RAIS MAGUFULI NAKUPA TANO

bulabo

JF-Expert Member
Aug 20, 2015
620
759
Rais Magufuli mwezi huu tunaelekea mwisho wa mwaka. Mimi nachukua nafasi hii kukupongeza kwa kazi nzuri...nakuombea kwa mwenyezi mungu uendelee hv hv bila kurudi nyuma. Mwaka tu mambo mengi umeyaweka sawa mfano shirika letu la ndege limerudi, heshima kazi sasa ipo, mtaani nako watu wana adabu ya matumizi ya pesa,utii wa sheria uko juu sasa, keki yetu tunaiona. Umeme haukatikikatiki ovyo kama zamani, kuwa na ndege sita ulizosema ni heko kwa sisi watz wazalendo.
Tumeona mambo unavyoyashugulikia bila aibu, bila uoga bila kumuonea mtu. Nchi yetu kidogo ilikuwa inaelekeaa kwenye matabaka mawili tajiri na masikini leo hii hata tajiri anaadabu fulani ambayo haikuwepo.

Kuna mambo mengi sana umeyafanya kwa muda wa mwaka mmoja huu japo binadamu wengine hata ukiwapa nyumba bado wataendelea kuona kama hakuna jema. We endelea kuchapa kazi.

Nasema heko RAIS wetu najivunia leo kuitwa mtz hata nikiwa kenya uganda n.k leo hii tembo wetu hawauwawi ovyo ovyo. Matumizi serikalini yanaenda kwa nidhamu na kwa bajeti.

Tukiendelea hv hv TZ hii itakuwa mbali sana baada ya miaka 5.

Watz wenzangu tumuunge mkono rais wetu.

Tanzania kwanza. Vyama baadae
 
Tuko pamoja sana......big up kwa rais magufuri amejitoa kimasomaso na kizalendo kurejesha heshima ya taifa. Na heshima imerejea na itaongezeka.......kama wananchi wataridhia magufuri akae hata miaka 100 tuweke mambo sawa.
 
Hongera sana rais kwakazi nzuri mungu akujalie afya njema ili uendelee kutetea maslai ya taifa pasipo kuogopa au kumwonea aibu mtu,
 
Safi sana na wale wa ufipa wameamua kuachana na biashara yao ile, sasa wamebeba mimba wote
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom