Rais Magufuli naomba abadilike amalizie awe hivi

mtoto wa mchungaji

JF-Expert Member
Oct 24, 2020
242
500
Sina haja ya kuzungumzia utendaji kazi wa Dkt. Magufuli kwani si Tanzania au Afrika tu, ni dunia nzima, leo kuanzia Latino mpaka Asia na kutoka Yulopa mpaka Amerika wote wanajua kuwa Afrika na hususani Tanzania kuna kisiki cha mpingo.

Ndugu zangu wanajamvi inawezekana vijana wadogo wasinielewe haraka lakini Tanzania na Afrika tumepata Raisi na kiongozi mweusi ndani na nje. Amebeba ule weusi wa ndani kabisa ndiyo maana anafanana na akina Mkwawa, Kinjekitile, Milambo na wengine wengi ambao waliukataa ubeberu, ugeni na utamaduni wa wazungu na hata Uarabu.

Sisi katika imani tunatafsili ujio wa Magufuli kama kazi ya Muzimu wa Wafrika.

Kuna vitu vingi ameonyesha kuwa yeye ni kama wale Ansesta wetu wa Afrika lakini kuna mambo mengine kayaacha nayo pia ni yamsingi. Mfano kutumia lugha yetu ya Kiswahili na kushawishi mataifa karibu yote ya Afrika kutumia Kiswahili hili amefanya. Na hii itaanza kuwafungua vijana wengi wa kibongo ambao wanaamini kuwa Kiingereza ndiyo supiria wakisahau kuwa kalne chache tu juzi Kilumi ndiyo kilikuwa Supiria na kiingereza hakikuwapo duniani zaidi ya pale kwa marikia. Hata Yesu yule mnazareti alilazimika kujifunza Kirumi hili aweze kuwasiliana na serikali ya Kaisalia. Lakini leo hakipo hadi ndani ya kanisa kimekufa.

Ambalo Magufuli ameliacha na ni la msingi ni uvaaji tu. Mimi ninamwomba Babalao aanze kuvaa kama mwafika tofauti na sasa anavyovaa kizungu muda wote, misuti na kujinyonga na vitambaa shingoni kama Dr Living Stone na Crlpeters (mkono wa damu) na wengine hii haileti maana.

Nashauri kama akishindwa kabisa basi avae kama Nelson Mandera yale mashati ya kijamaa na kama akishindwa kabisa basi avae kama Olugusen Obasanjo au hata kama Kanal Muhamal Gadafi hawa hawakuvaa tai kabisa. Na kama akishindwa kabisa basi amalizie kama Mrisho Mpoto.

Nimeamua kusema haya kwa sababu Magu, kwa sasa na hata vizazi vijavyo atabakia kuwa Icon ya bara la Afrika hivyo atazidi kutupa heshima Afrika kwa nguo tu, kwa maana utamaduni wetu utapata heshima na kurudi kuwa bora kuliko wa kizungu au wa kiarabu kama kanisa na Msikiti ilivyo kosea fungua milango ya tamaduni za kigeni azi ifu Afrika hatukuwa na mavazi. Nikweli Magufuli amefanya kazi kubwa sana katika Kiswahili na mambo mengine mengi mimi naomba aongeze na hili la kuvaa tu hili amalize kitu kikamilike.

Namaliza kwa kuwaomba washauri wa Rais wajaribu kumshahuri tena wasubiri akiwa ameturia amemaliza kula ule ugali wake wa muhogo aliosema anaupenda na samaki ndiyo wampe haya, hatochomoa.

Nawasilisha, Mtoto wa Mchungaji niliye lelewa na kukua kwa sadaka.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom