back
Top Bottom