Rais Magufuli nakupongeza kwa hili; Fanya na hili baba...

Boeing

Senior Member
Apr 16, 2017
151
421
Nakuandikia nikiwa kama mwananchi wa kawaida. Naamini katika madhaifu na kutokukamilika kutokana na ubinadam wetu. Yapo mazuri na mabaya umefanya. Huo ndio ubinadam. Naamini tunajifunza kutokana na makosa, hivyo kadiri muda unavyokwenda utajisahihisha kwa Yale mabaya na hatimaye utafanya mengi mema.

Katika jambo ulilofanya na kufurahisha wengi ni hili la kufuta ada na michango mingine ya hovyo iliyofanya maskini ashindwe kumsomesha mtoto
wake.

Zipo Halmashauri kadhaa wazabuni kwa kushirikiana wa wakuu wa shule ambapo walikuwa wakipeana 10% wanafanya kutetea juu ya wanafunzi kula eti ndo wanafaulu. Kuna vikao vinafanyika na watetezi wa hilo jambo wanajitokeza kuhonga wakurugenzi na wakuu wa wilaya ili wakubali hili. Baadhi ya hili nitaleta mojawapo ya hiyo Halmashauri. Naomba katika hili uwe mkali sana mh. Baadhi ya wakuu wa shule wamehamishia suala la michango kwenye

*fedha za taaluma
*ulinzi
*uniform
*Ujenzi
*madawati
*tahadhari n.k

Ukicheki uwiano wa michango na utekelezaji ni vitu tofauti kbsa. Mfano mtoto mmoja anachajiwa 40000 za ulinzi, shule ina wanafunzi 500 na walinzi wawili tu!!!!!!

Mwanafunzi analipa 70000 ya uniform anapewa skirt 2,shati 2, na sweta 1, vitu ambavyo kwa kwa Fundi mwingine unaweza kupata kwa 40000 ila hawaruhusiwii! Wazazi wanaibiwa sana.

Baada ya kukataza michango hiyo baadhi ya wakuu wa shule wanataka kuchukulia kama kisingizio endapo kama itatokea wanafunzi wakafeli. Imefika mahali wakuu wa shule wanawaambia walimu wasiumize sana vichwa kwamba wakifeli ni jukumu la serikali.

Sasa mh Fanya hivi:
1. Shikilia suala la michango, kama itakuwepo ianishwe na serikali
2. Walimu wafundishe na wale watakaofelisha wakuu wao wawajibishwe ikiwezekana washushwe vyeo vyao. Kuna walimu wengi hawajaajiriwa na wanatafuta kazi.

HONGERA MH RAISI. RUDISHA HADHI YA SHULE ZA SERIKALI. UZEMBE NDIO UNAPELEKEA SHULE KUFELISHA NA LAWAMA KUIANGUKIA SERIKALI.

AKSANTE
 
Back
Top Bottom