Rais Magufuli: Namshukuru ndugu Bashiru, Channel 10 tulinyang'anywa na kudhulumiwa

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,445
7,810
Leo Rais Magufuli amezindua jengo la Jitegemee linalomilikiwa na Chama cha Mapinduzi lililokarabatiwa, miongoni mwa taasisi zilizopo ndani ya ni studio mpya za AMGL zinazoendesha vituo vya Channel 10, Plus na Magic FM.

Baada ya uzinduzi huo, Rais Magufuli aliomba kuchagua mziki wake na kuchagua kibao cha Professa J.

"Kwahiyo nikitaka mziki wangu hapa unaweza ukapigwa! Mimi nataka mziki mmoja nafikiri umepigwa na Professa J unazungumzia mtu aliyekwenda kumsema baba yake na baba yake akamrudi vizuri, akasema nazungumza na wewe sijui unaitwaje huo wimbo?"

Rais Magufuli aliwekewa kibao cha Baba kilichoimbwa na Stamina akimshirikisha Prof J.

RAIS MAGUFULI: Sina maneno mengi lakini nimefurahi sana kupewa nafasi ya kuja kuzindua jengo hili, jengo zuri, ninawapongeza sana walioshiriki katika kufanya ukarabati wa jengo hili wakiongozwa na mzee Gachuma na kwa taarifa ambazo zimetolewa hapa, jengo hili lilikuwa likarabatiwe kwa bilioni 2 point something, limekarabatiwa kwa fedha nafikiri milioni 700 na kitu, huu ni ushujaa asanteni sana.

Lakini nashukuru sana kuona TV zetu, Channel 10, channel 10 plus, Magic na kadhalika. Vyombo hivi vilikuwa vya chama cha mapinduzi lakini palijitokeza hapa katikati kwa mfano channel 10 ikachukuliwa ikawa mali ya watu wengine, tulinyang'anywa na kudhulumiwa na ndio maana mimi namshukuru sana mheshimiwa Bashiru, nilipounda tume ya kuchunguza mali za chama cha mapinduzi, akaenda akaligundua hili na tukairudisha channel 10 ikawa ndani ya chama cha mapinduzi, kwahiyo mnaweza mkaona ni kwa namna gani ufisadi ulikuwa umeota mizizi hata vyombo vya chama cha mapinduzi vilikuwa vinapotea bila hesabu.
 
kavamia duka la vitenge na wapambe wake 4 anadai apewe milioni 100 tofauti na hapo anamfungulia kesi ya uhujumu uchumi.
Suala hili lilifikishwa kwa DC, RC na RPC alikuwa analifuatilia. Ikumbukwe sio mara yake ya kwanza hii.
Mkuu huyu mbona ni kawaida yake huyo hata wakubwa wake wanafahamu?
 
Back
Top Bottom